Wasaalam,
Kule x kuna hoja kwamba, baadhi ya "makonda" wa ma Bus ya abiria wanazuiwa wanafunzi kupanda ma Bus hayo.
Tangu kuja kwangu iliambatana na ujumbe uliokuwa umetumwa kwenda kwa
CarolNdosi na uliosomeka "Carol , naomba usaidie hili, moja ya changamoto kuubwa ni wanafunzi kupanda daladala sijui ni sheria ipi inaruhusu konda kuaamua kupakia au kutopakia, kiufupi wakinamama wanaopeleka watoto wao asubuhi vituoni wanapitia shida sana"
Baada ya kuwasiliana na taasisi ya udhibiti (LATRA) na kwa kuzingatia kuwa, changamoto hii huenda inawakumba wazazi wengi, naomba kutoa mrejesho kwa majukwaa yote kuwa; Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi na kinachotakiwa ni Wazazi hao watoe taarifa LATRA waambatishe na namba ya gari husika. Namba ya LATRA hiyo hapo.
Ahsanteni kwa ushirikiano, tuwalinde watoto wetu🇹🇿
Shukrani kwa
CarolNdosi kwa ushirikiano. Mkurugenzi @latra_tz ahsante kwa ushirikiano.
Naona suala hili limekuwa ni Ajenda ya Kisiasa ambayo imekuwa ikijadiliwa mara nyingi sana miaka nenda rudi Bila ya kupatikana kwa Suluhu ya maana.
Kwa maoni yangu, kiini au root cause ya kuibuka kwa janga hili kubwa sana hapa nchini ni Serikali yenyewe. Serikali ndio ambayo imeasisi janga hili kutokana na kuwa na Sera mbaya katika Utawala wa nchi sambamba na kukosa Mipango Mikakati iliyo madhubuti, ya muda mfupi na ya muda mrefu yenye lengo la kutatua changamoto za kijamii ikiwamo na hii changamoto ya Usafiri na Usafirishaji.
Mhe. Waziri, nyinyi kama Serikali, Je, mmeshawahi kufanya Utafiti katika nchi zingine ili kujua wenzetu kwenye hizo nchi zao wamewezaje kuondokana na hili tatizo la Usafiri kwa watoto wa shule? Je, mmeshawahi KUFANYA Utafiti wa namna hii?
Sera mbovu Sana za Siasa mbaya za Ujamaa ndio kichocheo kikubwa Cha kuwepo kwa Janga hili, mnachanganya Mambo ya biashara katika muktadha wa dhana mbili tofaufi kabisa ambazo kamwe haziwezi kuchangangwa kwa pamoja: Biashara ya Soko Huria katika dunia ya Ushindani wa kibiashara na Soko HOLELA katika dunia ya kufikirika ya Siasa za Ujamaa.
Usafirishaji Abiria ni Ajira au KAZI kama kazi nyingine yoyote ile yenye kulenga kupata Ujira au Mshahara kupitia makusanyo ya Nauli kutoka kwa Abiria. Hao Makonda na Madereva pia wanalenga kupata faida kutokana na hiyo biashara yao.
Tuachane na dhana potofu za Itikadi za Siasa za Ujamaa, tuishi katika dunia ya Uhalisia.
Wanafunzi, Wanajeshi pamoja na watu wengine ambao wamepewa exemption ya kulipa nauli katika Usafiri wa umma wanapaswa walipe nauli yao kamili.
Wanafunzi wasiokuwa na mshahara wanalipa nauli ndogo ya Shilingi 200/=, huku Askari na Wanajeshi wenye Mishahara na marupurupu hawalipi nauli kabisa, Je, wewe kama Waziri unaona jambo hili liko sawa sawa???
Je, wewe binafsi upo tayari kila mwezi kutoa kutoka sehemu ya fedha za mshahara wako na posho unazopata Kuwapa Watoto Yatima au Kuwapa Watu wengine wenye hali ngumu za kimaisha? Upo tayari kufanya hivyo?
Kwa Nini Basi Makondakta na Madereva wa daladala walazimishwe kufanya hivyo ukizingatia kwamba wapo baadhi ya hao Wanafunzi wazazi wao Wana vipato vikubwa vya kutosha?? Hoja ya msingi hasa ni Nini kwenye suala hili????