Madereva wa kampuni ya mabasi ya Sauli wamshambulia abiria aliyeripoti kuhusu mwendokasi

Last week nilitoka Mbeya kuja Dar, nilikuwa naendesha gari dogo, nilikuwa speed 130km/hr but bus la Saul lilinipita ningali mwendo huo.
Mleta mada yupo sahihi, haya mabus ya Saul yanakimbia sana!
 
Huyo abiria nae hana akili kama ataki mbio si apande mabus ya Harusi yanajulikana. Yaani upande basi la wafanyabiashara then utake speed ya Harusi
Wafanyabiashara ndio wale tulikuwa tunawaweka kwenye viroba juzi Mafinga kisa upuuzi huohuo. Mnakimbizwa bila sababu mnawahi kufanya biashara gani? Sasa wameacha biashara na kuacha familia zao kisa upuuzi huo huo. Ipo siku ya Sauli inakuja. Mtalia na kusaga meno endekezeni ujuha tu.
 
MABASI YA SAUL NI MAJENEZA YANAYO TEMBEA... Nashangaa watu wanaendelea kuyapanda na ajali kila mwezi...
Alafu jamaa mwenyewe ana mabasi 7 tu. Anahonga sana matrafiki. Hakuna trafiki wenye njaa kama wa Mbeya- Dar. Buku buku zinawatoa utu. Madhara ya speed kubwa nimeyaona juzi Mafinga, tulipotoa na kuweka vipande vya miili ya marehemu kwenye viroba. Mungu atusaidie kwa kweli.
 
Wewe umeambiwa hautakufa, Au wewe ni msaidizi wa mwenyezi Mungu hapa duniani?
Umeandika kitu cha kijinga sana binti yangu. Wote tutakufa ila yakupasa uepuke vitu vingine. Kuna vifo vingine tunavitafuta. Kuna siku nilikutana na Sauli inashuka Kitonga kwa speed ya ajabu na anaoovertake bila umakini. Pale unajitafutia kifo mwenyewe.
 
Mimi napenda basi linalokimbia sana
Huyo abiria siku ingine apande trekta litakaliendana na spidi yake atakavyo
Watu unataka kuwahi tuendako halafu mtu anataka dereva aendeshe basi mwendo wa konokono
 
Ukiona gari linaendeshwa vibaya tupigie makao makuu ya traffic au hata sms kwa namba 0784688881 tutachukua hatua. au mtaarifu balozi yoyote wa RSA ikiwa ni pamoja na Mimi.
Nyie mnaepokea bukubuku mkipigiwa si mtamtaja kama mlivyomtaja huyo abiria. Hamuaminiki nyie, elfu moja moja zinawatoa utu.
 
Mimi napenda basi linalokimbia sana
Huyo abiria siku ingine apande trekta litakaliendana na spidi yake atakavyo
Watu unataka kuwahi tuendako halafu mtu anataka dereva aendeshe basi mwendo wa konokono
Hongera sana ngoja siku tuje kukusanya mabaki yako kwenye kifungashio cha 500. Wenzako juzi walikuwa wanapenda hivyo hivyo hakuna kulala za Mbeya Dar tunakusanya mabaki yao kwenye vifungashio pale Mafinga. Bado wewe, pendeni sifa tu.
 
Hongera sana ngoja siku tuje kukusanya mabaki yako kwenye kifungashio cha 500. Wenzako juzi walikuwa wanapenda hivyo hivyo hakuna kulala za Mbeya Dar tunakusanya mabaki yao kwenye vifungashio pale Mafinga. Bado wewe, pendeni sifa tu.
wote wanaokufa sababu huwa ni basi kukimbia?
 
Kwa vile watu wote hawafi kwa malaria kwa hiyo hamna umuhimu wa kulala kwenye chandarua?
Wanaolala kwenye vyandarua Hawafi kwa malaria? Kwani mbu hushambulia mtu akilala tu nje akitembea Hawako au akikaa nje mbu huwa hawako?
 
Nyie mnaepokea bukubuku mkipigiwa si mtamtaja kama mlivyomtaja huyo abiria. Hamuaminiki nyie, elfu moja moja zinawatoa utu.
Sio wote.
Kuna watu wamelitumikia jeshi la polisi mpaka kustaafu bila kupokea hela ya mtu Wala kuliibia jeshi.
Nakubali Askari wa barabarani wengi ni wabovu lkn Kuna waadilifu pia.
 
Mtu asiye ma maono (Vision) yeye si mtu wa kujijali maisha yake wakati wote,

Yeye vyovyote na chochote hata cha hatari ya kupoteza uhai wake huwa hajali na huwa anakuwa hana cha kupoteza.

Imeandikwa;

“Pasipo maono watu hushindwa kujizuia”

“Without vision people perishes “

Kwa hiyo ninapotafakali Neno la Mungu na kuona jinsi wengine ambavyo wako tayari kuyaweka maisha yao rehani huwa sishangai sana.
 
Wanaolala kwenye vyandarua Hawafi kwa malaria? Kwani mbu hushambulia mtu akilala tu nje akitembea Hawako au akikaa nje mbu huwa hawako?
Kwa hiyo unaona hamna umuhimu wa kulala kwenye chandarua? Unaonaje hospital tufugie kuku sababu kufa kupo tu, si ndio?
 
Huyo siyo abiria, ni jinga fulani lenye bifu na Kampuni ya Mabasi ya Sauli.

Mabasi yote kuna maeneo yanaongeza mwendo la sivyo mtafika kesho yake.

Kama anaona shida, atumie usafiri wa ndege.

Alafu speed ya 115 anaona nyingi. Atakuwa kichaa huyo
 
Unafikiri kwa kutumia makalio

Siku ukipoteza kiungo ndio utaelewa
 
Ajali kazini.
Boda boda wangu alikuwa makini Sana barabara anaendesha kwa kufuata Sheria,lakini jana daladala imemfata pembeni ikamburuza ndo tumetoka kumsitiri mida hii.Hata wa mwendo wa harusi wanapata ajali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…