Madereva wa Bolt waandamana kwenye ofisi za kampuni hiyo kupinga ongezeko la ofa wanazopata wateja

Madereva wa Bolt waandamana kwenye ofisi za kampuni hiyo kupinga ongezeko la ofa wanazopata wateja

Madereva kadhaa wa Bolt walifanya maandamano hadi makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Kinondoni, Dar es Salaam, siku ya Jumatatu, Februari 2, 2026, kupinga tozo kubwa na ongezeko la punguzo kwa wateja.

Madereva hao walifika nje ya ofisi hizo majira ya saa 4:00 asubuhi, lakini walitawanywa na polisi. Baadhi yao walijaribu kuomba kuonana na Mkuu wa Mkoa.

Hili ni tukio la pili la maandamano ya madereva wa Bolt kuhusu suala hilo hilo. Maandamano ya kwanza yalifanyika Oktoba 15, 2024, ambapo madereva walikusanyika nje ya ofisi za Bolt Kinondoni, hali iliyopelekea kufanyika kwa kikao kati yao, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) na wawakilishi wa Bolt.

“Mikopo ya wateja imekuwa kero; nauli inaonekana ni shilingi 10,000 lakini kwa mteja inaonekana shilingi 5,000. Hili linatupa changamoto kubwa,” alisema mmoja wa madereva.

Kwa kawaida, punguzo linalotolewa kwa wateja hukatwa kwenye kamisheni ya Bolt. Hata hivyo, madereva wanasema kuwa utaratibu huo unavuruga mwenendo wa kawaida wa biashara kwani ofa hizo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara.

Ikilinganishwa na maandamano ya Oktoba 2024, idadi ya madereva waliofika ofisi za Bolt safari hii ilikuwa ndogo zaidi. Baadhi ya madereva walihusisha hali hiyo na changamoto za kujiandaa na kuzungumza kwa sauti moja miongoni mwa madereva wa Bolt.

Mkuu wa Wilaya ameita kikao na madereva hao baadaye leo, ambapo wawakilishi wa LATRA pia watashiriki. Tukio hili linajiri siku moja baada ya Uber kutangaza kujiondoa katika soko la Tanzania, hali inayofanya Bolt kuwa mchezaji mkubwa zaidi na kwa kiasi kikubwa kampuni pekee yenye nguvu ya kudhibiti soko.

Soma Pia Madereva Taksi Mtandao (Bolt) wagoma, wataka ongezeko la nauli, Polisi waingilia kati
===

Several Bolt drivers marched to the company’s headquarters in Kinondoni, Dar es Salaam, on Monday, February 2, 2026, protesting high charges and increased customer discounts.

The drivers arrived outside the offices at around 10:00 a.m., but were dispersed by police. Some attempted to seek an audience with the Regional Commissioner.

This marks the second protest by Bolt drivers over the same issue. The first protest took place on October 15, 2024, when drivers gathered outside the Bolt offices in Kinondoni, leading to a subsequent meeting with the Land Transport Regulatory Authority (LATRA) and representatives from Bolt.

“Customers offers have become an annoyance, the fee will read 10,000 but to the client will read 5,000, this is very challenging,” one of the drivers said.

The discounts offered to customers are normally deducted from Bolt’s commission. However, drivers argue that the practice disrupts the normal flow of business as such offers have become more frequent.

Compared to the October 2024 protest, the number of drivers who reached the Bolt offices this time was much smaller. Some drivers attributed this to challenges in organizing and speaking with one voice among Bolt riders.

The District Commissioner has called for a meeting with the drivers later today, where representatives from LATRA will also be present. The incident comes a day since announcement by Uber to leave the Tanzanian market, practically making Bolt the largest player and the only player with enough muscles to control the market.

Source: The Chanzo
Hivi kwani kukiwa na ofa, si maana yake Bolt wana top up ile amount ambayo mteja amepewa discount? Does it mean kwamba kama nauli ilitakiwa kuwa 6000, then kwa sababu ya ofa mteja akaambiwa alipe 3000, si inamaanisha kuwa 3000 iliyobaki Bolt watamlipa dereva wao wenyewe, na dereva mwisho wa siku atapata ile ile buku 6? Au kukiwa na ofa maana yake inakula kwa dereva? Nielewesheni taratibu nielewe kwa nini madereva wamind Bolt wakitoa hizo ofa kwa wateja?
 
Kuna siku niliona mtu amerikwesti ikaja mia tano kwa sababu ana ofa

Nawaza kama wewe
 
Ile discount inafunikwa na commission wanayochukua Bolt. Ikizidi hiyo commission, inakula na commission ya madereva.

Bolt wanafanya kitu kinaitwa blitzscaling, wanateka soko kwa nguvu kubwa bila kujali hasara.
 
But the difference is the same. Au mimi ndo sielewi mahesabu?
Kwani hiyo commission wanayochukua Bolt, si ni cost ambayo ni LAZIMA mwisho wa siku driver ailipe? Au kuna namna ya kutoilipa?
 
Sijui waweke option ya kutip tu... Sema wabongo na kutip wapi na wapi
Walio wengi wanatumia ujanja wa kubadili destination, anakubaliana na mteja kama alikuwa anatoka Mawasiliano kwenda Tabata, anafupisha safari lakini mteja analipa ile iliyokuja mwanzo kabla ya kufupisha safari.

Ingawa kuna wengine wanaomba kuongezewa umbali ukiwa mrefu na bei wanaona haijipi.
 
Back
Top Bottom