Mimi nilimzimikia sana huyu dada kwa uzuri wake, wala hakuonekana mwenye kujikweza wala kutaka makuu, kwani sikuwahi kusikia kama ana kashfa yoyote ile. Kwa kweli, kama amekamatwa Brazil kwa sababu ya mihadarati, nimehuzunika. Nilikuwa ninamweka mahala pa pekee, na kama angekuwa mvumilivu, angefika mbali.
Huu u-Masogange ukomeshwe jamani. Tuwaonye hawa akinadada wenzetu, kwamba HAKUNA MAISHA YA MKATO! Kila mtu afanye kazi kwa bidii na uadilifu, Mungu atamwona, atampa riziki yake halali. Hizo pesa za Shetani zinawaumbua watu kila uchao.
Pole Aisha. Pole. Waliokudanganya wako wapi? Wao wanapeta, wewe uko jela!