Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Mbona serikali haiamuru wanafunzi kula mgahawani Bure? Kwani watoto hawapati njaa shuleni
Kwanini serikali iwaonee daladala, serikali haijui hii ni biashara
Msimamo wangu: ili kuepuka usumbu wanafunzi walipe nauli kamili
Ni mfano halali kabisa. Pia watoto wapewe sare, viatu, daftari nk karibu na bure na wenye maduka!
 
Na mimi najiuliza swali moja: unaenda kusajili biashara, unasoma Sheria na kanuni unaelewa kuwa, kwa utaratibu huu hapa sitapata faida, bado unasajili na maoni hutoi wala ushauri, unaingia kwenye mkataba wa kisheria kwa huduma hiyo halafu unaenda kutekeleza unakiuka Sheria, watu wanakulalamikia, unasema msinilalamikie..... Jamani kwani hii inaitwaje jamani? 😁
Wee mama Vicky unajificha kwenye kichaka cha usajiri, sheria na kanuni zake. Ili kuitetea serikali, kwa kua wee unalamba asali.

Chukua maoni hapa, wapelekee wahusika huko, hakuna kuogopana, ukweli lazima tuseme. Iwe unataka au hutaki, habari ndo hiyo
 
Wazazi tusikwepe wajibu wetu, na tukipigania unafuu, basi tuiandame serikali, sio wafanyabiashara!
 
Pia,
Wazazi tuwapeleke watoto wetu shule zilizo karibu na maeneo yetu, kwasasa shule za kata zipo karibu kila kata hasa za Dar es Salaam lakini mzazi unachagua shule za mbali hasa kwa hawa watoto wa primary...wanafika wamechoka hata uwezo wake wa kufikiri unapungua
 
Wee mama Vicky unajificha kwenye kichaka cha usajiri, sheria na kanuni zake. Ili kuitetea serikali, kwa kua wee unalamba asali.

Chukua maoni hapa, wapelekee wahusika huko, hakuna kuogopana, ukweli lazima tuseme. Iwe unataka au hutaki, habari ndo hiyo
Hatari sana hawa latra wangetusaidia huku daladala hizi muda wa abiria wengi, zinajibanza nyuma kidogo ya vituo rasmi ili watupige bei kubwa kwa lengo la kupata siti. Hii changamoto ya miaka
 
Hatari sana hawa latra wangetusaidia huku daladala hizi muda wa abiria wengi, zinajibanza nyuma kidogo ya vituo rasmi ili watupige bei kubwa kwa lengo la kupata siti. Hii changamoto ya miaka
Hili tutajadili siku nyingine, leo tuko na suala la ubebaji wa wanafunzi kwenye dala dala.
 
Afadhali yako dk ukiulizwa jambo mtandaoni huwa unatafuta majibu na kuyaleta hata kama wakikubeza lakn unajua kuleta mrejesho kwa kile ulichokipata..
WENGNE SASA, HAWAONEKANI, HUTUMA MACHAWA NA KUJA KUTUKANA WATU NA KUPIGA MAPAMBIO.
ubarikiwe mh waziri.
 
Wee mama Vicky unajificha kwenye kichaka cha usajiri, sheria na kanuni zake. Ili kuitetea serikali, kwa kua wee unalamba asali.

Chukua maoni hapa, wapelekee wahusika huko, hakuna kuogopana, ukweli lazima tuseme. Iwe unataka au hutaki, habari ndo hiyo
cocastic bhana😅
 
Maoni hata wewe unaweza kuyapeleka tu moja kwa moja Ili yabaki original bila usanifu. Namba zenyewe kwa urahisi wako ndiyo hizo hapo tafadhali
 
Ni kweli kabisa maoni ni hatua endelevu na hapa sasa mmejua na mawasiliano ya kituo cha LATRA nadhani sasa ni kuendelea kutoa mrejesho moja kwa moja. Ahsante Sana kwa muda wako.
Katika hili nakupongeza Mhe Waziri kwa kufanyika daraja na kutoa majibu ya maswali japo kwa ufupi hakika wewe ni kiongozi wa kuigwa , kama wizara zote zingekuwa na viongozi active kama wewe hakika Kuna lawama nyingne zingepungua katika jamii. Chukua maua yako
 
Hawezi kujibu hili, kuna swali nilimuuliza jana hajajibu hadi sahivi, na nilitaka ajibu ili tubambane zaidi, kaamua kukimbia.

😂😂😂😂😂
Siyo lazima nijibu Kila kitu kwa kuwa haya ni maoni na siyo mahakamani ambako lazima ujibu hivyo, kama unayo mengine tiririka tu kwa kumbukumbu na matumizi ya baadae tafadhali 🤗
 
Katika hili nakupongeza Mhe Waziri kwa kufanyika daraja na kutoa majibu ya maswali japo kwa ufupi hakika wewe ni kiongozi wa kuigwa , kama wizara zote zingekuwa na viongozi active kama wewe hakika Kuna lawama nyingne zingepungua katika jamii. Chukua maua yako
Tuendelee kushirikiana daima na wale wa kuiga mazuri yangu machache Mungu awape Rehema ✍🏻
 
Hiyo route imesajiliwa lini LATRA?
NI route ya kufoji ingawa njia ipo nzuri tu, so polisi wana haki ya kuwakamata. Lakini kama ujuavyo, ukikamatwa huko unatoa chochote kitu unatembea.
Sio ruti rasmI
Ila inapunguza sana folen ya mbagala
 
Hapo kwenye bango kuna namba za LATRA, hebu katoe maoni tafadhali. Uwe na jioni njema ya Baraka ✍🏻🙏🏽
Ila Mheshimiwa mama Dorothy gwajima,hili suala ni very sensitive kwa upana wake ni muhimu wadau wanaohusika waelimishwe na sio kushurutishwa.
Tukichukua hoja ya mdau mmoja hapo juu ni kuwa hawa makonda wanakimbizana na hesabu ya boss kwa maana hiyo hawezi kuwaacha abiria akawabeba wanafunzi.

Pia Sera yetu ya elimu ni kama inawabeba zaidi wazazi kuliko hata Wanafunzi, wazazi hawalipi Ada hata senti kweli ashindwe kumpa mtoto nauli kamili...ukiwa kama waziri Mheshimiwa kwanini serikali inalea Aina hii ya ulemavu kwa wazazi?

Kila kitu kitolewe bure kweli hapo kuna elimu.
Kwanini wabunge wa majimbo husika wasilete magari yatakayo wasaidia hao Wanafunzi kwa gharama ya wazazi?

Any way kwa kuwa hii hoja ni suala mtambuka let's watch how it will end.
 
Back
Top Bottom