Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Kwani songesha usipowalipa wanakufanyaje??
 
Next vunja line lala mbele dingii
 
Hapo kuishika kwa madoido naona hicho ndio ili kukwaza sana
 
Watu wengi huwa hawajutii kukopa kwa sababu ya kiwango cha pesa wanachokopa, suala la kujuta huwa linatokana na ile amani unayoipoteza baada ya kukopa.

Hapa ndipo wengi huwa wanakuja kugundua baadae kuwa peace of mind is more expensive than money.

Hebu fikiria mtu anakopa laki tano akiamini atalipa baada ya mwezi mmoja, matokeo yake ghafla biashara inadorora au anapoteza kazi, mtu wa aina hii kuanzia hapo kila simu atakayo kuwa anapigiwa atakuwa anaona ni kama mdai wake anamtafuta, yani kila notification lazima iwe inamstua. Akimuona mtu anayefanana na mdai wake barabarani lazima atabadilisha njia, mwisho lifestyle yake kwa ujumla inabdilika kwa sababu ya deni.

Madhara ya kuwa na deni ambalo kwa muda huo hauoni namna ya kuweza kulipa huwa yanaongezeka hatua kwa hatua, kwanza hautokuwa unalala kwa amani, jambo lingine unaanza kuwa unawaza kupita kiasi, baadaye unaona uanze kuwakwepa marafiki na ndugu kwa kuhofia kuulizwa maswali labda kwanini umebadilika, mwisho wake unajitenga na watu, confidence yako inashuka, hata maamuzi yako ya kawaida yanaanza kuwa mabovu kwa sababu akili yako yote imefungwa kwenye deni.

Walio wengi pia huwa wanaishia hatua ya kupoteza uaminifu wao. Leo unasema nitakulipa kesho, kesho unasema wiki ijayo, siyo kwa sababu unapenda kudanganya, bali kwa sababu unatafuta muda. Taratibu unajikuta unajenga tabia ya kutoa visingizio kila siku. Deni linaweza kubadilisha tabia ya mtu ambaye hapo awali alikuwa mkweli.

Kuna msemo unasema, "ukikopa, unakuwa umenunua furaha ya leo kwa gharama ya amani ya kesho." Ndiyo maana kabla ya kukopa mtu anapaswa ajiulize ikitokea amechelewa kulipa, je bado atakuwa na uwezo wa kuishi kwa utulivu? Kama jibu ni hapana, ni bora uvumilie shida yako uliyo nayo leo kuliko kuingia kwenye maisha yenye presha.

Kifupi hekima ni kujua ni lini ukope kwa nini ukope, na kwa mpango gani utalipa. Hapo ndipo tofauti kati ya mtu anayelitawala deni na yule anayetawaliwa na deni inaonekana.
 
Watu wengi huwa hawajutii kukopa kwa sababu ya kiwango cha pesa wanachokopa, suala la kujuta huwa linatokana na ile amani unayoipoteza baada ya kukopa.

Hapa ndipo wengi huwa wanakuja kugundua baadae kuwa peace of mind is more expensive than money.
Exactly 💯
Msongo wa mawazo unabisha hodi
Yes Yes Yes Yes
👏👏
Kifupi hekima ni kujua ni lini ukope kwa nini ukope, na kwa mpango gani utalipa. Hapo ndipo tofauti kati ya mtu anayelitawala deni na yule anayetawaliwa na deni inaonekana.
Shukran brother kama kawaida yako👏👏 The Thinker 🧠
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…