Madereva wa mabasi ya Kanda ya Ziwa kuelekea Dar acheni ligi barabarani

Madereva wa mabasi ya Kanda ya Ziwa kuelekea Dar acheni ligi barabarani

Mkuu mbona sikuhizi Hawakimbiii! Kuna siku nilitoka huko saa kumi na mbili, saa moja na nusu tulikua ubungo Shell, enzi zile kuna zile Ally's sports achana na hizi Ally's star.. 2011 hiyo, zilikuaga scania 95 hatari sana!
Bro hizo chuma zilikuwa zinatembea sana,zilipelea akafungiwa root ya dar mwanza,waliingiza gari nyegezi SAA kumi na mbili 15'
 
Tumetoka hapa Nyegezi Stand muda si mrefu.

Aisee, haya mabasi yanakimbizwa hatari. Naona kuna ligi flani inafanywa barabarani.

RTO wa mikoa husika chukueni hatua.
Nyegezi hiyo ndio iliyoimbwa au?
 
Bro hizo chuma zilikuwa zinatembea sana,zilipelea akafungiwa root ya dar mwanza,waliingiza gari nyegezi SAA kumi na mbili 15'
Jamaa walikua wanatembea sana, then hakuna muda wa kupoteza, nakumbuka tuliacha mtu washroom shinyanga pale, anapiga simu watu wanaitafuta tinde., akapewa connection ya gari nyingine ila mpaka tunatoboa ubungo hakuna gari ya mwanza imeingia!
 
Mkuu mbona sikuhizi Hawakimbiii! Kuna siku nilitoka huko saa kumi na mbili, saa moja na nusu tulikua ubungo Shell, enzi zile kuna zile Ally's sports achana na hizi Ally's star.. 2011 hiyo, zilikuaga scania 95 hatari sana!
Hazikuwa 95 zile....nyingi zilikuwa F114 330 chache 94. Hayo ma F330 yalikuwa yana mwendo si mchezo.
 
Hazikuwa 95 zile....nyingi zilikuwa F114 330 chache 94. Hayo ma F330 yalikuwa yana mwendo si mchezo.
Yeeeeeeees.., nilisahau Mkuu, ndio hiyo! Tahmeed nae anazo hizi engine ila shida ni VTS tu.
 
Ndio barabara yenye bus nyingi

Allys
Tungis
Tanzanite
Happy nation
Kibo
Kisbo
Isamilo
Kisesa
Zuberi
Abood
Najimunisa
Dar lux
Na N.K

Mbona madereva wanapeana nafasi ktk kupitana
Hawana kubaniana

Shinyanga mnaingia pamoja
Singida mnaingia pamoja ktk misosi
Hata dodoma pia.

Kuachana kunaanza Dom kuelekea Moro hapo akikutangulia mtu amekutangulia aiseh
Bila kuitaja Phoenix hiyo list yako imeniudhi
 
IPO siku utakuja kuzinduka ukiwa KABURINI.
Kufa kupo tu unaeza fia usingizni,unakuta watu wana haraka na mishe zao mzee. Ushapanda Sai Baba ya Nairobi? Au buffalo na Ngorika miaka ya 2004?
 
Kumbuka njia ya dar-mwanza inajumuisha mikoa ya kanda ya ziwa,mikoa ya kanda ya kati na mikoa ya magharibi.hivyo ni njia yenye mabasi mengi sana ndio maana kunakua na league za kijinga.
Sio ligi za kijinga bob, kila mtu anataka kuoata jina kubwa kwa abiria ww zubaa kama Sai Baba ukimbiwe na abiria
 
Tumetoka hapa Nyegezi Stand muda si mrefu.

Aisee, haya mabasi yanakimbizwa hatari. Naona kuna ligi flani inafanywa barabarani.

RTO wa mikoa husika chukueni hatua.
Sasa si utaje umepanda gari Lipi Kati ya hayo Mkuu,nianze nalo?!Nipo Kazini muda huu ..
 
Toka nipate ajali na basi la Ally's Star mwaka jana, sina hamu na hiyo njia tena. Bora nijichange nipande pipa tu.
Mkuu Pipa siyo Hatari zaidi?!Hilo hata viungo nasikia vyaweza visionekane hata Kimoja !?
 
Mkuu si kweli kwamba Mwanza- Dar ina gari nyingi kushinda njia nyingine kwa mfano Dar -Arusha.
Hizo kampuni nyingi huwa ni gari moja tu inatoka Labda Ally star Ndio huwa anatoa 3
Acha bwana Zuberi hutoa mpaka 5.
 
Jamaa walikua wanatembea sana, then hakuna muda wa kupoteza, nakumbuka tuliacha mtu washroom shinyanga pale, anapiga simu watu wanaitafuta tinde., akapewa connection ya gari nyingine ila mpaka tunatoboa ubungo hakuna gari ya mwanza imeingia!
Tuliwadhibiti
 
TRAFIC Police Mkuu....Nilipanda mule siku Moja Saa 11 alfajiri Toka Mwanza....Saa 12 kamili jioni eti tupo Ubungo Mataa!!!Nillichukia mno...2012 ...nakumbuka mpaka leo.
Bora Mkuu! Hiyo siku iligongwa gia na Dereva mmoja alikua anaitwa Mzee Paulo! Tulipotoka Gairo kuitafta msamvu mzee alimwaga moto mpaka nikaanza kujilaum kwanini sikuandaa zuberi au master city!
 
Siku hizi bus hazikimbii mbwembwe tuu,zamani sawa zimefungwa VTS na Latra zote labda mtu achezeee
 
Back
Top Bottom