Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Msafirishaji anapopewa leseni na LATRA hupewa masharti ya leseni, hii ni pamoja na kutobagua abiria. Serkali hutekeleza jukumu la kuwalinda watoa huduma, hii ndiyo sababu wasafirishaji wamepandishiwa nauli za watu wazima kutoka sh. 500 hadi sh. 600 - 1400 ili wasifanye kazi kwa hasara.
Hapa ndiyo sijui wengi wamesahau au ndiyo ile fulani kanichukulie cheti usikilize na masharti halafu fulani akipenda naye hata hasikilizi. 😅
 
Jamani unataka nichangie mjadala nikiwa na hasira Kali hivi 😬😬😬, hee tutafika kweli 🤣, huku wewe hapo unaachilia spana 🔧 konki plus, si tutapata stroke 🤣
Naamini mijadala yetu inaweza kuwa rafiki na ujumbe ukaenda vilevile maana kikubwa ni Nia zetu wote mioyoni mwetu kwenye kutimiza wajibu wa Maendeleo na ustawi wa jamii 🇹🇿
Naam bila shaka mkuu
 
Unajifanya unatukana bila kuwa hata na nidhamu. Issue kama hii imekuwa raised humus na kiongozi wa serikali wewe unalibeba jukumu la matusi badala ya kujadili hoja.
Mkiambiwa muende VETA mnanuna.
Khanisi sio tusi mkuu! Usiogope kama upo ivyo kaka! Nisamehe kwa hilo.
 
Msafirishaji anapopewa leseni na LATRA hupewa masharti ya leseni, hii ni pamoja na kutobagua abiria. Serkali hutekeleza jukumu la kuwalinda watoa huduma, hii ndiyo sababu wasafirishaji wamepandishiwa nauli za watu wazima kutoka sh. 500 hadi sh. 600 - 1400 ili wasifanye kazi kwa hasara.
Kuna kipindi hata kuwa mtumwa au kumilikiwa na Mtu mwingine hio ilikuwa ni Sheria na Haki ya mtu.., sasa kuwepo kwa hio Haki haimaanishi Sheria hio haikuwa Kandamizi..., hivyo sababu tumeona hili suala linajirudia na tumeona watu wanapaki magari kwa kushindwa kurudisha mikopo, tumeona makonda wanalalamika na kulia kwamba Hajapa Hesabu ya Tajiri..., Common Sense na busara ni kujiuliza ni wapi tunaweza kurekebisha..., Ukizingati hata hio 600 hadi 1400 anayotoa mtu mzima kulingana na kipato chake bado ni mtihani..., basi tujiulize je kuna a better alternative ?

Jibu ni ndio kwa matozo tunayotoa na sababu Usafiri, pamoja na Nishati na Afya ni moja ya huduma ambazo hakuna alternative kwa mbangaizaji kwanini hizo baadhi ya TOZO na MAKODI tusiwekeze kwenye usafiri wa UMMA ambao utakwenda sambamba na hawa watu binafsi kufanya biashara zao na kutafuta mkate wao ? After all economy of scale sababu ni UMMA ukiwa na a large number of fleets hata hizo mia mia au hata bure kwa wazee wakizichanga bado watabreak even (kumbuka hapa issue ni ku break even) sababu kuwatoa raia point A mpaka B kwa prices ambazo ni affordable that in itself bado ni Job well Done kwa serikali (kwahio badala ya kuwa kiranja na kupangia watu bei / vitu ambavyo wenyewe wanaona haviwezekani kwanini wasionyeshe mfano)??? After all pesa yetu wanachukua....
 
Najua uzi utafutwa😂sasa ukiwekq tu we nitag
Huu haufutwi, wee subiri, yaan nakala iwe kwa Mama Vicky afu ufutwe? mello na modes wake watatafuta Pa kujificha.

Nasemaje hili kundi maalumu lazima lifikiwe.
 
Muheshimiwa waziri umefocus sana na hizo namba za latra, tunajua taasisi za serikali kuzipigia simu ni sawa sawa na na kulamba kiganja cha paka hamna kitu wanajisikia sana na si kwamba hawajui wanajua vizuri tu, bahat nzuri mimi nimewahi kuwa muhanga enzi nasoma ikabidi niwenajilipia nauli kamili, inafika kipindi mpaka mmna mkalili konda, NASHUKURU NI MIAKA MINGI IMEPITA

Wazo ni kuwa serikali inamagari mengi sana, wawabebe hao wanafunzi kwa hiyo 200 tuone, polisi, jeshi, nataasisi nyingine ikawekwa muda bwana saa 12 kamili magari yatapakia wanafunzi, kuwapeleka karibu na shule au shuleni

Anyway usije niambia nipige simu, maana kazi yangu yenyewe ni kupiga simu kwenye hayo maofisi ya serikali kutatua tu changamoto ndogo wanakupiga danadana kama nini

Last mimi napenda unavyojaribu kutoa elimu kwa watu kazi njema sana
Ni busara zaidi kubadilisha mtizamo wako kuhusu LATRA, inawezekana unasema kutokana na uwezo wako wa kuhisi, lakini haujachukua hatua kuthibitisha hisia zako.
Si kweli kwamba LATRA hawapokei simu, na si kweli kwamba LATRA hawatatui changamoto zinapowasilishwa kwa njia ya simu au e-mrejesho.
Piga simu, toa taarifa kama kuna uonevu wowote unaofanywa na watoa huduma barabarani, kisha fatilia kujua hatua zilizochukuliwa, ni busara sana sisi raia kuwa mstari wa mbele kuwasaidia watoto wetu huko barabarani.
1. Kuwasemea kwa hao watoa huduma
2. Kuwa wepesi kutoa taarifa LATRA inapotokea changamoto barabarani hasa zinasohusiana na kuzuiwa kwa wanafunzi kupanda kwenye daladala.(Tuwapende na kuwathamini wanafunzi bila kujali kiwango cha uhusiano uliopo)
Kwa nyakati tofauti mimi nimetoa taarifa na zimefanyiwa kazi, napata wasiwasi unaposema Mamlaka husika hawafanyi chochote, Je umepiga simu? Je umetoa taarifa? hawakupokea kama mzazi au mtanzania uliyewahi kupitia changamoto kama hii ulichukua hatua gani??
Wanatatua changamoto, ni rai yangu sisi kuwapa ushirikiano ili waendelee kutatua changamoto hizi.
 
Wasaalam,

Kule x kuna hoja kwamba, baadhi ya "makonda" wa ma Bus ya abiria wanazuiwa wanafunzi kupanda ma Bus hayo.

Tangu kuja kwangu iliambatana na ujumbe uliokuwa umetumwa kwenda kwa CarolNdosi na uliosomeka "Carol , naomba usaidie hili, moja ya changamoto kuubwa ni wanafunzi kupanda daladala sijui ni sheria ipi inaruhusu konda kuaamua kupakia au kutopakia, kiufupi wakinamama wanaopeleka watoto wao asubuhi vituoni wanapitia shida sana"

Baada ya kuwasiliana na taasisi ya udhibiti (LATRA) na kwa kuzingatia kuwa, changamoto hii huenda inawakumba wazazi wengi, naomba kutoa mrejesho kwa majukwaa yote kuwa; Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi na kinachotakiwa ni Wazazi hao watoe taarifa LATRA waambatishe na namba ya gari husika. Namba ya LATRA hiyo hapo.

Ahsanteni kwa ushirikiano, tuwalinde watoto wetu🇹🇿

Shukrani kwa CarolNdosi kwa ushirikiano. Mkurugenzi LATRA ahsante kwa ushirikiano.

Shukrani sana Mheshimiwa waziri kwa kuwa mfuatiliaji mzuri wa mambo mbalimbali yanayoihusu wizara yako pamoja na mambo yanayohusu wizara za kisekta.

Pia kama wazazi tunaiomba serikali ipitie upya suala la adhabu mashuleni kwa watoto wetu maana wamekuwa wahanga wakubwa wa mara kwa mara kwa kukumbana na walimu wasio na maadili ya kazi kuwaadhibu kusikofuata utaratibu matokeo yake watoto wanapata majeraha ya kudumu mwilini.

Tukio la hivi karibuni nafikiri jana usiku mwanafunzi amefariki dunia kwasababu ya kipigo kutoka kwa Mkuu wa shule akishirikiana na walinzi wa shule mkoani Rukwa katika shule ya St. Kagwa kama sijakosea.

Kwanini serikali inakuwa nzito kutafuta mwarobaini wa ukatili huu dhidi ya watoto?

Hadi wafe watoto wangapi ama wapate ulemavu wangapi ndiyo serikali ishtuke?

Inaumiza mno watoto kukatishwa ndoto zao za maisha wakati serikali yao ipo inatazama tu.
 
Wajibu wa Serikali katika kutatua changamoto hizi SUGU ni upi ukiachana na suala la kutunga sheria, miongozo, kanuni na taratibu ambazo kiuhalisia zimeshindwa kuzaa matunda kwa miongo kadhaa?
 
Mbona serikali haiamuru wanafunzi kula mgahawani Bure? Kwani watoto hawapati njaa shuleni
Kwanini serikali iwaonee daladala, serikali haijui hii ni biashara
Msimamo wangu: ili kuepuka usumbu wanafunzi walipe nauli kamili
We jamaa hauko sawa, unauhakika wanafunzi wote wanaoenda shule wanakula migahawani? ni wanafunzi wangapi hawana uwezo na wanashinda njaa shuleni chakula wanapata baada ya kurejeq nyumbani!!??...unamaanisha hawa wabaki nyumbani wasiende shule sababu hawana uwezo wa kulipia nauli?? PATHETIC...
 
Na kwenye hizo hekaheka usisahau zile hekaheka za kusaka walimu wa tuition,mara mchikichini,mara pale Nakiete kwa nyuma mara Tambaza nyieeee ilikuwa ni oyaoya halafu jumapili mchana unazamia disco Billicanas kuna mashindano ya kushake mama anajua umeenda discussion aweeee....ila hapo wewe ulikuwa primary😂😂😂
Enzi hizo niko kadogo.

Nilikua na sis yangu demu wa mzee wa zeze (TID) basi huko bills ndo viwanja vyao..!!

Home walishangaa kumuona kwenye video yake, mzee aliongea kidogo ampe radhi..!! Anajua sis yupo shule kumbe anaswampa na Khaleed 😹😹😹
 
Back
Top Bottom