Zamani ukitoka mbeya na bus letu kamata au relwe na wengine wote kituo ni rujewa mnapiga chai,mikate mayai,
Safari inaendelea.
Iringa ngoma inapanda juu stendi mnaenda kupiga menyu popote hali yako tu.
Mama ntilie kibao ,una hela kulikua na hotel pote pale.
Unakula mnatimua.
Kwenda Dom Mtera hapo mkipanda king cross,shalawambe au Urafiki mkifika pale bwawani kuna wamama walikua wanauza msosi mtamu balaa.
Wali maharage unapewa bonge la perege.
Bei 500 tu enzi hizo.
Manyoni stendi pale bus linasimama mnaambiwa kaleni mnakotaka kuna waarabu wana mahoteli kibao pale mnakula na dereva haondoi gari km mtu hajakaa mle ndani.
Kulikua hamna haraka.
Njia mbovu yaani abiria mpk mnakua ndugu.
Singida Iramba gari iguguno pale inapigwa kigogo mnatafuna kuku kienyeji km wote,unabeba dumu lako la maji twenzetu maana kufika ni majaliwa.
Singida-Arusha babati breki mnakula mbuzi mpk mkome mnazama kwenye mchuma safari inaendelea.
Dodoma-Arusha ,kondoa pale ikisimama bus mtakula nyama mpk za porini.
Haya tukiunga Mtwara-Dar kula Rufiji tu au Nangulukulu.
Hapo mi nilikua natafuna samaki tu.
Mnaopenda Nyama huwa mnalishwa vitu vya ajabu tu huko njiani.
Siku tulikwama porini hapo mbele ya nangulukuru matopeni ikachukua siku nzima kuchomoka.
Tumefika kijiji jirani Somwe sijui tuna njaa balaa.
Tukazama vihotel vyao aloo yaliletwa mapande ya manyama sio ya nchi hii.
Na viazi,mi nilitafuna viazi na chai maziwa poa.
Enzi zetu ukisafiri kufika ni majaliwa.
Tunatoka nyumbani na mabumunda,maandazi dumu la maji lita 5-10,nyama za kukausha(biltongs) kibao
Hamna cha juice,wala soda
Mkikwama huko njiani hata wiki unasurvive.
Sasa siku hizi kuna hawa matapeli wa usafiri mnakoma.
Mi nakula mwewe tu then naunga gari nikikaribia bush.