Madeni yasikufanye ujiue au kujivua utu, vumilia yatapita tu

Madeni yasikufanye ujiue au kujivua utu, vumilia yatapita tu

We tulia tu Tushaambiwa tunadaiwa watz wote sijui tilioni ngapi jumla.
Yaani ww hilo deni lako cha mtoto una deni lingine huku hujui.
Kula ugali maharage piga kimya
 
Madeni siyo ya kuyaogopa, kwanza ukiwa na deni ndo utapata akili ya kutafuta pesa kila kitu kinachangamoto yake lakin wakati huohuo kinatengeneza nafasi nyingine ndani yako
 
Nawasalimu sana ndg zangu, ningependa kushea nanyi mawili matatu yanayohusiana na maisha na kwanini hupaswi kuukatisha uhai wako kisa madeni,

1. Mimi ni mwajiriwa niliyekata tamaa na maisha kutokana na changamoto za maisha nazopitia kwani hata kula yangu shida na kuvaa ndio usiseme, nina suruali tatu na shati tatu tu.

2. Mara kibao nimejitahidi kuwashirikisha ndg na jamaa zangu wa karibu kuhusiana na hali ya ugumu wa kimaisha naopitia lakini hakuna nachoambulia zaidi ya dharau kutoka kwao na kejeli.

3. Kuongeza deni juu ya deni sio dawa ya kujikomboa kutoka kwenye madeni bali ni kuongeza ugumu wa maisha

4. Nimelazwa ndani mara kibao kisa madeni ya watu na mtu asikudanganye huwezi jishughulisha vyema kwa lolote lile ukiwa na madeni.

5. Madeni ni mabaya sana yani tena sana, yanarudisha nyuma, yanadharirisha ila yote na yote usiutoe uhai wako wala usiuvue utu wako kisa madeni, maisha inabidi yaende tu mie madeni yangu nayamaliza 2027 .

6. Hata siku hii ya leo sijala kitu lakini Mungu ni mkubwa najua yeye ndio anayeijua kesho yangu .

Ukiona hayakuhusu kaa kimya Mungu asije akakupatia mtihani kama huu pia.
Nilijua ni mimi tu aisee najutraaaaa na sitokaa nikarudia nimedharirika nimepoteza direction ya maisha hakuna kinachoenda kwe maisha nna sket mbli tshert mbil na sijui yatapita yaend wap ni kam yapo kuninyoosha aman naiskia kwenye redio nimechoka yule alojirusha ghorofan nataman ngekuwa mimi nipumzike kwa kwel but all in all Mungu mwema[emoji24][emoji24]ila hii hali sikia tu
 
Hyo hali isikie tu kwa mwingine ikikufika ni hatari sana, kuna muda unakata tamaa hata yakuishi tena maana hauoni mbele wala nyuma.pole sana mungu akuvushe
Ni kwel mtu hawez elewa mpaka yakufike mi najutraaaaaaaa[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Deni haliuwi mtu. Musiba anadaiwa Bil 7 na aliyeanzisha Deni kafa. Mdaiwa anadunda tu mtaani. Ni kujifunza kuwa positive.
Den haliui aisee linakosesha aman asikwambie mtu mwenye connectio na kaz yoyote ya ya usafi tu anipe nilipe madeni ya watu niishi kwa aman plz
 
Back
Top Bottom