Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Ni ujinga tu! Kwani umelazimishwa kula hapo?andaa chakula chako nyumban gari ikisimama kwenye hivo vituo toa chako kula shida ipo wap?

Alafu kitu kingine upo safari safarini unakula kula ili iweje? Si unywe hata soda na biskuti ukifika unapokwenda utakula vizuri. Watu mnajiendekeza kula mataka taka ya njiani .

Binafsi ninapo safiri huwa nanua tende,maji na soda Basi mpka nafika silagi kitu kingine.

Nanunua tende kavu robo nakula mdogo mdogo na huwa sihisi njaa nikila tende nashushia soda tu na maji mpaka nafika.

Alafu kitu kingine upo safari safarini unakula kula ili iweje? Si unywe hata soda na biskuti ukifika unapokwenda utakula vizuri
Kwa nini, ulazimishe mtu aishi unavyotaka wewe?,

Binafsi ninapo safiri huwa nanua tende,maji na soda Basi mpka nafika silagi kitu kingine.
• Hivyo vyakula ulivyo taja hapo ni hobby yako wewe siyo mtu mwingine,
• Waache Abiria wachague wanacho taka, Siyo kupelepelekwa kama mfungwa.
 
na ndiyo aina ya viongozi tulionawo hawajali wananchi zaidi ya kushindana kupiga madili na kurishana madaraka
• So sad, binadam mwenzie anavyo teseka yeye ndo anafurahia, Kweli Africa is dark content.
• muafrika yupo tayari kumpa ardhi mzungu/muarab, alafu anamnyima muafrika mwenzie.
 
Muwe mnavumilia, njaa ya siku moja haiwezi kukuua.
Kusafiri sio mateso kuvumilia kitu gani?ile ni adventure tu.
Tunachoongea hapa mtu unafika stendi unakula na dereva anapumzika.
Tuliopanda ma Leyland enzi hizo ni saa nzima injini inapoa.
Mnakimbilia wapi?
Singida-Dom masaa 8 hapo njiani mshabondwabondwa sana kwenye mashimo.
Dom-Ira kupitia mtera kipindi cha mvua njiani siku 2.
Mbeya-Dar barabara yao nzuri tu ila ndo hivyo kufika usiku tu hata afanyaje.
Ndo wakaja,kina Zainab,tawaqal,southern comfort fujo zikaanza.
Siku hizi hizo Scania na yutong wanabet huku wamebeba maisha ya watu.
Kuna siku ndani ya bus kwenda Mbeya.
Dereva tumeanza nae vizuri tu.
Kufika iringa kapotea,bus yule konda kapewa.
Likawa linapepezwa km ndege ile inaenda kupaa.
Ndio niliacha kupanda Mabus.
Madereva ni wahuni tu siku hizi.
Zamani walikua watu wazima wenye kujitambua.
Sio sasa
 
Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.

• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma

Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.

Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.

1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?

2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini


Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
Hili tatizo limezungumzwa sana hapq ila serikali imeweka pamba masikioni. Angalau ujio wa safari za usiku utapunguza tatizo hili kwani unajilia nyumbani jioni kabla ya kusafiri.
 
Kipindi chenu, mulisafiri kistaarabu sana, ila kwa Sasa ni changamoto kubwa sana.
Kabisa,gari ikikwama ndo mnachimba dawa,mnarudi mnasukuma wenyewe.
Likitoka na matope yetu.dere atangoja tu mjae wote maana mbele hajui kitachotokea.
Mkijaa mnaanza tena,ni pori kwapori njia mbaya.
Hamuachi mtu njiani
Maana kiwaacha huko mbele nani atasukuma bus?
 
Back
Top Bottom