DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Ukiniuliza mimi Ntakwambia kuna Shida nyingine tofauti na Language barrier..BICHWA KOMWE - and DR Mambo Jambo mje mtoe muongozo kwenye hili.
Kwanini..
Kwanza Daktari ndo translator Mkubwa kwenye tasnia..
Kwa sababu anasikiliza Hostoria ya Mgonjwa kwa Kiswahili anaiandika maelezo kwa kingereza..
Halafu akishaiandika anaelezea kwa kiswahili kwa mgonjwa..
Pili sitaki kuamini kwamba Daktari akiwa Muhimbili anakuwa anaongea Kingereza vizuri ila akiwa Temeke,Mwananyamala na Ubongo kingereza kinamponyoka...
Maana yake ni kwamba Daktari akipata ajira mubimbili anaingiwa na pepo la kingereza anaongea.kingereza fresh kabisa....
Daktari huyo huyo akiajiriwa Temeke au Kigamboni pepo la kingereza linamtoka anakuwa hajui kingereza na anakuwa mkali..
Kuna kitu ambacho kinafichwa nyuma ya pazia..
Anywei..
Mafunzo ya Udaktari yote MD mpaka Zaidi ya hapo yanafundishwa kwa lugha ya kingereza hata Practical.zake zote hufundishwa kwa kingereza Presentation za wagonjwa Wodini plus mitihani ya Wagonjwa na clinical yote ni kwa lugha ya kingereza hata akiwa wodini ni hivyo hivyo...
Sasa ghafla mtu ambaye kasoma kingereza miaka 6 bila Chembe ya kiswahili ghalfa anasahau kingereza????