Wakataa ndoa kuna muda wana point, imagine mtu umeolewa na mtu kama huyo jamaa unayemzunguzia, kwanini usikatae ndoa na kukimbia, na kuja kutuletea uzi humu? hakuna ndoa hapo ni mtu mmoja ameamua kumsindikiza mwenzie aishi maisha yake.
Anachofanyiwa huyo dada ni unyanyasaji wa kihisia, ni vile tu hana pa kwenda.
Ngoja nikusanue mleta mada, Ukiwa na mume ambaye ni rafiki yako, haihitaji akuambie nani amepiga simu saa nane usiku, Simu ikiita mida ambayo "siyo" unaanza kuguess atakuwa fulani, au ni fulani, au ni fulani, na katika assumption moja ujue kuna jibu sahihi. Haihitaji mtu akuambie mlinzi kapiga simu, akipiga simu mlinzi utajua tu!
Nataka kusemaje? Kama unapendwa kweli, Unakuwa unamjua mumeo na ratiba zake bila ya kumfatilia nyuma nyuma au kushika simu yake.