Huu ni utetezi wa hovyo kabisa...kwamba stend kama Nane nane Dodoma, Msamvu. Hakuna maeneo yaliyotengwa ndani ya stedi kwa ajili ya kutoa huduma ya chakula?
Maeneo yapo, lakini kwa kuwa hakuna usimamizi na nia thabiti ya kusimamia zitoe huduma, ndio maana madereva na wamiliki wa mabasi wanawapeleka abiria kula katika maeneo binafsi yenye bei za kuruka.
Angalia pale Singida, chakula 7000 hadi kumi ila kihalisia ni cha bei ya 2500 hadi 4000. Lakini ni nani asimame awasemee abiria?
Kwa wenye uchumi wa kati sawa lakini kwa mtu wa kuunga Unga aliyeunga kupata nauli ya 100000 kwenda Bukoba atamudu chakula kwa bei hiyo?