Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Jali afya yako unapoondoka nyumbani una hakikisha una vyakula vya kukaanga kama kuku au nyama na chapati zako kabisa na chupa za maji
Hapo utaishinda njaa na safari

Kula hovyo tatizo hao wanauza mpaka vilivyolala na ukianza kulalamika tumbo unalaumu tena
Kiukweli hoteli za vyakula barabarani huwa bei kubwa sio Bongo tu ni kila mahali duniani
Ukienda hata Ulaya ni hivyo hivyo tena utashangaa wanavyopandisha bei mpaka unanunua kwa shingo upande
Kwa bongo huwa najipanga toka nyumbani, sio kwa sababu ya bei hapana bali naogopa kuanza kumsumbua konda
 
Mkuu ndio maana kuna mikate na soda/juice za kopo. Kama ukigundua madreva wanapaki basi sehemu za gharama ya juu dawa ni kusafiri na mikate, viazi au mabumunda uwe unakula njiani taratibu bila shuruti mkuu.
Mkuu, we unahisi haiwezekani kubeba vitumbua kwenye Rambo?

• Lengo ni kutatua tatizo, Yani siku zima ushindie mikate na juice, ?
 
Kabisa mkuu, Hili suala liangaliwe upya,
Sijui wanatuchukuliaje wasafiri sababu hatuna option nyingine🤔 ila kuna siku nilienda Moshi na Kilimajaro Express sijui ni hotel yao ile atleast wanajitahidi chips safii nikashangaa maana nishazoea Mbeya kwetu mwendo mdundo chips zimepoaa 😀(sijui ni ulafi ila lazima nile njiani)
 
Wapande ndege dkk 45 to 60 wapo kwao hizo expenses za misosi wataziepuka
 

Jali afya yako unapoondoka nyumbani una hakikisha una vyakula vya kukaanga kama kuku au nyama na chapati zako kabisa na chupa za maji. Hapo utaishinda njaa na safari

Upo sahihi kabisa mkuu, lakini Madereva wastulazimishe tukale sehemu fulani.. Basi lisimame sehemu ambayo kila mtu awe na uhuru wa huduma.
 
😄 Siyo ulafi mkuu, safari ya masaa kumi na mbili kwenye basi, njaa lazima uipate tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…