Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

.mwanza--Dar
• mbeya--Dar
• kigoma--Dar
•Arusha-- Dar
• Ruvuma--Dar

Wana paki kwenye hotel nzuri na chakula cha bei nzuri
Dar-iringa, dar-dodoma, dar-njombe ,etc, kampuni ya mabasi ya ABC
Hawa wanapaki Kwenye hotel za mmiliki wa hayo mabasi tu, morogoro hapo!
Nauli zake ziko juu kuliko mabasi mengine,pia hizo hotel yake mabasi yanapisimama🙌🙌 uwe umejipanga!
 
Nunua biskuti na juice... hautakufa njaa kwa kukosa lunch siku moja
Nunua biskuti na juice,

• kwa nini tuishi kwa biscuit na juice, mamlaka zinakazi gani,?
• Hapa tunazungumzia Abiria kuwa huru wakati wa safari, mbona tren inahuduma zuri angalau, na inasimama kwenye vituo vya kawaida kabisa.
 
Usi complicate mambo ngoja nikupe life hacks, kuna kitu kinaitwa lunch box. Wewe kabla hujasafiri kwenda huko unakokwenda jiandalia chakula chako kifunge vizur, wakat wenzako wanasuka kwenye gari wewe ndio kwanza unatoa kuku wako unamla taratibu,

Hapo ume save cost mkuu,
Mzee wang ndio trick yake hii, anatoka nyumbani na kuku rosti, ndizi za kuchemsha barabaran huko ananunua maji tu.
Mwanzoni niliona mzee umri unamsumbua, lakini siku niliyolishwa chips kavu na nyama ngumu kuliko maisha yangu ndio nilielewa!!
 
Serikali inafahamu haya lakoni imekaa kimya, Hovyo sana
Mi kiukweli nikitaka kusafiri,nanunua soda,grand malt,ndizi mzuzu,matunda navyotaka vyote!
Nawahi kuamka ,naandaa kabisa chakula changu ,juice natengeneza usiku nailaza kwenye friji!

Njiani sinunui kitu inanisaidia hata kukwepa gharama tu,soda ya buku utauziwa buku jero barabarani...
 
Mzee wang ndio trick yake hii, anatoka nyumbani na kuku rosti, ndizi za kuchemsha barabaran huko ananunua maji tu.
Mwanzoni niliona mzee umri unamsumbua, lakini siku niliyolishwa chips kavu na nyama ngumu kuliko maisha yangu ndio nilielewa!!
Tena hapo mm nakaush kuku na ndizi zangu, hapo basi likisimama yangu maji tuu, kama mzee wako

Juzi kati mara ya mwisho kutua dar nikawa na chupa yangu ya juice ndani kuna juice yangu safii, kufika mombo ni mambo ya fresh from the farm, kutua bongo watoto wa uswahilini kaka kawaida na maneno yao kuona chupa wakaamza mzee chai tena, nikaona hawa watanijazia nzi ikabidi niwakubalie kuepusha lawama

Hayo mabasi yapo kibiasha kwa wafanyabiashara
 
Nafikiri sababu ni demand kubwa, yaani lazima utakula kwa hiyo wanapandisha bei wanavyoona wao ingawa sio sawa
Kama hawapati wateja na vyakula vinalala labda, ila wanauza sana tu
Na sidhani kama kodi kuna kodi hapo bali kajenga mwenye mali hapo
Hii ya kuwa na uhakika wa wateja ilibidi iwafanye wauze kawaida. Maana faida ipo, ila wao wamekaa kindezi kuwaza faida kubwa zaidi.

Balozi Polepole kwenye kipindi cha hoja za wananchi sijui channel ten aliagiza kuwa mabasi yasimame stendi dakika 20 watu wale vyakula kwenye migahawa waitakayo, na sio kuwalazimisha wale kwenye hotel moja.

Kabla ya utekelezaji akapewa ubalozi. Hayajatekelezwa mpaka leo.
 
et safar ya masaa 8 au 9 yaan sa kumi upo arusha unahangaik n vyakul mombo ... sa ingne nashangaa mtu anashukia same et anakul mombo nae kufuat mkumbo
Furaha ktk maisha ni zile good moments na hakuna starehe nzuri inayoleta furaha kama kula
 
Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.

• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma

Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.

Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.

1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?

2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini

Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
Point 💯.
Ahsante kwa kuusemea umma.
 
Huyo mama nae ni mjinga na mpumbavu, yani anajua fika hotelini chakula ni bei ghali yeye anaenda na hela ndogo alafu anataka huruma. Ukiona chakula cha hotelin hukiwezi na una watoto pika chako nyumbani beba kwenye hotpot wenzako wakishuka kununua wewe unashuka na chako unakula hakuna mtu atakuuliza. MUACHE KUILAUMU SEREKALI KWA UJINGA WENU.

Huyo mama nae ni mjinga na mpumbavu
Wengine safari ndo inakua ni mara ya kwanza,, kwa hiyo usiseme ni mjinga
 
Kwa hapo ni sahihi sio rahisi kihivyo .
Kikubwa serikali ingeweka utaratibu wa chakula kwenye mabasi na bei elekezi bila kusahau watu wa afya kuhakiki hivyo vyakula maana uchafu ni mwingi pia .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Naam mkuu, Labda siku Tukija kupata viongozi, wanaojielewa.
 
Sehemu nyingi tu mkuu,
nimesafiri na hiyo njia mara nyingi ila kwa elfu 7 kuwa bei ya chini kuna walakini mfano sehemmu kama aljazira bei ni 3000 wali maharage na mbogamboga,wali nyama 5000..ila msosi mbovu. Kuna ule mgahawa wa kinyanambo na iringa pale ndo jau sambusa tu inafika 1000 ila bado wali bei ya chini sio elfu 7.
 
Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.

• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma

Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.

Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.

1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?

2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini

Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
Siku nyingine tumia akili kidogo, hizo sehemu wanazosimamisha mabasi, watu si lazima wale chakula cha hapo inaposimama basi, wengine wanapata pa kujisaidia, sehemu safi na salama.

Nakushauri uwe unabeba kabisa chakula chako cha kula njiani ukiwa na safari ndefu, hata kama una pesa za kutosha. Usafiri wa mabasi, hususan wa mwendo mrefu, siyo wa kuuamini sana, kuna basi kusimama kwa muda mrefu au hata kulala njiani kwa sababu tofauti tofauti.
 
Asante Mkuu kwa maoni yako! Kama LATRA wamepandisha nauli na serikali imeziba masikio haitaki kusikio kilio cha wananchi, na hili wanaweza wasikusikilize!
Mkuu nadhaini mtu akitaka kusafiri kama hana uwezo wa kula kwenye hotel hizo, afungashe chakula chake kwenye hotpots! Basi likifika kwenye maeneo hayo mtu anafungua chakula chake anakula!

Asante Mkuu kwa maoni yako! Kama LATRA wamepandisha nauli na serikali imeziba masikio haitaki kusikia kilio cha wananchi

Wanafanya hivyo kwa sababu, wanajua kabisa, uchaguzi ukifika kura watapewa kama kawaida.
 
S9k8 nyingine tumia akili kidogo, hizo sehemu wanzosimqmw watu si lazima wale chakula cha hapo inaposimama basi, wengine wanaenda kujisaidia sehemu safi na salama.

Nakushuri uwe unabeba kabisa chakula chako cha kula njiani ukiwa na safari ndefu, hata kama una pesa za kutosha. Usafiri wa mabasi, hususan wa mwendo mrefu, ssiyowa kuuamini sana, kuna kusimama au hata kulala njiani kwa sababu tofauti tofauti.

S9k8 nyingine tumia akili kidogo
• Mbona wewe haujatumia akili ku-comment, iweje mimi nitumie akili.?
• Nyinyi FIS EM ndo mnaleta umasikini hapa Tz
 
Back
Top Bottom