Madeni yasikufanye ujiue au kujivua utu, vumilia yatapita tu

Madeni yasikufanye ujiue au kujivua utu, vumilia yatapita tu

Shondo

Member
Joined
Apr 26, 2023
Posts
7
Reaction score
53
Nawasalimu sana ndg zangu, ningependa kushea nanyi mawili matatu yanayohusiana na maisha na kwanini hupaswi kuukatisha uhai wako kisa madeni,

1. Mimi ni mwajiriwa niliyekata tamaa na maisha kutokana na changamoto za maisha nazopitia kwani hata kula yangu shida na kuvaa ndio usiseme, nina suruali tatu na shati tatu tu.

2. Mara kibao nimejitahidi kuwashirikisha ndg na jamaa zangu wa karibu kuhusiana na hali ya ugumu wa kimaisha naopitia lakini hakuna nachoambulia zaidi ya dharau kutoka kwao na kejeli.

3. Kuongeza deni juu ya deni sio dawa ya kujikomboa kutoka kwenye madeni bali ni kuongeza ugumu wa maisha

4. Nimelazwa ndani mara kibao kisa madeni ya watu na mtu asikudanganye huwezi jishughulisha vyema kwa lolote lile ukiwa na madeni.

5. Madeni ni mabaya sana yani tena sana, yanarudisha nyuma, yanadharirisha ila yote na yote usiutoe uhai wako wala usiuvue utu wako kisa madeni, maisha inabidi yaende tu mie madeni yangu nayamaliza 2027 .

6. Hata siku hii ya leo sijala kitu lakini Mungu ni mkubwa najua yeye ndio anayeijua kesho yangu .

Ukiona hayakuhusu kaa kimya Mungu asije akakupatia mtihani kama huu pia.
 
Nilitaka nimuulize hilo swali ila nikikumbuka kuna wakati unaajiriwa na ofisi kali, full kiyoyozi na ukitoka watu lazma wageuze shingo ila hali ya wallet na account ya bank zipo ICU.

Unakuta title kubwa ila mshahara unaopokea ni hand to mouth.. Mungu amsaidie tu
Ndio ni mwajiriwa kabisa ila ajuae ni Mungu kama ulivyosema
 
Back
Top Bottom