Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Zamani ukitoka mbeya na bus letu kamata au relwe na wengine wote kituo ni rujewa mnapiga chai,mikate mayai,
Safari inaendelea.
Iringa ngoma inapanda juu stendi mnaenda kupiga menyu popote hali yako tu.
Mama ntilie kibao ,una hela kulikua na hotel pote pale.
Unakula mnatimua.
Kwenda Dom Mtera hapo mkipanda king cross,shalawambe au Urafiki mkifika pale bwawani kuna wamama walikua wanauza msosi mtamu balaa.
Wali maharage unapewa bonge la perege.
Bei 500 tu enzi hizo.
Manyoni stendi pale bus linasimama mnaambiwa kaleni mnakotaka kuna waarabu wana mahoteli kibao pale mnakula na dereva haondoi gari km mtu hajakaa mle ndani.
Kulikua hamna haraka.
Njia mbovu yaani abiria mpk mnakua ndugu.
Singida Iramba gari iguguno pale inapigwa kigogo mnatafuna kuku kienyeji km wote,unabeba dumu lako la maji twenzetu maana kufika ni majaliwa.
Singida-Arusha babati breki mnakula mbuzi mpk mkome mnazama kwenye mchuma safari inaendelea.
Dodoma-Arusha ,kondoa pale ikisimama bus mtakula nyama mpk za porini.
Haya tukiunga Mtwara-Dar kula Rufiji tu au Nangulukulu.
Hapo mi nilikua natafuna samaki tu.
Mnaopenda Nyama huwa mnalishwa vitu vya ajabu tu huko njiani.
Siku tulikwama porini hapo mbele ya nangulukuru matopeni ikachukua siku nzima kuchomoka.
Tumefika kijiji jirani Somwe sijui tuna njaa balaa.
Tukazama vihotel vyao aloo yaliletwa mapande ya manyama sio ya nchi hii.
Na viazi,mi nilitafuna viazi na chai maziwa poa.
Enzi zetu ukisafiri kufika ni majaliwa.
Tunatoka nyumbani na mabumunda,maandazi dumu la maji lita 5-10,nyama za kukausha(biltongs) kibao
Hamna cha juice,wala soda
Mkikwama huko njiani hata wiki unasurvive.
Sasa siku hizi kuna hawa matapeli wa usafiri mnakoma.
Mi nakula mwewe tu then naunga gari nikikaribia bush.
Hiyo ndo ilikuwa safari mkuu, Siyo siku hizi, viongozi wana tamaa, kila kitu wamegeuza kuwa biashara, bado biashara yakuuzwa watu,
 
• Jaribu kuwa seriously basi, hao waliowahi kufika akina nani sasa?
• Kuna safari nyingine siyo lazima mwambie mtu baki, na je kama unaojuana nao hawajawahi enda hiyo trip! Utamuuliza Nani, au tuwe tunapiga ramli kabla ya safari?
Kama safari ni ya siri lazima uweke pesa ya akiba, alafu mkuu kuna mikate ya bukubuku na juice za jero unaweza nunua, hakuna ulazima wa kuhangaika na mavyakula ya gharama wakati mfuko auruhusu.
 
Kama safari ni ya siri lazima uweke pesa ya akiba, alafu mkuu kuna mikate ya bukubuku na juice za jero unaweza nunua, hakuna ulazima wa kuhangaika na mavyakula ya gharama wakati mfuko auruhusu.
alafu mkuu kuna mikate ya bukubuku na juice za jero unaweza nunua,
Kwa hiyo mkuu, unashauri tuishi kwa style hii,?

wakati mambo yakiwekwa sawa, Abiria watakula chakula kizuri kabisa na kwa bei rafiki kabisa.
 
Zamani ukitoka mbeya na bus letu kamata au relwe na wengine wote kituo ni rujewa mnapiga chai,mikate mayai,
Safari inaendelea.
Iringa ngoma inapanda juu stendi mnaenda kupiga menyu popote hali yako tu.
Mama ntilie kibao ,una hela kulikua na hotel pote pale.
Unakula mnatimua.
Kwenda Dom Mtera hapo mkipanda king cross,shalawambe au Urafiki mkifika pale bwawani kuna wamama walikua wanauza msosi mtamu balaa.
Wali maharage unapewa bonge la perege.
Bei 500 tu enzi hizo.
Manyoni stendi pale bus linasimama mnaambiwa kaleni mnakotaka kuna waarabu wana mahoteli kibao pale mnakula na dereva haondoi gari km mtu hajakaa mle ndani.
Kulikua hamna haraka.
Njia mbovu yaani abiria mpk mnakua ndugu.
Singida Iramba gari iguguno pale inapigwa kigogo mnatafuna kuku kienyeji km wote,unabeba dumu lako la maji twenzetu maana kufika ni majaliwa.
Singida-Arusha babati breki mnakula mbuzi mpk mkome mnazama kwenye mchuma safari inaendelea.
Dodoma-Arusha ,kondoa pale ikisimama bus mtakula nyama mpk za porini.
Haya tukiunga Mtwara-Dar kula Rufiji tu au Nangulukulu.
Hapo mi nilikua natafuna samaki tu.
Mnaopenda Nyama huwa mnalishwa vitu vya ajabu tu huko njiani.
Siku tulikwama porini hapo mbele ya nangulukuru matopeni ikachukua siku nzima kuchomoka.
Tumefika kijiji jirani Somwe sijui tuna njaa balaa.
Tukazama vihotel vyao aloo yaliletwa mapande ya manyama sio ya nchi hii.
Na viazi,mi nilitafuna viazi na chai maziwa poa.
Enzi zetu ukisafiri kufika ni majaliwa.
Tunatoka nyumbani na mabumunda,maandazi dumu la maji lita 5-10,nyama za kukausha(biltongs) kibao
Hamna cha juice,wala soda
Mkikwama huko njiani hata wiki unasurvive.
Sasa siku hizi kuna hawa matapeli wa usafiri mnakoma.
Mi nakula mwewe tu then naunga gari nikikaribia bush.
Ahsante sana. Wewe kweli mkongwe unazijua vyema chocho na ulaji wa njiani. Nangurukulu mpaka kesho nikifika pale ni mwendo wa Samaki tu, sinunui vitu vingine.

King Cross amezingua sana kutonunua basi mpya, mpaka leo angekuwa king of road - Ira to Dom
 
Kwa hiyo mkuu, unashauri tuishi kwa style hii,?

wakati mambo yakiwekwa sawa, Abiria watakula chakula kizuri kabisa na kwa bei rafiki kabisa.
Jamaa anashauri twende na mode ya kuendana na kilichopo, hataki tuwe na mfumo rasmi wa mabasi kupaki stendi na watu kuruhusiwa kula popote wakupandapo. ABC yeye kajitengenezea mpaka Hotel, CATE Morogoro
 
• Mimi sijasema basi lisimame popote,

• Basi lisimame sehemu yenye unafuu wa mahitaji muhimu,
 
Kwa hiyo mkuu, unashauri tuishi kwa style hii,?

wakati mambo yakiwekwa sawa, Abiria watakula chakula kizuri kabisa na kwa bei rafiki kabisa.
Mkuu mwenye hotel amewekeza pesa kutengeneza miundo mbinu ya hotel, amelipa kod, analipa wafanyakazi, amenunua vifaa vya kwa ajili ya biashara(jiko, sahani, friji, mfumo wa ges kwa ajili ya kupika na vyombo vingine. Kumbuka vitu vyote hivi huuzwa kwa bei ya juu) na amenunua malighafi kwa ajili ya kutengeneza chakula, dereva na konda wanataka kula bure, mwenye basi anataka nae alipwe, wafanyakazi wamemuibia, kuna misimu haina hela kipindi cha biashara kutokana na watu kutosafiri sana.
Nb: kumbuka mtaji wa biashara ni mkopo kutoka benk.
Hivi mkuu unazani atumie njia gani ili aweze kumudu gharama zote za uwendeshaji wa hotel na yeye pia apate faida.
FANYA UJARIBU KUFIKIRI WEWE NDIO MWENYE HOTEL
 
Jamaa anashauri twende na mode ya kuendana na kilichopo, hataki tuwe na mfumo rasmi wa mabasi kupaki stendi na watu kuruhusiwa kula popote wakupandapo. ABC yeye kajitengenezea mpaka Hotel, CATE Morogoro
Hii tabia ni mbovu sana siku hizi na watu wanakariri.
Mabus ya Mbeya mnashushwa hapo ilula aljazeera dk 10.
Kijipande cha kuku na viepe kisahani 8000 vimishkaki vya ajabu kimoja buku,bufee ndani mule mivyakula imeoza sahani 5000 na utakoma njiani tumbo.
Mi huwa nangoja Iringa pale chini,samaki wa mtera kachomwa nanunua sinia zima na mahindi ya kuchoma ya kutosha na maji kubwa natafuna njia nzima
 
Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.

• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma

Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.

Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.

1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?

2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini

Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
Kimsingi maeneo ya Huduma za Chakula wanakopaki zile bei sio halali ni wizi mamlaka husika fanyieni kazi hili jambo.
 
Natumia matakro yako
Mkuu,matusi ya nini?hapa tunajadili mambo yakusafiri kikawaida tu.
Mjibu mwenzio kwa staha.
Ukianza matusi humu kuna watu wanatukana mpaka we utajiblock mwenyewe.
Hizi ni story tu za utamaduni huu kushusha watu mahali wakale na kwenda choo dk 10.
We unaona inawezekana?
Sasa hapo jadili hoja,mambo ya matako we unayo pia
 
Kimsingi maeneo ya Huduma za Chakula wanakopaki zile bei sio halali ni wizi mamlaka husika fanyieni kazi hili jambo.
Kabisa mkuu, njaa inauma unalazimika kununua, na huwa wanafanya makusudi, wanawatembeza route ndefu, ili akipaki bas sehemu anayotaka, anajua kabisa lazima mtanunua tu chakula.
 
Back
Top Bottom