Hebu twende taratibu, kwani hapa hii mada si umeleta wee? Mie nataka tujadili na wee, hao LATRA nitawafuata kwa wakati mwingine na kwa matakwa yangu.Piga simu hapo LATRA waulize hivi; jamani Mimi nilisajili huduma yangu kwa mujibu wa sheria ila sasa sijui Sheria yenyewe na kanuni zake au sema umesahau hivyo unaomba elimu kuhusu wajibu wako kwa abiria wa makundi mbalimbali. Hakika watakupa elimu safi kabisa
Ahsante Sana kwa maoni yako. Sasa huwa ni hivi, mfano sisi huku wizara ya maendeleo ya jamii tunasajili NGOs mbalimbali. Kuna forums kabisa za sisi kukutana na hizo NGOs na kupokea maoni yao. Hivyo hivyo na sisi kuwapa elimu wakati wanasajiliwa na vitendea kazi. Hivyo hivyo na kwa ofisi za wasajili wengine hufanya. Sasa iwapo LATRA wametangaza na simu hizo hapo, maana yake wanataka mawasiliano na jamii na watoa huduma pia. Na uzuri hizo simu zinarekodi na taarifa kwa kumbukumbu, nilidhani sasa, ni wakati wa kutoa maoni haya Ili mshirikiane vema kufikia uelewa wa pamoja. Sasa taasisi inatoa namba zake ambazo labda wengine walikuwa hawazijui, je siyo kwamba ni hatua nzuri zaidi?Mheshimiwa mimi ninaheshimu sana juhudi zako kutetea jamii .
LAKINI KATIKA HILI
mangiaji namba 2 ngara23 ameeleza vizuri sana.
1. Jukumu zito la kuhudumia wanafunzi ameachiwa kondakta na Serikali kujiweka kando kwa kigezo cha sheria.
2. Huyu konda wengi hawajasoma lkn mmebebesha jukumu la kusaidia wanafunzi.
3. Unaposema akalalamike LATRA mnyonge huyu atasikikizwa na nani?
USHAURI
Hayo magari yafikiriwe kupewa ruzuku waweze kujiendesha
Wasaalam,
Kule x kuna hoja kwamba, baadhi ya "makonda" wa ma Bus ya abiria wanazuiwa wanafunzi kupanda ma Bus hayo.
Tangu kuja kwangu iliambatana na ujumbe uliokuwa umetumwa kwenda kwa CarolNdosi na uliosomeka "Carol , naomba usaidie hili, moja ya changamoto kuubwa ni wanafunzi kupanda daladala sijui ni sheria ipi inaruhusu konda kuaamua kupakia au kutopakia, kiufupi wakinamama wanaopeleka watoto wao asubuhi vituoni wanapitia shida sana"
Baada ya kuwasiliana na taasisi ya udhibiti (LATRA) na kwa kuzingatia kuwa, changamoto hii huenda inawakumba wazazi wengi, naomba kutoa mrejesho kwa majukwaa yote kuwa; Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi na kinachotakiwa ni Wazazi hao watoe taarifa LATRA waambatishe na namba ya gari husika. Namba ya LATRA hiyo hapo.
Ahsanteni kwa ushirikiano, tuwalinde watoto wetu🇹🇿
Shukrani kwa CarolNdosi kwa ushirikiano. Mkurugenzi @latra_tz ahsante kwa ushirikiano.
Kama zanzibar mbona search tuKiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
Hata ww muheshimiwa unaweza kupeleka pendekezo hilo kwenye mamlaka husika ili kuondoa kero hii, serikali ikianza kuwalipa ruzuku hao wenye magari hili jambo linaisha.Hujambo? Pamoja na maoni haya ambayo naamini LATRA watasoma, tukumbuke pia kuwa, tukishasajili huduma zetu, tunakuwa tumekubali kuwajibika kwa sheria iliyotusajili. Aidha, pia tunakuwa na uhuru wa maoni kwenye taasisi iliyotusajili. Ahsante kwa mchango wako.
Issue sio maoni Mheshimiwa, hapo ni nyie serikali badala kulazimisha sana muone ni namna gani mtawasidia.Kuna mtu kuna umoja au shirikisho la watoa huduma hizi, kama ni hivyo, kwenye ajenda za kutoa maoni si haya ndiyo mngekuwa mnawasilisha kwenye mamlaka ya usajili
Uzuri hapo namba za msajili mmeziona, ilikuwa vema kuwa na utaratibu wa kutoa maoni, jamii inajengwa kwa maoni ya pande zote siyo kwa kuvunja sheria
Wee ndo inatakiwa uwaeleze, sio mitaala ya masomo, Bali ni mfumo mzima wa Elimu ambayo wanatakiwa wakapate shuleni huko.Sasa inabidi nikupeleke tu kwa kuwa ndiyo wenye dhamana na Sheria hiyo, nikisema nibebe dhamana nitakosea Sheria. Mojawapo ya jukumu la Wizara ninayoisimamia kama Waziri wa Jamii na Makundi yake maalumu ni pamoja na kuwaelimisha jamii kuhusu wapi waende kwenye wizara mahsusi kwa ajili ya huduma fulani. Mfano, nikisema jamani wapelekeni watoto shuleni wakapate elimu, nakuwa sina tena wajibu wa kuanza kuelezea kuhusu mitaala ya masomo maana huo ni wajibu mahsusi wa waziri wa elimu. Ahsante Sana
Sasa hakuna mjadala usio na mwisho kulingana na malengo ya mleta hoja. Fanya kuwa nimeleta hoja yangu kwa lengo la kujibu hoja ya aliyeniTag na kuelimisha jamii kuhusu uwepo wa fursa ya mawasiliano ya jamii na taasisi ya huduma hizo za kijamii. Ukihitaji mjadala zaidi, subiri sasa atakayetumia hizo namba za LATRA kuwasilisha malalamiko iwapo yatakuhusu, utaalikwa kule mkajadili kwa kina. Mimi lengo langu ilikuwa kusambaza taarifa kwa jamii kuhusu uwepo wa kituo cha mawasiliano na jamii kama ninavyosambaza za wizara zingine zote pale inapotokea mwananchi amekuja kwangu. Zaidi ya hapoz ubarikiwe ✍🏻 usiku mwema.Hebu twende taratibu, kwani hapa hii mada si umeleta wee? Mie nataka tujadili na wee, hao LATRA nitawafuata kwa wakati mwingine na kwa matakwa yangu.
Ni vema wee ndo unatakiwa uambatanishe hapa hizo sheria na kanuni zake, kwa niaba yao km ambavyo umeleta hii mada.
Sasa ikiwa unashindwa kuisapoti mada yako, basi kuna shida mahali.
Hawezi kukuelewaWee ndo inatakiwa uwaeleze, sio mitaala ya masomo, Bali ni mfumo mzima wa Elimu ambayo wanatakiwa wakapate shuleni huko.
Huwezi kukwepa hilo, ukiwa unachukua jukumu la wizara nyingine, basi dhamana uko nayo, na huwezi kosea sheria, kwani iko ndani ya uwezo wako.
Sichukui jukumu la Wizara ingine Bali majukumu ya wizara ya maendeleo ya jamii ni pamoja na kuelimisha jamii kuhusu Yale ya ujumla, soma historia ya maafisa maendeleo ya jamii utaona mchango wao kwenye maendeleo pasipo kuingia kwenye umahsusi wa kisekta. Mfano, huduma za Dawati la jinsia ziko vituo vya Polisi, je hujaona maafisa ustawi wa jamii wakiwaeleza jamii kuwa, ukiona ukatili toa taarifa Dawati hilo? Je kwa kufanya hivyo ndiyo wanageuka maafisa Polisi?Wee ndo inatakiwa uwaeleze, sio mitaala ya masomo, Bali ni mfumo mzima wa Elimu ambayo wanatakiwa wakapate shuleni huko.
Huwezi kukwepa hilo, ukiwa unachukua jukumu la wizara nyingine, basi dhamana uko nayo, na huwezi kosea sheria, kwani iko ndani ya uwezo wako.
Ataelewa tu.Hawezi kukuelewa
Nadhani iundwe seraKwanini magari ya serikali , STM, STN, STL, DFPA, DFP, SU, PT, nk hayawachukui wanafunzi?
Na ndo kinachosababisha waone ugumu kupakia wanafunziKiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
Hao maafisa ustawi wa jamii, wanaishia kusema "ukiona ukatili toa taarifa kwa dawati la jinsia" pasipo kueleza nini ni ukatili? Na kwa kutaja baadhi ya matendo ambayo ni ukatili? Na waende huko wakapate haki au stahiki kutokana na ukatili huo?Sichukui jukumu la Wizara ingine Bali majukumu ya wizara ya maendeleo ya jamii ni pamoja na kuelimisha jamii kuhusu Yale ya ujumla, soma historia ya maafisa maendeleo ya jamii utaona mchango wao kwenye maendeleo pasipo kuingia kwenye umahsusi wa kisekta. Mfano, huduma za Dawati la jinsia ziko vituo vya Polisi, je hujaona maafisa ustawi wa jamii wakiwaeleza jamii kuwa, ukiona ukatili toa taarifa Dawati hilo? Je kwa kufanya hivyo ndiyo wanageuka maafisa Polisi?
Lc 300 ndo kipaumbele hizo school bus sio muhimu kwa sasa teheeeeeHivi Mama, huko kwenye vikao vyenu hamkuwahi kujadili Serikali kununua mabus yakutosha mkoa wa Dar es salaam kwa ajili ya Wanafunzi tu na wazazi wawe wanachangia kiasi fulani labda monthly.
Hii kero ipo miaka nenda rudi toka enzi zile za Tambaza mpaka Leo hapo Dar bado kunashida ya usafiri wa Wanafunzi tu, inamaana mpaka Leo hatuna solution?
Mama shida nyingine kuubwa mashule ya vijijini huko unakuta watoto wako kwenye highway wanaomba lift kwenye malori na magari yanayopita matokeo yake watoto wa kike wanakuwa kwenye hatari kwa hawa wahuni wa malori, na wengine.
Huko mawilayani kutokana na mashule kuwa mbali bodaboda wamekuwa ndio waume sasa wa mabinti. (Hatari sana)
Hili suala la usafiri wa Wanafunzi msiishie tu Dar es salaam hata mikoani sasa mnahitaji kuumiza kichwa, kwangu mimi naona suluhu ni Serikali kuanza school buses kuanzia kwenye miji mpaka mawilayani na vijijini huko.
Kwenye hizi highways mabus ya Wanafunzi yawe yanazungukuka muda wa kuingia na muda wa kutoka.
Kila Mkoa kwenye highways zake unakuwa na mabus yake maana tuna miji mingi mabarabarani, wilayani pia kila kwenye population kubwa inawekwa bus..nk
Huu umbali wanaotembea hawa watoto naamini hata upeo wao unakuwa mdogo mashuleni huko.
Sheria na Haki sio necessarily the same thing kuna sheria kandamizi, kuna sheria ambazo sio sustainable na sheria nyingi zimekaa kisiasa.., kwahio tutakuwa kama maroboti kusoma sheria na kutaka kuzisimamia kama vipofu bila kujadiliana kuboresha kilichopo na ni vipi kinafanya au hakifanyi kazi... (Au nyie watunga Sera wawakilishi wetu kupeleka / kuchukua mawazo yetu katika utungaji wenu wa Sera)Yaani humu napata changamoto moja kujibu hoja zenu, najadili na watoa huduma hizi waliosajili huduma zao kwa mujibu wa sheria au watoa huduma bubu bila usajili? Au wamesajili ila hawakuisoma Sheria yenyewe?
Nisaidie hapo ufafanuzi kwanza Ili nijue naelimisha akina nani tafadhali
waache kununua mabus ya kampeni wakununulie school bus?[emoji28] Ccm ife kwanza, but dada yangu Dkt. Gwajima D abaki hapo hapo kwenye hii wizara aliopo sasa, tunampenda sana mchapa kazi huyu.Kwanin serikali isinunue mabasi special kwa ajili ya wanafunzi?
Yanawekewa utaratiby tu wa muda wa kiwakusanya na kuwapeleka. Pia mda wa kuwachukua.
Serikali inatenga fungu la kuyahudumia magar hayo maana hayatakua na jam kubwa. Yanapita asubuh na jioni.
Kwanza itachangia mahudhurio kuongezeka mashuleni.
Hela ipo, kodi zetu zipo.
Mimi sijambo kabisa, hofu na mashaka ni kwako uliye mbali na upeo wa majicho yangu 👁️ 👀.Hao maafisa ustawi wa jamii, wanaishia kusema "ukiona ukatili toa taarifa kwa dawati la jinsia" pasipo kueleza nini ni ukatili? Na kwa kutaja baadhi ya matendo ambayo ni ukatili? Na waende huko wakapate haki au stahiki kutokana na ukatili huo?
Hawawi maafisa polisi, ila wanachukua majukumu, hujambo lakini?