Hapo kwenye bango kuna namba za LATRA, hebu katoe maoni tafadhali. Uwe na jioni njema ya Baraka ✍🏻🙏🏽
Sasa Mheshimiwa, with due respect, kila mtu hapa unamwambia apige namba atoe maoni kwenye hiyo namba, sasa nini maana ya wewe kuanzisha huu mjadala na wakati unajua namba ipo public kila mtu anayo???
Ni vipi unakwepa majukumu yako ya kijamii hata kujibu tu kisiasa kwamba "nitafatilia" pia hutaki, na unajua ninyi viongozi wetu mmezoea kutudanganya watanzania miaka yote tangu uhuru na hakuna wa kuwawajibisha.
Anyway mimi naomba nikupe ushauri, you opt to digest it, take or leave it, but it's workable... Tangu nasoma shule za katikati ya jiji miaka ya tisini, changamoto ya usafiri kwa wanafunzi imekuwepo, ilikuwepo ipo na itaendelea kuwepo. Serikali haijawahi na haioneshi nia ya kushughulikia hili tatizo zaidi ya siasa tu na ahadi miaka yote (unless kuna plans ambazo bado hamjaziweka wazi kwetu) zaidi watoto wanazidi kuteseka kila uchwao. Inauma sana unapoona awamu zote za uongozi hakuna aliyetatua hili swala.
1. Kama serikali imeweza kujenga SGR na BRT na NYERERE DAM na other Mega projects, inashindwaje kuanzisha Shirika la usafiri wa wanafunzi Tanzania liwe na ma'bus ya kutosha kila kona?? Shirika hilo liendeshwe kwa ruzuku ya serikali na wapakie wanafunzi tu na watu wenye ulemavu tu. Na muda wa kazi (public buses) iwe ni asubuhi kuanzia saa moja mpaka saa tatu na jioni kuanzia saa tisa mpaka saa 12. Kama Chama Tawala kina ma'bus tena ya kifahari, ni maajabu kukosa ya wanafunzi.
2. Kwa kua serikali imejitahidi kwa asilimia kubwa kusogeza huduma za elimu karibu kabisa na makazi ya wahitaji (kata) basi Wizara yako na Wizara ya elimu na zingine zote husika, zishiriki kuhamasisha wazazi kupeleka watoto wao katika shule zilizo karibu na mazingira yaliyopo, umbali ambao ni walking distance kwa mwanafunzi. Na kama imetokea wizara ya elimu imempangia shule mtoto iliyo mbali na makazi yake labda kwa sababu ya kuhama makazi au mfumo tu, basi utaratibu wa mtoto kuhamishwa kwenda shule ya jirani usigubikwe na urasimu iwe ni rahisi.
3. Magari yote ya serikali na mashirika yake ambayo yanabeba wafanyakazi wao yaamriwe mara moja na wizara ya uchukuzi kuanzia hivi sasa yasimame kila kituo kuchukua wanafunzi. Hayo sio ma'bus binafsi ni ya watanzania wote wakiwemo wanafunzi hivyo hayapaswi kua na ubaguzi. Hii iwe amri na sio ombi.
4. Serikali iwape ruzuku wamiliki wa Daladala kila mwezi au iwaondolee kodi kabisa kwenye uendeshaji kwa minajili ya kubeba wanafunzi bila idadi. Kinyume na hapo ni uonevu kwa wenye magari kwa kigezo cha leseni yako inasemaje. Kumbuka leseni haibadiliki ili hali ya uchumi inabadilika. Leseni iliyochukuliwa miaka 20 nyuma ina utaratibu ule ule wakati bei ya mafuta imeshapanda.
5. Kwa leo naishia hapa wadau wataongeza..