Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 1,710
- 8,690
- Thread starter
-
- #61
Yaani humu napata changamoto moja kujibu hoja zenu, najadili na watoa huduma hizi waliosajili huduma zao kwa mujibu wa sheria au watoa huduma bubu bila usajili? Au wamesajili ila hawakuisoma Sheria yenyewe?Huyo mtoto akisha soma na akafanikiwa utampelekea pesa ya Shukrani huyo mwenye gari ambaye alikuwa anakubebea mtoto wako bei sawa na bure?
Wenda ww ndo khanisi unaye penda vya dezo, hiyo gari imenunuliwa kwa hela, inahitaji matengenezo, inahitaji mafuta,inahitaji kulipiwa bima, inahitaji kulipiwa kodi, inahitaji hela ya kuoshwa,inahitaji pesa ya mlinzi wa kuilinda ina hitaji pesa ya kumlipa direva, inahitaji pesa ya kumlipa kinda, na bosi mwenye gari apate faida.
Kama mnataka dezo iambie serikali tako iwalipe ruzuku hao wamiliki wa mabasi badala ya kununua mav8 au wapeni watoto wenu pesa iliyo kamilika,kama huwezi mtafutie mtoto shule ya karibu na nyumbani.
Watoto uwazae mwenyewe kwenye majukumu utake usaidiwe na wengine?
Ya huduma za kusafirisha abiriaShughuli gani mayoo wane
Njia rahisi ni kuwapa ruzuku wenye magari ya abiria , hakuna hata mmoja angemuacha mwanafunzi.Kiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
Kasome sasa Sheria yako kisha uulize kwa kurejea vifungu halafu LATRA watakuja na elimu husika kwa kinaKwahiyo kwa kuwa imesajiriwa ndo nini? Na huo usajiri wa hizo dala dala ni kubeba abiria, au wanafunzi?
Nasubiri jibu.
Nakuhakikishia hili hamtofanikiwa wala tusiwe wanafikiSasa hayo maoni si ndiyo Sasa arudi kwa msajili? Asiporudi akaanza tu kuvunja Sheria unadhani akishtakiwa Sheria itamwacha? Hebu na wewe tafakari
Kuna mtu kuna umoja au shirikisho la watoa huduma hizi, kama ni hivyo, kwenye ajenda za kutoa maoni si haya ndiyo mngekuwa mnawasilisha kwenye mamlaka ya usajiliNjia rahisi ni kuwapa ruzuku wenye magari ya abiria , hakuna hata mmoja angemuacha mwanafunzi.
Mimi natoka bunju kuja makumbusho mara nyingi, kiasi cha wanafunzi waliopo njiani hao makondakta wakiamua kuwapakia kesho hawataingiza gari barabarani.
Uzuri hapo namba za msajili mmeziona, ilikuwa vema kuwa na utaratibu wa kutoa maoni, jamii inajengwa kwa maoni ya pande zote siyo kwa kuvunja sheriaNaongelea angle moja tu.
Ile chenji ya 1,000 inauzwa kwa 800.
Ukimpakia mwanafunzi kwa nauli ya 200 halafu akakupa 1000 na ukamrudishia chenji yake ya shilingi 800, hapo tafsiri ni kwamba amepanda bure kabisa.
Sisi watu wazima wenyewe kuna muda makonda sehemu ya nauli 600 inabidi watukate 500 kwa sababu hawana chenji. Mfano abiria wa ruti fupi mfano Masaki-Simu 2000 ambapo nauli ni 600 lakini makondakta huwa wanapokea 500 kwa sababu ya uhaba wa chenji.
Sasa fikiria kwenye gari kama hilo watu abiria watu wazima umewafanyia punguzo la 100 halafu umebeba wanafunzi 8 na jioni inabidi hesabu itimie.
Tusiangalie upande mmoja.
Kwani mama, unaposisitiza sheria lazima ifuatwe; kuna sheria inamkataza au i amlazimisha konda kubeba wanafunzi? Konda na dereva reserve the rights to board any passenger at their own discretion. Wanaweza kunikataa hata mimi mtu mzima na nauli yangu kamili. Sio kosa kisheria.Hujambo? Nikuambie jambo ? Maboresho yanapokuwa yanaendelea kwenye eneo lolote , huwa hayafuti Sheria iliyopo kazini hadi hapo Sheria husika itakapofutwa au kubadilishwa. Sasa ni muhimu sana pamoja na maoni tuwe tunakumbuka kutimiza wajibu wa sheria ambayo Iko wakati huo. Ahsante Sana
Mkuu, unataka miili ya watoto izagae huko mabarabarani?wazazi walazimishwe kununua baiskel kwa wanafunzi wao itapunguza tatizo kwa kiasi flani.
Huyo anaongea tu hamna anachoelewa unatumia tu nguvu kumweleweshaUhalisia wa mtaani hauko hivo
Boss anakubali hayo masharti lakini kondakta anapewa gari na huo mzigo wa kulipia halafu umpe wanafunzi walipe 200 yeye ataishije
Mimi nikapenda nikushauri kuwa, ukiwa kwenye mfumo wa huduma ambayo umeisajili, unakuwa pia na uhuru wa kutoa maoni kwenye taasisi rasmi ya usajili.Kwani mama, unaposisitiza sheria lazima ifuatwe; kuna sheria inamkataza au i amlazimisha konda kubeba wanafunzi? Konda na dereva reserve the rights to board any passenger at their own discretion. Wanaweza kunikataa hata mimi mtu mzima na nauli yangu kamili. Sio kosa kisheria.
Tukubali tu, kuna tatizo kubwa la kimamlaka; raia wanateseke, watoto ambao wazazi wao wanapigwa TOZO kila mahali....wanateseka huku viongozi mnaogelea kwenye raha. V8 serikali inaweza kuzinunua na kuzimantain, ila bus za wanafunzi haiwezi?
Wewe ni waziri wa makundi maluum. Kuna sababu gani za msingi mtoto wa Mbagala mnampangia shule ya kusoma Kurasini? Matatizo mengine mnayatengeneza wenyewe.
Serikali imejenga barabara za mwendokasi, miaka inakatika mradi uko dhooful haali. Sasa kama serikali haikujiandaa walijenga za nini?
Sijui huwa mnamshauri nini Mh. Rais huko vikaoni.
Piga simu hapo LATRA waulize hivi; jamani Mimi nilisajili huduma yangu kwa mujibu wa sheria ila sasa sijui Sheria yenyewe na kanuni zake au sema umesahau hivyo unaomba elimu kuhusu wajibu wako kwa abiria wa makundi mbalimbali. Hakika watakupa elimu safi kabisaKwahiyo kwa kuwa imesajiriwa ndo nini? Na huo usajiri wa hizo dala dala ni kubeba abiria, au wanafunzi?
Nasubiri jibu.
Mimi nimeshuhudia mateso ya Wanafunzi kugombania daladala ni muhanga pia maana nilikuwa nasoma mbali na ilikuwa hakuna namna zaidi ya kupanda Daladala.Kiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
wazo lako zuri sana mkuu lakini kwa serikali hii ni ndoto kutimia hilo japo uwezo wanao wakiamua..si uliona ccm kwenye ule mkutano wao wa majuzi dodoma mabasi mengi makubwa tena mapya yamenunuliwa kwa ajili ya kubeba machawa wa mama.! jayo ndo mambo serikali yako inayapa kipaumbile..hizo habari za wanafunzi watajijua wenyewe.Hivi Mama, huko kwenye vikao vyenu hamkuwahi kujadili Serikali kununua mabus yakutosha mkoa wa Dar es salaam kwa ajili ya Wanafunzi tu na wazazi wawe wanachangia kiasi fulani labda monthly.
Hii kero ipo miaka nenda rudi toka enzi zile za Tambaza mpaka Leo hapo Dar bado kunashida ya usafiri wa Wanafunzi tu, inamaana mpaka Leo hatuna solution?
Mama shida nyingine kuubwa mashule ya vijijini huko unakuta watoto wako kwenye highway wanaomba lift kwenye malori na magari yanayopita matokeo yake watoto wa kike wanakuwa kwenye hatari kwa hawa wahuni wa malori, na wengine.
Huko mawilayani kutokana na mashule kuwa mbali bodaboda wamekuwa ndio waume sasa wa mabinti. (Hatari sana)
Hili suala la usafiri wa Wanafunzi msiishie tu Dar es salaam hata mikoani sasa mnahitaji kuumiza kichwa, kwangu mimi naona suluhu ni Serikali kuanza school buses kuanzia kwenye miji mpaka mawilayani na vijijini huko.
Kwenye hizi highways mabus ya Wanafunzi yawe yanazungukuka muda wa kuingia na muda wa kutoka.
Kila Mkoa kwenye highways zake unakuwa na mabus yake maana tuna miji mingi mabarabarani, wilayani pia kila kwenye population kubwa inawekwa bus..nk
Huu umbali wanaotembea hawa watoto naamini hata upeo wao unakuwa mdogo mashuleni huko.
Mheshimiwa mimi ninaheshimu sana juhudi zako kutetea jamii .Na ushauri wangu ni kuwa, nyie watoa huduma naamini mliisoma Sheria kuhusu usajili wa huduma zenu hivyo, mnao wajibu wa kwenda kwa msajili na kusema, tuna hoja na ushauri na mapendekezo. Mimi kwa nafasi yangu kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Makundi maalumu, huwa natumia muda kuelimisha jamii yote kadri hoja zinavyonifikia. Ahsante Sana kwa ushirikiano wako/wenu
Hiyo route imesajiliwa lini LATRA?Ukitaka kushuhudia ngumi za konda na wanafunzi
Ruti ya tandika kwa mparange to mbande
Huwa ni 1000
Mwanafunzi hapandi hata akiletwa na ving’ora vya serikali
Sababu kuu wanasema ruti ina mabao kama yote
Mpaka ufike mbande 5000-10,000 unaiacha njiani
Afu unapakiaje wakusoma
Kwa ruti hii makarao wanachangia watoto wasipakiwe
Sasa inabidi nikupeleke tu kwa kuwa ndiyo wenye dhamana na Sheria hiyo, nikisema nibebe dhamana nitakosea Sheria. Mojawapo ya jukumu la Wizara ninayoisimamia kama Waziri wa Jamii na Makundi yake maalumu ni pamoja na kuwaelimisha jamii kuhusu wapi waende kwenye wizara mahsusi kwa ajili ya huduma fulani. Mfano, nikisema jamani wapelekeni watoto shuleni wakapate elimu, nakuwa sina tena wajibu wa kuanza kuelezea kuhusu mitaala ya masomo maana huo ni wajibu mahsusi wa waziri wa elimu. Ahsante SanaUsinipeleke kwa LATRA, hapa niko na wewe, nikishamalizana na wee, nitaenda huko kwa LATRA, na nita deal nao vile ambayo hiyo sheria na vifungu vyake vinataka.
Nasubiri Jibu mheshimiwa.
Serikali itambue daladala ni biashara na iheshimu hiyo biasharaMimi nimeshuhudia mateso ya Wanafunzi kugombania daladala ni muhanga pia maana nilikuwa nasoma mbali na ilikuwa hakuna namna zaidi ya kupanda Daladala.
Kwa kweli Wanafunzi tunapata tabu na kuteseka mno , kutoka na ukweli kwamba asilimia kubwa ya Makondakta hawawataki kabisa Wanafunzi wanaona kama Virus , sometimes unakuta gari halina Wanafunzi kabisa lakini ameshajiwekea Sheria yake binafsi kuwa hapakii Wanafunzi na kuwasukuma mlangoni.
Laiti wangekuwa na utaratibu wa kuchukua at least Wanafunzi 5 , au 10 kwa kila gari ingesaidia sana ila tatizo wengi wanawakataa Moja kwa Moja au kuchukua wawili tu wakuzugia .