Madeni yasikufanye ujiue au kujivua utu, vumilia yatapita tu

Madeni yasikufanye ujiue au kujivua utu, vumilia yatapita tu

Kuna mtu aliuza nyumba yake ya pekee kwa akili ya madeni. Demi ni zuri ukipiga mahesabu ya kina.
 
Basi mi sugu 😀😀😀😀

Nikikaa mwenyewe ndo nalia ila nikiwa na watu walaa niko fresh kabisa sikondii wala nini
kweli umekuwa sugu 😅😅 ila wengine ilifikia level unadaiwa na watu na unadaiwa na taasisi .. acha tu
 
Nawasalimu sana ndg zangu, ningependa kushea nanyi mawili matatu yanayohusiana na maisha na kwanini hupaswi kuukatisha uhai wako kisa madeni,

1. Mimi ni mwajiriwa niliyekata tamaa na maisha kutokana na changamoto za maisha nazopitia kwani hata kula yangu shida na kuvaa ndio usiseme, nina suruali tatu na shati tatu tu.

2. Mara kibao nimejitahidi kuwashirikisha ndg na jamaa zangu wa karibu kuhusiana na hali ya ugumu wa kimaisha naopitia lakini hakuna nachoambulia zaidi ya dharau kutoka kwao na kejeli.

3. Kuongeza deni juu ya deni sio dawa ya kujikomboa kutoka kwenye madeni bali ni kuongeza ugumu wa maisha

4. Nimelazwa ndani mara kibao kisa madeni ya watu na mtu asikudanganye huwezi jishughulisha vyema kwa lolote lile ukiwa na madeni.

5. Madeni ni mabaya sana yani tena sana, yanarudisha nyuma, yanadharirisha ila yote na yote usiutoe uhai wako wala usiuvue utu wako kisa madeni, maisha inabidi yaende tu mie madeni yangu nayamaliza 2027 .

6. Hata siku hii ya leo sijala kitu lakini Mungu ni mkubwa najua yeye ndio anayeijua kesho yangu .

Ukiona hayakuhusu kaa kimya Mungu asije akakupatia mtihani kama huu pia.
Unalazwaje ndani kisa madeni? Halafu tena mwajiriwa, uliza sisi tuliojiajiri na maisha yalivyotupiga tangu Mwendazake ashike nchi, Mwendazake aliua sekta binafsi kabisa, wahandisi na wasanifu majengo tuliojiajiri mambo yakaanza kwenda kombo, sasa madeni yametukaba tunapumua kwa mashine, wewe mwajiriwa huna madeni usihofu.....
 
Nadaiwa pesa kiasi cha Tsh milioni 37 halafu zote nilipiga hasara sina hata mia mbovu zaidi ya kijimshahara
Ulizimbotea sio? Mademu wanamaliza hela sana pia. Pole lakini hilo si deni, achana nalo anza upya...
 
Hiyo hali isikie tu kwa mwingine ikikufika ni hatari sana, kuna muda unakata tamaa hata ya kuishi tena maana hauoni mbele wala nyuma. Pole sana Mungu akuvushe
Siku ikitokea umekata tamaa ya kuishi usiende kwenye majengo marefu kujirusha, mnatupa kazi sana yakusoma taarifa, wee ukichoka maisha nenda kwenye mto wenye mamba ukapotee huko tusijue yaliyokukuta...

Au ingia kwenye pipa lenye conc. Sulphuric Acid
 
Back
Top Bottom