Fursa Pesa
JF-Expert Member
- May 30, 2012
- 4,631
- 3,527
Ndiyo,tena safi kabisa.Sasa basi zima kila mtu abebe hotpot, Inakuja kweli hiyo?
Hii itawafanya wengi kubadili kasumba iliyozoeleka sasa,muhimu ni kuzingatia ni menu gani muhimu Kwa safari.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo,tena safi kabisa.Sasa basi zima kila mtu abebe hotpot, Inakuja kweli hiyo?
Hao feo ndio wanasimama mafinga pale ushuz mtupuKuna basi linaitwa SuperFeo ya kutokea Moshi kwenda Songea wana kiburi na dharau kwa abiria. Abiria unaburuzwa kutoka Moshi saa 12 asubuhi chai saa 8 Dodoma pale FourWays wana hoteli yao chakula ni kiporo na sahani wanauza sh. 8000. Kuna hoteli nzuri Babati hasa pale Himiti bei ndogo
Tatizo ule utaratibu wetu wa zamani wa kuandaa vitu vya safari tumeuacha.
Ni vizuri kujiandalia chakula unachokipenda ili kuondoa usumbufu wenye kuweza kukuletea madhala ya shida za mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
Lakini ni vizuri kushauri namna iliyo bora hasa ni lishe gani za kisafari zilizo muhimu.
•Lakini ni vizuri kushauri namna iliyo bora hasa ni lishe gani za kisafari zilizo muhimu
Balozi wenu wa Cuba alianzisha program flani ya kuelezea kero ili zifanyiwe kazi, nakumbuka hili nalo aliwahi kupewa na alipokuwa anaendelea kulipa ufumbuzi mkaanza kelele na ngoma juu.
Baadaye na kwa gafla chuma akatoweka ndipo issue ikafia hapo.
But jamaa alikuwa karibu apate ufumbuzi as wasilazimishe abilia kula kwenye hiyo migahawa ambayo madereva wanapokea posho ya 10kl au 20kl kila wanaposimama na wengine wanachukua mshahara kila mwezi.
NB. Ushauri wangu kwako msafiri, naomba kila ujuapo unasafiri chukua mkate wako wa brown, peanut butter, juice, maji na peremende zako kadhaa kaanze safari.
Hizo kelele zilipigwa na CCM au wananchi?,Balozi wenu wa Cuba alianzisha program flani ya kuelezea kero ili zifanyiwe kazi, nakumbuka hili nalo aliwahi kupewa na alipokuwa anaendelea kulipa ufumbuzi mkaanza kelele na ngoma juu.
Kwa hatua hii inaonyesha viongozi hatuna kabisa, zimebaki picha tu kwenye ukuta.Ushauri wangu kwako msafiri, naomba kila ujuapo unasafiri chukua mkate wako wa brown, peanut butter, juice, maji na peremende zako kadhaa kaanze safari.
Safari Dar-Mbeya treni ya tazara hutajuta,Mi kiukweli nikitaka kusafiri,nanunua soda,grand malt,ndizi mzuzu,matunda navyotaka vyote!
Nawahi kuamka ,naandaa kabisa chakula changu ,juice natengeneza usiku nailaza kwenye friji!
Njiani sinunui kitu inanisaidia hata kukwepa gharama tu,soda ya buku utauziwa buku jero barabarani...
Majuzi hapa nimeenda iringa, nikaambiwa na wajuzi wa safari za ardhini kuwa nikate basi linaitwa ABC UPPER CLASS ni VIP. Tukapelekwa kwenye hoteli yao pale Morogoro, nimezoea nikiwa safarini sili vitu vya majimaji. Nikawahi pale jikoni nipate angalao kuku kavu na ndizi/chips kavu. Ni maajabu sana ile hoteli mazingira mazuri sana, hoteli ya kisasa lakini vyakula utalia! Nimekuta kuna wali na mchuzi au chai na maandazi ya jana pekee. Kuuliza bei nikasema hapa Mtanzania wa kawaida hawezi kula kwa namna yoyote. Hii biashara ya vyakula waachiwe wachaga na watu wa kaskazini huko, hoteli zao pale Mombo ni za uhakika na vyakula vya motomoto.Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.
• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma
Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.
Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.
1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?
2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini
Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
Sio kweli, kwani mtaani tunaokula kwa mama lishe matumbo yanavuruga?Tafuta tuu hiyo afu nane, watu wameshalamika sana, ila ukumbuke cheap is expensive... Utauziwa afu tatu kilomita mbili nyingi tumbo linaanza kuvuruga
Sio kweli, kwani mtaani tunaokula kwa mama lishe matumbo yanavuruga?Tafuta tuu hiyo afu nane, watu wameshalamika sana, ila ukumbuke cheap is expensive... Utauziwa afu tatu kilomita mbili nyingi tumbo linaanza kuvuruga
• Upo sahihi kabisa mkuu, ubebaji wa vyakula kutoka nyumbani bado ni kero tu, kuna watu safari zao ni zaidi ya siku mbili au tatu.
• point muhimu ni kurekebisa/kushauri mamlaka itoe tamko. Litakalo kuwa na faida pande zote.
Mi sikula nyama yoyote,wenzangu waliitandika haswa.nilishiba viazi vyangu na chai ya rangi nikashiba kabisa.Wasiwasi wako tu...pale Kuna wanyama pori, swala kama wote nadhani enzi hizo kabla Kilimo hakijawa cha kukata misitu!!
• Yeah mkuu, tren inapita pori to pori lakini Huduma ni zuri sana kwa abiria wao,Safari Dar-Mbeya treni ya tazara hutajuta,
Unalamba first class
Mlimba kuna misamaki hatari.
Ukimtuma mtu kimbia pale lete viepe yai chap anarudi navyo unampa chake.
Unafika Iyunga umeshiba balaa na kinywaji mle unajinywea tu unaenda kula mbonji.
Km una hela msosi umo humo wa moto unagonga safari inaendelea.
Ni laki tu utafika Mbeya na kurudi na kula fresh tu.
Magari yaMbeya Wana mpishi wao sehemu Moja inaitwa Mtandika karibu na Ruaha MbuyuniUkifanya uchunguzi utagundua pia kwamba Madereva wenyewe hawali kwenye hotel hizo huwa wanalipwa hela tu , wao wanakula sehemu maalum , wana wapishi maalum humo njiani huwaletea msosi kwenye maeneo wanayoahidiana
Mama lishe halazi msosi mkuu walaji wapo mda wote km wewe.Sio kweli, kwani mtaani tunaokula kwa mama lishe matumbo yanavuruga?
Majuzi hapa nimeenda iringa, nikaambiwa na wajuzi wa safari za ardhini kuwa nikate basi linaitwa ABC UPPER CLASS ni VIP. Tukapelekwa kwenye hoteli yao pale Morogoro, nimezoea nikiwa safarini sili vitu vya majimaji. Nikawahi pale jikoni nipate angalao kuku kavu na ndizi/chips kavu. Ni maajabu sana ile hoteli mazingira mazuri sana, hoteli ya kisasa lakini vyakula utalia! Nimekuta kuna wali na mchuzi au chai na maandazi ya jana pekee. Kuuliza bei nikasema hapa Mtanzania wa kawaida hawezi kula kwa namna yoyote. Hii biashara ya vyakula waachiwe wachaga na watu wa kaskazini huko, hoteli zao pale Mombo ni za uhakika na vyakula vya motomoto.
😄😄😄,Nikawahi pale jikoni nipate angalao kuku kavu na ndizi/chips kavu. Ni maajabu sana ile hoteli mazingira mazuri sana, hoteli ya kisasa lakini vyakula utalia! Nimekuta kuna wali na mchuzi au chai na maandazi ya jana pekee
Yani vyakula lazima vitabaki tu, kwa sababu bei zao zipo juu, na basi likitoka hapo halisimami tena, Sasa hapo wanawatesa Abiria bila faida yeyote,Hii biashara ya vyakula waachiwe wachaga na watu wa kaskazini huko
Mama lishe halazi msosi mkuu walaji wapo mda wote km wewe.
Akirudi nacho home ni ukoko tu.
Huko manjiani kula miubwabwa na nyama mnakula viporo tu.
Beba kilo kitimoto kavu na ndizi njiani we unatafuna tu.
Mkuu ukoko huwa haubaki, bodaboda huwa wanaweka order ya ukoko sufuria zima pamoja na maharagwe ya kutoshaAkirudi nacho home ni ukoko tu
Tena hizo sehemu za vyakula zinakuwa mbali na mji hakuna alternatives.
Nakumbuka wakati natoka Morogoro kwenda Mwanza tukikuwa tukishushwa Singida, chakula bei af sina imani nacho. Awamu zilizofuata nilikuwa nachukua zangu broiler na chips kavu Morogoro kwa 3000 take away, ilikuwa wakishuka kwenda kula mimi natoa take away yangu wakirudi wanakuta nakula chips kuku taratibuu. Nasubiri wanaouza soda nachukua nashushia
Wanataka ukishuka usiende sehemu tofauti na pale, ndo maana wameziweka ndani ndani huko,Tena hizo sehemu za vyakula zinakuwa mbali na mji hakuna alternatives
Hii bwana natamani sio SiriSafari Dar-Mbeya treni ya tazara hutajuta,
Unalamba first class
Mlimba kuna misamaki hatari.
Ukimtuma mtu kimbia pale lete viepe yai chap anarudi navyo unampa chake.
Unafika Iyunga umeshiba balaa na kinywaji mle unajinywea tu unaenda kula mbonji.
Km una hela msosi umo humo wa moto unagonga safari inaendelea.
Ni laki tu utafika Mbeya na kurudi na kula fresh tu.