Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ha ha 😂Kwani wao kiingereza wanakijua vizuri au ni kile kiingereza cha kiarabu mambo ya guud morningii ..
Kifupi tulikuta wote hakuna anayejua kiingereza kwa ufasaa.
Sasa ilibidi kwa kuwa wamekuja huku kwa dharura tuwape short course ya kiswahili kwa miezi mitatu then tuwasambaze kwenye hizo hospitali hapo mambo yangeenda sawasawa.
Nadhani Sudan kusini wanajua kiingereza kuliko Sudan(kaskazini)Hawakijui vizuri lakini wanajitahidi kuongea sio kama Sisi
Kuna jamaa ni Msudani Kusini, Kuna kazi nilifanya naye Juzi Jumatatu, the guy is fluent in English
Kutokea hapo nikajilaumu kwanini nilisoma Shule za Kata 🙌
Me nadhani kama Wazazi tujitahidi kupambana watoto wetu wasisome hizi Shule za Kidumu na fagioKweli mkuu
Hata Mimi nafikiri hivyo, jamaa wako fluently sana kwenye KiingerezaNadhani Sudan kusini wanajua kiingereza kuliko Sudan(kaskazini)
Ila ni aibu MkuuUmetisha sana 😁😁😁
Hakuna sehemu lugha ni rahisi kama wacheza mpiraHata Mimi nafikiri hivyo, jamaa wako fluently sana kwenye Kiingereza
Sisi Wale Wakoloni walizingua baada ya kutawaliwa na Mataifa mawili Kwa nyakati tofauti
Hatukujua tutumie Kijerumani ama Kiingereza maana wote walitutawala
Kivipi Mkuu iwe rahisi kwao?Hakuna sehemu lugha ni rahisi kama wacheza mpira
Wasomi wengi wa Tanzania kiingereza kimewatupaMadaktari wengi English imewatupa
Sijui tunakwama wapiSerikali na taifa linatakiwa kuona kiswahili ni lugha kubwa kama ambavyo mataifa mengine yanavyokiona kiswahili,
Iwe lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya chini mpaka juu,
Kila taifa lenye lugha kubwa linaitumia lugha yake kufundishia
Ie. France,England,China na nyinginezo
Tuache kuchukulia poa kiswahili
Wajinga ndiyo waliwao..Eti English libaki kuwa somo tu! Lakini cha ajabu hao wanaoshauri hivyo watoto zao wanawapeleka ulaya na Marekani kuanzia chekechea ndiyo ujue viongozi wa nchi hii walivyo na roho mbaya wanatamani sisi na watoto wetu tuendelee kuwa wapiga kura wao tu na sio kushiriki katika uongozi.
Sudani inaongea English gani mpaka madaktari wa Kitanzania wawakimbie hao WASudani?Mwisho wa mwaka 2023 Wanafunzi wa masoma ya udaktari kutoka Sudan, wanao fadhiliwa masomo Yao na serikali ya tz 🇹🇿, hapa Nchi
Walisambazwa kwenye hospital za hapa Dar es salaam, wakitokea muhimbili, Kwa ajili ya kufanya practical training . Ili kuwapa sehemu zingine Sio wote wakae Tu muhimbili.
Katika hospital walizopelekwa ni mwananyamala, Temeke, ubungo, kigamboni etc.
Waka kabidhiwa Kwa wakuu wa idara mbalimbali Katika hospital hizo.
Cha kushanga wakuu wa idara wakashindwa kuwapa ushirikiano wa kutosha , wakawa Wana kula Kona, wengine wanakuwa wakali ili wasiulizwe maswali.
Shida kubwa ni Kwamba ma daktari walishindwa kuongea Nao English, kama taifa tumeingia matopeni Tena coz masoma wanayosoma ni Kwa lugha ya English.
Kwa hiyo hawa wanafunzi wakawa Wana lalamika kukosa ushirikiano report ikaja kuwa kuna language berrier. Na hawawezi Endelea Tena na practical training Yao, coz hakuna wanaoweza kufanya Nao communication.
So mwanzoni wa February 2024 ikabidi warudishwe muhimbili wakamalizie practical training Yao.
Ushauri: Kiswahili hakina tija Kwa taifa kifutwe mashuleni kabisa.
View attachment 2918900
Mkuu Kwan ulitumia nguvu kiasi Gani kuongeaIla Kiingereza bado ni changamoto kubwa sana Kwa wasomi wetu.
Ajabu wale waliosoma miaka ya 60/70/80 wanatema Lugha barabara sijui sisi wengine tunaferi wapi.
Nina rafiki yangu Mzungu anaishi London, weekend hii alinipigia simu Whatsapp, niliongea naye dakika 15 hivi baada ya kumaliza kuongea naye nikawahi Panadol faster maana kichwa kilishaanza kuniuma
Imagine sasa hao Madaktari wenyeji walipaswa kuongea nao Kila Siku masaa 7 ama 8 Kwa Siku 🙌
Haha tatizo watu hamtaki kuambiwa ukweliSudani inaongea English gani mpaka madaktari wa Kitanzania wawakimbie hao WASudani?
Nilikuwa Sudan kabla ya kutengana kaskazini na kusini, nikiwa based pale JUBA. Ni wasudani wachache saaaana wanaongea kingeereza tena ni kama asilimia 5 hadi 10 ya wakazi wote. Asilimia kubwa wanaongea Kiarabu, Kitgrinya, Kinuer na lugha zingine. hii ilikuwa ni 2006-2008, Ndo nilitoka huko.
Baada ya Sudan kusini kujitangaza huru 2011 ndo wakaamua kutumia kiingereza kama lugha yao ya taifa. Kwa sidhan kama tayari wana Kiingereza cha kutisha. Japo kwa muonekano hawa wanatoka kazini ambako lugha kuu ni Kiarabu. Labda kama una hoja nyingine.