Ukweli kesi ya Mbowe Kila anaeifuatilia anajua kabisa kuwa kesi hii ni ya kutunga,na ukweli pia kesi ya Sabaya kila anaeifuatilia anajua kabisa kuwa kesi yake ni ya ukweli.
CCM wote wanajua kabisa kesi ya Mbowe ni ya kumkomoa,na CCM wote wanajua kabisa Kesi ya Sabaya ni kweli alfanya makosa yale.
Lakini Wana CCM hawawezi kufurahia Sabaya Kufungwa na hawawezi kufurahia Mbowe kushinda Kesi.
Kesi ya Mbowe ikifanyiwa masihara inaenda kuiaibisha serikali na kumpaisha Mbowe kimataifa.
Kesi ya Mbowe kama akifungwa itaenda kumfanya Mbowe kuwa mmoja ya wafungwa maarufu duniani kama Nelson Mandela,Mahatma Ghadi,Martin Luther King,Ken Saro Wiwa na Kenneth Kaunda.
Ifahamike kwamba makosa ya Mbowe sio halisia.
Kesi hii imeanza kivuta hisia za watu wengi ndani na nje ya nchi.
Watu hawafurahi Sabaya Kufungwa kwa sababu hawampendi,hapana,bali ni kwa sababu kafanya uhalifu kweli na watu wanajua.
Kama angekua hajafanya makosa kweli wangesikitika tu
Watu hawasikitiki Mbowe kuwekwa mahabusu au kushitakiwa kwa sababu wanampenda,hapana,kama angekua amefanya makosa kweli wangefurahi tu kushitakiwa na wangefurahi akihukumiwa kifungo.
Hao Mabalozi kuja mahakamani Kesi ya Mbowe sio wajinga,wala sio kwamba wanampenda sana Mbowe,hapana,bali wanakuja kushuhudia jinsi Mbowe anavyoonewa au jinsi gani maamuzi yatakavyofanyika.
Jamani ee!
Maamuzi ya Kesi ya Mbowe yatakua na athari kwa nchi yetu,
Sisi Tanzania Kila siku tunasemo wetu kuwa tunajenga nchi,au tunajenga Uchumi.
Tunaweza kuona ni masihara lakini kimasihara tu tunaweza kuona nchi yetu inatengwa kidogokidogo.
Kama tunabisha tukumbuke Zimbabwe iko wapi?
Kuwapoteza wadau wa maendeleo kama Denmark sio jambo Dogo.
kutengwa hakuji mara moja,kunakuaja kidogokidogo na kukufanyia kitendo cha Kujenga Uchumi kuwe kigumu.
Ushahidi wa ujambazi wa Sabaya hauna mashaka,
Lakini ushahidi wa Kesi ya Mbowe ina mashaka Sana.
Na kama Mahakama itafuata haki kwenye Kesi ya Mbowe Basi wale mashahidi na serikali wanastahili kufunguliwa mashitaka kwa kutoa ushahidi wa uongo na wale askari waliowatesha makomandoo wetu wanastahili kushitakiwa.
Tukisema Dunia mzima inafuatilia Kesi ya Mbowe tunamaanisha hivi.
Hapa Tanzania tuna mabalozi wa nchi nyingi Sana,mabalozi ni wawakilishi wa nchi zao,wapo mabalozi wanakuja mahakamani kufuatila Kesi hii na wale wasiokuja wanaifuatilia kwa vianzio vyoa wanavyovijua.
Kuna vyombo vya habari vya kidunia kama CMN, BBC,DW,VOA,Aljazeera ntc,Hawa wote hawana habari na Sabaya,bali Wana habari na Mbowe.
Sababu juu ni Sabaya kafanya makosa kweli na Mbowe hajafanya makosa kweli.
Samia anahujumiwa.
Mbowe sio Gaidi.