DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Pole daktari. Kimsingi wabongo, tuna shughuli nzito utamaduni unatuathiri.

Mbaya zaidi wakati mwingine unaweza kukuta chuoni unafundishwa vizuri, intern safii lakini ukifika kazini kuanza kutekeleza unaonekana unachelewesha muda.

Ni sawa na mtu anayejua mgonjwa mwenye magonjwa mengine anatakiwa kuzungumza nini na mfamasia, ikiwamo historia ya madawa na dawa nyingine anazotumia.

Akimkuta mfamasia, akampatia tu dawa halafu akaja kulalamika, yule mfamasia hakuniuliza hata nina dawa gani nyingine, kukiwa na interaction je? Lakini hapohapo mwingine akiulizwa anasema wewe bwana nipatie dawa maswali mengi ya nn kila siku mi dawa natumia😾. Sadly hawa wa pili ndio wengi sasa.

Ukifuatilia unaweza kukuta mwanzo alifuata hizo taratibu, baadae akajifunza zinapoteza muda akaacha. Kwa hiyo chuoni kapikwa, intern kapikika ila baadaye kakata kamba utamlaumu nani?.

Na wengine tusiwaseme madaktari tu tukasahau proffesional nyingine utamaduni mbovu ni janga sana;
Shoe shine anaweza anza tu kutia kiwi bila kufuta na maji, procedure
Taratibu za matumizi ya vifaa zinabakwa tu
Fundi gari/pikipiki anaweza kuanza kufungurunyua bila hata kutest chombo labda ndo procedure.
Mpenzi mke au mme kukurukia tu bila hata foreplay 😉🤣🤣
Yote hayo ni utamaduni wa kutofata taratibu tunazofundishwa.
, I was so disappointed hasa kwa sababu wakati yule daktari anajaza fomu yangu ya bima, niligundua kuwa kumbe ni MD kabisa (kwa maana ya kwamba ana shahada ya udaktari), yaani ndo nilichoka kabisa, maana mwanzoni nilidhani ana diploma tu (CO).
 
Nakubaliana na wewe hapo kwenye utamaduni mbovu kwetu Watanzania, you are 100% spot on.
 
Watu wanasoma hizo course kwa ku-resit sana level za chini. Akishafika hapo anakuwa na msongo wa mawazo na majukumu mengiii. Pole mkuu ila tunaumizwa sana na hawa watu
Tutafika mbinguni tumechoka sana!!
 
Mkuu yeye alikuwa anaumwa!Sasa hapo anajigangeje na Yuko hoi?
 
We mwenyewe daktari na hujui unaumwa nini ila unataka dakitari mwenzako akwambie unaumwa nini, na anapokwambia unaumwannini bado hukubali, na humkubali.

M naona nyie wote ndio walewale
 
Duuuuhhh!! Aisee, hatari sana.
Pole sana mkuu.
Hayo ndiyo yanayotusibu huku wenzenu huku uraiani.
 
We mwenyewe daktari na hujui unaumwa nini ila unataka dakitari mwenzako akwambie unaumwa nini, na anapokwambia unaumwannini bado hukubali, na humkubali.

M naona nyie wote ndio walewale
Kwa hiyo kama nilikua najua naumwa nini ndo ningenunua tu dawa pharmacy, ninywe, halafu nilale?
Ukiwa daktari ukiumwa moyo ukiwa unaenda mbio, inabidi ujisikilize mapigo yako ya moyo mwenyewe, usikilize kama hewa inaingia kwenye mapafu, usikilize pulse rate yako inaendaje kisha ujue shida inayokusumbua, uingie pharmacy, uchukue dawa,, umeze uendelee na maisha yako? Ndo udaktari huo au sio?
Usipoweza kujifanyia hivyo wewe mwenyewe udaktari wako una shida?
 
Shida yetu ni kwamba elimu yetu tumeichezea vya kutosha..
 
Sio vijana tu hadi madaktari wazee nao hamna kitu ni vihiyo.
Kikubwa ninachomshukuru Mungu CO nilisoma tanzania ila MD nimesoma Sweden,vyuo vyote tanzania ni uozo .
Tumepoteza ndugu zetu wengi kwa uzembe wa Dr
Huu ni uongo unaofana na ukweli labda ungesema kuna mahali kuna shida ila sio kuwa Vyuo vyetu vyote uozo hawa Proff wetu waliojaa vyuoni kwetu ndio hawahawa wamesoma Sijui Calgarly mara KUMAMOTO, sijui Zhengjeng na ndio hufundisha na kuandaa mitaala huku vyuoni inamaana nawenyewe ni UOZO japo wamesoma hukohuko Nje ambako wewe unaona wako vizuri

Mara kadhaa nimekuwa naona Gynacologist sijui Cardiologist(toka nje) wanakuja fanya kambi katika vituo ambavyo nakuwepo pia mbona wengi wamekuwa wakiwakubali sana baadhi ya wataalam wetu wandani wako vizuri!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…