DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sasa utajifanyia diagnosis ugenini?
 
Akili zote ziko kwenye kula kimasihara,yaani shida tupu kuanzia vipimo vya lab,namuuliza daktari kama kuna kipimo cha HCG hajawahi kusikia hata hiyo hormone,asa ningemwambia estradiol,kiufupi sikumlaumu sana maana kusahau kupo ila kwa jinsi anavyonisikiliza nikaona hapa hamna kitu,nikaghairisha matibabu.
 
Zamani kazi hizo zilikuwa za wito,sasa hivi tunasoma tupate ajira,ila kuna vijana wako vizuri bado,daktari wangu ni she(specialist)lakini yuko vizuri sana na kuna mahali pia nilikutana na kijana naye pia anajua na anaipenda kazi yake,asilimia kubwa vijana ni wa hovyo
 
Unamuonea tu daktar wa watu ila vitendea kazi ulijiridhisha kuwa vipo ? Health center zina uhaba wa vifaa , so shukuru hata alipo doubt BP kama diagnosis yake , mwisho wa siku ww kama daktar inabidi ujue wap kwa kwenda kulingana na case yako maana naamin lzm kichwan unakuwa ddx zako , kwenda health cente alitakiwa afanye hvyo commoner
 
Mkojo ulikuwa dark brown, hii hospital ipo sehemu ya wenye nazo[emoji383]. Sitaji jina kwa sababu za privacy.
Hadi hapo inakuwa ni uongo, privacy ya kitu gani kwamba wewe pekee ndo mgonjwa hospital nzima?
 
Hamaanish kujitibu , ila ww km dr lzm uwe na ddx zako ambazo zitakuguide uende wap kupata huduma nzuri
 
Kuna dogo yuko Mloganzila yeye ukimweleza tatizo kazi yake ni ku-google ndo anakupa majibu
Ndo maana nimesema kuwa mtoa mada alitakiwa ajue tatizo lake kabla hajaenda hospital.
Siku hizi ukiweka dalili zote unaletewa majibu, dawa etc
 
Aliniambia binti yangu ambaye ni daktari, '' Baba usiende kwa madaktari vijana, hawa walisoma ili wapate vyeti sio kuelewa''. Na mimi nakubaliana nae kabisa. Bora nitibiwe na nurse mtu mzima kuliko kutibiwa na daktari kijana.
Usikariri sasa kuna kada madaktar wapya ndo bora kulingana na mitaala mipya
 
Vifaa pekee alivyohitaji ni mikono yake, stethoscope pamoja na Manual BP machine, ambavyo vyote vilikwepo mezani kwake niliviona.
Ilikua ni saa tisa za usiku mind you, ilikua logical kwenda the nearest facility. Nimesisitiza si kwamba nilitegemea matibabu ya kibingwa usiku ule pale health center, ila nilihitaji mtu tu wa kusikiliza kifua changu, mapigo yangu ya moyo na pulse yangu na aweze kuniambia kwamba, brother hapa you need to go for specialist care, au bro, this is minor, haina issue. Na any MD with a stethoscope and a manual BP machine should have been able to do so.
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani pia.
 
Mwanzo alishindwa kulala lkn baada ya tukio akapona kabisa. Sasa sijui ni ugonjwa gani mkali hivyo na ukipona bila dawa

Njooni kwetu madokta wa mitishamba hatuna mbambamba
Nimesema kuwa nilitoka hospitali hapo health center saa 11 alfajiri, hadi nafika home ni around kumi na mbili kasoro, hakukua na suala la kulala tena hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…