Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Korogwe sehemu gani mkuu, Au michungwani!
Sijui jina kuna stendi ndogo ya kizushi kosta nyingi za misiba zinaenda pale pia ndani kuna baa. Pamekaa kisela ila hizo mbuzi zinazochomwa hapo ni shida mkiingia tu mnagombaniwa maama wachomaji ni wengi....

Nipe mwongozo ni wapi km umepajua kwa hayo maelezo
 
Ni michungwani mkuu, Pale nyama ni uhakika.
 
Sana huwa nazikubali sana nyama za pale kwanza unajichagulia sio mahoteli anayosemea mleta mada unapewa vinyango kubwa kubwa zishapoa chipsi mafuta ili mradi vurugu
• Yeah, nikiwa nasafiri kwenda Tanga, pale lazima nipitie, nipate Nyama Choma.

• Hotel Zingine za wenye mabasi ni changamoto sana.
 
Njia nyingi huwa kuna machimbo hujutii pesa yako shida ni kupata huo uhuru wa kufika hapo
Yeah zamani ilikuwa hivyo basi linapaki sehemu yoyote ile ili watu wale wanacho kitaka, ila Madereva kwa sasa hawezi kukupeleka sehem ya aina hiyo, kwa sababu wanaangalia maslai zaidi Kwao.
 
.mwanza--Dar
• mbeya--Dar
• kigoma--Dar
•Arusha-- Dar
• Ruvuma--Dar

Wana paki kwenye hotel nzuri na chakula cha bei nzuri
Ruvuma - Dar ni uongo mtupuuu.
Yaan Mafinga na al Jazeera kitonga ndo sehemu nzuri?
Hauko serious wee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
nashangaaa kuwa watu wanacheka, huyo maMa kama na muona hivi sio poa kabisa
 
Ruvuma - Dar ni uongo mtupuuu.
Yaan Mafinga na al Jazeera kitonga ndo sehemu nzuri?
Hauko serious wee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ulamke mwana veve 😋,
 
Tafuta tuu hiyo afu nane, watu wameshalamika sana, ila ukumbuke cheap is expensive... Utauziwa afu tatu kilomita mbili nyingi tumbo linaanza kuvuruga
Wacha weeeee. Kwamba wale ndo wasafi? Kama dereva na makonda(wasaidizi/wahudumu kwenye basi) wanakula bure,watashindwa kusimama? Maana vituo wanavyosimama ukishuka tu imekula kwako. Kwenye elfu 7 au 8, kila buku ikiwa kufidia chakula cha dereva na watu wake,unadhani waizaji wana hasara? Sema mngeomba basi waruhusiwe na wapishi wa bei ndogo maeneo hayo. Nani atalishughulikia?! We nunua biskuti zako na soda kubwa na keki,jikaze. Kwa wenye watoto ndo mtihani
 
niliambiwa kikombe cha maziwa ni tsh2000
 
Wasukuma wataivamia hii thread mpka ishangae yenyewe si unaona nyie mnavyoshibaga kwenye sikuku wao ndo wanashiba hvyo kila siku then muwauzie kisahani cha wali 7000 wakati kwao ni kama salad na kuchangamsha mdomo wakiwa wametoka kula ugali
 
Siyo kila mtu anauwezo wa kupaanda ndege,
Safari ya ndege hata haina raha,ni huo unyama wa madereva tu na tamaa zao.
Ila kupanda Bus mpite mahali mpige menyu safi huko njiani mnapita,mikumi,gangilonga mafinga, huko kote vijijini raha tupu kuangalia yale mazingira.
Hii tabia ya kusema dk 10 ushuke,foleni ya chakula,ule,kwenda chooni ni unyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…