Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)
Hakuna uzimamizi wa sheria, wanaotakiwa kufanya hivyo wamelala, bodaboda hawavai helmet, gari mbovu ziko road, service road zimejaa biashara, jumlisha hili la kunyanyasa wanafunzi.

Wanaowajibika kusimamia na kutekeleza sheria, na sisi wananchi tuko kimya.
 
Siyo lazima nijibu Kila kitu kwa kuwa haya ni maoni na siyo mahakamani ambako lazima ujibu hivyo, kama unayo mengine tiririka tu kwa kumbukumbu na matumizi ya baadae tafadhali 🤗
Mie ukinijibu lile swali, basi ndo nitaendelea na mengine kutiririka. Maana ni muhimu lile swali kujibiwa na kutolewa ufafanuzi.
 
Maoni hata wewe unaweza kuyapeleka tu moja kwa moja Ili yabaki original bila usanifu. Namba zenyewe kwa urahisi wako ndiyo hizo hapo tafadhali
Sitaki maoni uyapeleke kwa LATRA, nataka uyapeleke huko Serikalini, kwenye vikao vya bunge, na baraza la mawaziri.

Najua umeelewa sasa.
 
Abiria pia tunachangia kwa kukalia kimya huu upuuzi wanaoufanya makondakta. Mi si mpandaji sana wa daladala ila mwezi uliopita nilipanda daladala ya makumbusho - mbezi kupitia goba mida ya jioni, kufika mwenge konda akawaambia wanafunzi wasubiri abiria wengine wapande kwanza... abiria walivyopanda konda akafunga mlango akawagomea kuingia gari ikaondoka, aisee nilimtukana yule konda na dereva wake hadi wakakosa cha kuongea..kilichonishangaza abiria wengine nao kimya hata hawasemi kitu kwa kile kitendo.. nilitamani nitukane bus zima. Daladala ilipofika tangibovu ndio wakajishtukia wakapakia wanafunzi maana kwa jinsi nilivyowamind walihisi sitowaacha salama naweza wachomesha.
😂😂😂😂We jamaa bwana,kwa hiyo matusi yako ndio ukajua konda kaogopa?
 
Na vitoto vya siku hizi mayaimayai sana...Wenzao tushakula rumba sana kwenye DCM za TMK -Mwenge,na unasukumana na konda hadi unawahi kwa Kipingu....sasa siku hizi konda anawaambia hao watoto hakuna kupanda vimekaa tu kama vi broiler vinapelekwa kibra.We LIKUD njoo huku uone raha ya kusoma shule za serikali.
 
1. Wanafunzi wapelekwe shule za karibu ambazo wanaweza Kutembea kwa mguu.

2. Serikali iweke idadi ya Wanafunzi kuingia kwenye daladala kwa kila trip.

Serikali isiingilie biashara za watu Kwa kisingizio cha Sheria.

Kama serikali inajali Sana inunue mabasi ya serikali kwaajili ya huduma hiyo. Au wapande Mwendokasi.

Au itoe fungu au kupunguza sehemu ya Kodi kwa wamiliki WA daladala kwa lengo hilo.
 
Serikali inunue mabasi kwa ajiri ya kubebea wanafunzi, mbona shule za private zina gari zao maalumu za kubebea wanafunzi wao, serikali inashindwa nn?

Kununua magari ya kifahari kwa viongozi inaweza? Ila kwa umma hawawezi? Mistake kupangia watu mali zao, wanatafuta kwa jasho afu tena muwafuje hovyo, nyie vipi?

Toeni hayo ma V8 na LC wabebwe wanafunzi, ila km watapanda dala dala walipe nauli husika ya abiria wa kawaida.

Hakuna kuchekeana lazima ukweli uwekwe wazi, Serikali iache uonevu,

Kama inajali.
Na sio ijali kwa gharama ya biashara za watu binafsi. Hiyo ni dhulma
 
Na vitoto vya siku hizi mayaimayai sana...Wenzao tushakula rumba sana kwenye DCM za TMK -Mwenge,na unasukumana na konda hadi unawahi kwa Kipingu....sasa siku hizi konda anawaambia hao watoto hakuna kupanda vimekaa tu kama vi broiler vinapelekwa kibra.We LIKUD njoo huku uone raha ya kusoma shule za serikali.
🤣🤣🤣🤣

Haya sasa twende kazi. Kimbia haraka Sana Hadi kwenye shule ya Ems kawatoe watoto wako huko uwalete Kayumba.

Thank me later
 
Sitaki maoni uyapeleke kwa LATRA, nataka uyapeleke huko Serikalini, kwenye vikao vya bunge, na baraza la mawaziri.

Najua umeelewa sasa.
Wewe ndugu nahisi unapenda ligi za maneno 😅... Nimesha reply hoja zako nyingi, sasa hapa lazima apatikane mmoja ajiongeze kuwa, kunyamaza nako huwa siyo ujinga, ni kuruhusu hekima ijidhihirishe. Haya Kila la heri ngoja niangalie na wengine wanasemaje mimi ligi za maneno hapana kabisa😅
 
Acha
Wasaalam,

Kule x kuna hoja kwamba, baadhi ya "makonda" wa ma Bus ya abiria wanazuiwa wanafunzi kupanda ma Bus hayo.

Tangu kuja kwangu iliambatana na ujumbe uliokuwa umetumwa kwenda kwa CarolNdosi na uliosomeka "Carol , naomba usaidie hili, moja ya changamoto kuubwa ni wanafunzi kupanda daladala sijui ni sheria ipi inaruhusu konda kuaamua kupakia au kutopakia, kiufupi wakinamama wanaopeleka watoto wao asubuhi vituoni wanapitia shida sana"

Baada ya kuwasiliana na taasisi ya udhibiti (LATRA) na kwa kuzingatia kuwa, changamoto hii huenda inawakumba wazazi wengi, naomba kutoa mrejesho kwa majukwaa yote kuwa; Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi na kinachotakiwa ni Wazazi hao watoe taarifa LATRA waambatishe na namba ya gari husika. Namba ya LATRA hiyo hapo.

Ahsanteni kwa ushirikiano, tuwalinde watoto wetu🇹🇿

Shukrani kwa CarolNdosi kwa ushirikiano. Mkurugenzi LATRA ahsante kwa ushirikiano.


Huu ndo ujinga wa ccm nguvu nyingi bila akili .
 
1. Wanafunzi wapelekwe shule za karibu ambazo wanaweza Kutembea kwa mguu.

2. Serikali iweke idadi ya Wanafunzi kuingia kwenye daladala kwa kila trip.

Serikali isiingilie biashara za watu Kwa kisingizio cha Sheria.

Kama serikali inajali Sana inunue mabasi ya serikali kwaajili ya huduma hiyo. Au wapande Mwendokasi.

Au itoe fungu au kupunguza sehemu ya Kodi kwa wamiliki WA daladala kwa lengo hilo.
1.Hilo ni tatizo sugu hapa mjini,mzazi anakaa msakuzi anapeleka mtoto diamond au Bunge..ni sifa za kijinga zinazo mtesa mtoto

2.walishatoaga idadi nadhani ni 2 up to 5 kama sikosei

3.Serikali ni mfumo wa kukandamiza wanyonge,ndio maana hata ardhi japo unailipia kila simu bado serikali imejitanabaisha ni mali yao,usishangae hata hizo daladala wanaona ni zao

4.Ukiongelea Mwendokasi ndio jinamizi lingine jipya,hao watoto wenyewe ndio wanabanwq mle hadi unakaonea huruma...huo mradi ni failure
 
Kuna mtu kuna umoja au shirikisho la watoa huduma hizi, kama ni hivyo, kwenye ajenda za kutoa maoni si haya ndiyo mngekuwa mnawasilisha kwenye mamlaka ya usajili

Uzuri hapo namba za msajili mmeziona, ilikuwa vema kuwa na utaratibu wa kutoa maoni, jamii inajengwa kwa maoni ya pande zote siyo kwa kuvunja sheria
Dr nimesoma reply zako nyingi ukiongelea kutoa maoni hii hoja yako watafuta utetezi uonekane kwenye kitengo chako wewe huna kosa

Wewe ndio umeleta mada humu sisi tunatoa maoni kulingana na mada uliyoleta usingeileta tusingeshughulika nayo kwahiyo usikwepe majukumu, wewe ni mtu wa serikali lakini pia ni mwanajamii peleka haya maoni huko kwenye vitengo vyenu na bungeni mtoe hizi sheria kandamizi utakuwa umesaidia Sana kuliko kujiona sio part ya tatizo hili
 
🤣🤣🤣🤣

Haya sasa twende kazi. Kimbia haraka Sana Hadi kwenye shule ya Ems kawatoe watoto wako huko uwalete Kayumba.

Thank me later
Aaaaah thubutuuuu
Mama yao nilishakula sana hizo mbilinge wao wanasubiri honi hapo getini🤣🤣🤣🤣
Halafu mbona hizo shule watoto wenu wanawahi sana kurudi?juzi nimemuona mtoto wa jirani std1 kaenda saa nne karudi saa sita au ndio ule mtaala mpya umeamua kupumzishe watoto akili?
 
1.Hilo ni tatizo sugu hapa mjini,mzazi anakaa msakuzi anapeleka mtoto diamond au Bunge..ni sifa za kijinga zinazo mtesa mtoto

2.walishatoaga idadi nadhani ni 2 up to 5 kama sikosei

3.Serikali ni mfumo wa kukandamiza wanyonge,ndio maana hata ardhi japo unailipia kila simu bado serikali imejitanabaisha ni mali yao,usishangae hata hizo daladala wanaona ni zao

4.Ukiongelea Mwendokasi ndio jinamizi lingine jipya,hao watoto wenyewe ndio wanabanwq mle hadi unakaonea huruma...huo mradi ni failure

Hatari Sana.

Wewe unakaa Bunju au Kijichi huko unataka upeleke mtoto Bunge kwa kutegemea hisani za makondakta. Mtoto kutwa nzima kuhangaika na hekaheka za barabarani.
Ndio maana Dsm ni Moja ya mikoa inayofelisha Sana hapa nchini.

Kama kila kata kuna shule ya serikali kwa nini Watoto wapande daladala kwa gharama za wafanyabiashara? Mbaya zaidi inakuwa lazima hapo ndipo dhulma ilipo.

Labda hiyo Sheria iwe ilitungwa zamani shule zikiwa chache lakini Kwa sasa haina Tija Sana
 
Wewe ndugu nahisi unapenda ligi za maneno 😅... Nimesha reply hoja zako nyingi, sasa hapa lazima apatikane mmoja ajiongeze kuwa, kunyamaza nako huwa siyo ujinga, ni kuruhusu hekima ijidhihirishe. Haya Kila la heri ngoja niangalie na wengine wanasemaje mimi ligi za maneno hapana kabisa😅
Ndugu yangu Lamomy nakuomba uje umchukue udugu wako cocastic yupo huku anabishana na vyombo vya dola watamsweka rumande😂😂
 
Wewe ndugu nahisi unapenda ligi za maneno 😅... Nimesha reply hoja zako nyingi, sasa hapa lazima apatikane mmoja ajiongeze kuwa, kunyamaza nako huwa siyo ujinga, ni kuruhusu hekima ijidhihirishe. Haya Kila la heri ngoja niangalie na wengine wanasemaje mimi ligi za maneno hapana kabisa😅
Kwanza nashukuru nimepata wasaa wa kujibizana nawee mama Vicky, maana kusemezana na waziri sio jambo dogo.

Afu ujue nn, mie nakukubali sana, tena mnoo, afu ni shabiki ako toka uko wizara ya Afya. Napenda pia unajipambanua wazi wazi ktk kutatua changamoto za wizara yako, hata za wizara nyingine ikiwa utahitajika uhusika wao.

Kongole kwako mama Vicky, bado nina jambo nawee kuhusu kundi maalumu fulani, nikitulia nitaleta hapa km uzi, na nita kutag ili uweze kutoa hata suluhisho na wengine wafaidike pia.

Uwe na siku njema!! 💖💖
 
Aaaaah thubutuuuu
Mama yao nilishakula sana hizo mbilinge wao wanasubiri honi hapo getini🤣🤣🤣🤣
Halafu mbona hizo shule watoto wenu wanawahi sana kurudi?juzi nimemuona mtoto wa jirani std1 kaenda saa nne karudi saa sita au ndio ule mtaala mpya umeamua kupumzishe watoto akili?
Kwanini unaishi duniani? Ukijibu Hilo swali nitakupa jibu lako
 
Dr nimesoma reply zako nyingi ukiongelea kutoa maoni hii hoja yako watafuta utetezi uonekane kwenye kitengo chako wewe huna kosa

Wewe ndio umeleta mada humu sisi tunatoa maoni kulingana na mada uliyoleta usingeileta tusingeshughulika nayo kwahiyo usikwepe majukumu, wewe ni mtu wa serikali lakini pia ni mwanajamii peleka haya maoni huko kwenye vitengo vyenu na bungeni mtoe hizi sheria kandamizi utakuwa umesaidia Sana kuliko kujiona sio part ya tatizo hili
Hujambo? Kadri jamii inavyoendelea kuniTag kuhusu hoja mbalimbali, nitaendelea ku reply kadri ya mipaka ya majukumu ya wizara hii na kuwaongoza kuhusu nini zaidi kifanyike iwapo wanahitaji maelezo zaidi. Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom