Madhara ya kumdanganya Mwanamke wakati Unamtongoza

Madhara ya kumdanganya Mwanamke wakati Unamtongoza

Kuna mshkaji wangu alkua anaazima gari yangu kila anavoenda kwa demu wake

Kumbe kule anasema gari ni yake na mimi ndio ninaazima kwake.

Basi siku moja yule dada alikua ana emergency anahitaji gari, akamuazima jamaa (hamaa hakumpa majibu ya kueleweka)

Mdada akaja kwangu straight akasema amekuja kuchkua gari yao

Ilibidi nianze kucheka kwanza[emoji23][emoji23]
Ungemuokoa mwana
 
Kuna dogo alimdanganya binti yeye ni Rubani... mbaya zaidi ni kwamba maisha aliyojivisha ni yenye standard kubwa kuliko! Wakitoka hata kwenda restaurant anayegharamia ni mwanamke. Dogo hata smartphone zile za TIGO za offa hana... ana simu ya tochi, anamwambia demu pesa ninayo ila kutoa sitaki... na alichomdatisha demu alikuwa anakaa Kariakoo kwa shangazi yake juu huko ghorofa ya nane "8" ..., yale maghorofa ya mtaa wa Livingstone na akadanganya pale kwake na anajenga hekalu jingine Kigamboni 😂😂😂🙌🏾.... uongo mwingine bana! Yaan ni mkubwa hata ukibebeshwa utaanguka na kupoteza maisha 😂

Yaliyomkuta alipogundulika mpaka leo hana raha, ingawa alimla mbususu binti mara moja kwa bahati... maana binti nae kwao mambo si mabaya.

Sasa tunamuulizaga dogo, "Hivi wewe Rubani unamjua au unamsikia?! Rubani unafkiri ni mtu wa mchezomchezo?! Unafkiri rubani anahangaika kutongoza mwanamke/wanawake?!

Ila sometimes wanawake mnatakaga kudanganywa wenyewe. Unadanganywa vipi na mtu ambaye hata kuandika vizuri sentesi ikaeleweka na kusomeka hawezi?!

JITAFAKARINI!
 
Kuna mshkaji wangu alkua anaazima gari yangu kila anavoenda kwa demu wake

Kumbe kule anasema gari ni yake na mimi ndio ninaazima kwake.

Basi siku moja yule dada alikua ana emergency anahitaji gari, akamuazima jamaa (hamaa hakumpa majibu ya kueleweka)

Mdada akaja kwangu straight akasema amekuja kuchkua gari yao

Ilibidi nianze kucheka kwanza[emoji23][emoji23]
Ahahahahaaaaa unacheka alafu unamwambia dem amwambie jamaa yake aje achukue wakutane hapo
 
Wakati unajifunza kutongoza unaweza danganya. Utadanganya kwa vile vitu vinavyokufanya uonekane una thamani. Nyumba, pesa, gari au unajuana na watu wakubwa.

Lakini haina maana ndo ukalie njia hiyo hiyo miaka yote. Ni muhimu ujifunze kumvutia na kumtunza mwanamke kwa mfumo unaosema ukweli na unaomfanya mwanamke akutake zaidi ye mwenyewe.

Hizi ni baadhi ya sababu kwanini usitegemee mfumo wa kudanganya kwenye kumvutia mwanamke.

Ni mfumo dhaifu.
Ni njia rahisi na ya haraka kumpata mwanamke. Lakini haina misingi mizuri.
Haina matokeo kwa muda mrefu. Hata maneno yako yanakua hayatoki moyoni.

Utapata urahisi kwa wanawake wasio na uzoefu wa wanaume, ila wale wenye uzoefu wataona uongo wako. Ni heri ujifunze kumvutia mwanamke bila kumdanganya kuliko kudanganya na kutumia muda mwingi kukumbuka uongo/ kukwepa uongo.

Utajisikia ushindi zaidi kwa kumpata mwanamke bila kumdanganya. Na utapa kujiamini zaidi.

Inaharibu mahusiano ya muda mrefu
Kwa mapenzi ya haraka haraka uongo utakusaidia. Lakini mahusiano ya muda mrefu atagundua tu ulipodanganya.

Ataona maisha yenu yote mliyoishi ni uongo. Na hatakua na haja ya kuendelea kuishi kwenye uongo. Na itakua ngumu kuweka mipango naye ya maisha. Hivyo, kama unataka mahusiano ya muda mrefu jiepushe na uongo.

Uongo unazaa uongo
Shida kubwa ya uongo ni kuutunza.
Ukisema uongo mmoja, inabidi uufiche na uongo mwingine mara mbili. Na uongo uongo marambili inabidi uufiche na uongo mara tatu. Mwisho wa siku unajikuta umejaa uongo.

Kitu kitakachozuia kujenga mahusiano imara kwa muda mrefu. Uongo pia unazaa na kuchochea tabia zingine zisizofaa.

Utavutia waongo wenzako
Ndege wafananao huruka pamoja.
Utajikuta kila mwanamke unayekua naye anakudanganya danganya tu. Kitu kitakachokufanya uamini zaidi kwenye uongo. Na kurudia mzunguko huo huo kwa kila mwanamke unayekua naye.

Cha msingi ni kujiepusha na uongo usio na maana. Na ili kuepuka uongo kirahisi, usijiweke kwenye mazingira yatakaokufanya useme uongo baadaye. Yaani jiepushe na vyanzo vya uongo.

Na hata ukitumia uongo, usiutumie sana kiasi kwamba ukashindwa kujitetea.

Share na Wengine Wapate Kujifunza.
Mleta mada katika vitu hujajua ni kwamba wanawake hawampendi mwanaume mkweli, sijui hizo tafiti zako umefanyia wapi, wanawake wanapenda mwanaume asiwe mkweli asilimia 90
 
Uongo ndo umeweka ndoa yangu kwenye mapito mabaya
Kipindi bado na mtongoza mke wangu nilimdanganya mambo mengi ambayo nilikuwa sina nikadanganya ninayo tulivyo kuja kuoana mke wangu alijua ukweli
Kila siku ni vurugo dah [emoji24][emoji24][emoji24]
Hapa ulikuosea mwanamke wa kuoa usimdanganye maana mnaenda kutengeza maisha yenu pamoja na ndiyo mtaishi maisha yenu yote, najua ameumia sana mkeo kwa hilo
 
Wewe danganya hit chukua video nyingi kabisa unasimamia ukucha hafu mwambie ukweli wooote hafu sikilizia sasa

Akizingua unakuwa unamtumia video moja moja mkibanduana ficha simu hakika ukimtaka lzm aje
 
Wanawake wanapenda maneno mazuri na story nzuri na drama za hapa na pale
Sababu mambo na vitu wanawake wanataka kwa wanaume vingi wanawaume hawana
Ukweli mtupu huo mkuu, na ndiyo maana wao wanatamani kusikia hata yasio na ukweli

Ila wale tunaowaoa tusiwadanganye maana ndoa ni jambo lingine kabisa linalohitaji kibali cha mwenyezi Mungu na sio ulaghai wa wenza bali ni Mungu aingilie kati ajue mtaishi tu pamoja na madhaifu yenu
 
Na tulipofika ukweli na uongo basi ukweli hauna nafasi katika mapenzi, mapenzi ya kweli na udanganyifu mapenzi ya kweli hayapo tena, usaliti, kuchepuka vs to stay royal basi usaliti unapokea kura nyingi

Tuishi tu vivyo hivyo tu, cha msingi angalia upo na nani ana malengo gani
 
Eva alimdanganya Adamu tule tunda tuliokatazwa na Mungu kwa maana lina uzima.

Udanganyifu mlianza kutufundisha nyie lakini
[emoji23][emoji23] Kwan Adam alikua hajui? Si walikatazwa wote? Adam alishawishiwa akaingia kingi kwa nn asikatae makosa ni ya wote.
 
[emoji23][emoji23] Kwan Adam alikua hajui? Si walikatazwa wote? Adam alishawishiwa akaingia kingi kwa nn asikatae makosa ni ya wote.
Adamu aliijua kweli ndiyo lakini sasa Eva alitumia mbinu danganyi ili amuingize Adam katika chaka kwa kumuaminisha tunda lina siri nyingi Mungu hataki wazijue,
 
Ukweli mtupu huo mkuu, na ndiyo maana wao wanatamani kusikia hata yasio na ukweli

Ila wale tunaowaoa tusiwadanganye maana ndoa ni jambo lingine kabisa linalohitaji kibali cha mwenyezi Mungu na sio ulaghai wa wenza bali ni Mungu aingilie kati ajue mtaishi tu pamoja na madhaifu yenu
Hata kwenye ndoa inabidi utumie uongo ili udumu naye
 
Niliwahi kumdanganya demu mimi ni mwanasheria kumbe uyo mwanamke nae ni mwanasheria, aiseee aliniuliza swali nikashindwa kujibu nikazuga naenda uani nikatokomea mbele kwa mbele sijawahi kuonana nae tena
 
[emoji1787]
 
Adamu aliijua kweli ndiyo lakini sasa Eva alitumia mbinu danganyi ili amuingize Adam katika chaka kwa kumuaminisha tunda lina siri nyingi Mungu hataki wazijue,
Wote wana makosa mana walikatazwa kwa pamoja wakajikuta wana akili kuliko aliewakataza.[emoji16][emoji16]
 
Danganya ila uongo ukaribiane na ukweli.

Ukijitia kuongea ukweli wote hupati mtu.
 
Back
Top Bottom