Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Kuna basi linaitwa SuperFeo ya kutokea Moshi kwenda Songea wana kiburi na dharau kwa abiria. Abiria unaburuzwa kutoka Moshi saa 12 asubuhi chai saa 8 Dodoma pale FourWays wana hoteli yao chakula ni kiporo na sahani wanauza sh. 8000. Kuna hoteli nzuri Babati hasa pale Himiti bei ndogo
 
Tafuta tuu hiyo afu nane, watu wameshalamika sana, ila ukumbuke cheap is expensive... Utauziwa afu tatu kilomita mbili nyingi tumbo linaanza kuvuruga
Uzuri wa chakula siyo bei. Vile vyakula vyao vingi ni viporo. Mamalishe wanapika vyakula vizuri halafu vya moto, kwanza hawana fridge viporo watatoa wapi
 
Sio mbaya ukinunua mkate, maji au soda ukiwa stendi ya magufuli kuepuka adha ya kununua au kutamani chakula cha watu wanapoenda kula sehemu hizo ulizotaja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…