Nakumbuka mwaka fulani , tulipata safari ya Mwanza kwa wiki tukitokea Dar ..Sasa Taasisi yetu ina watu wachache sana ila bajeti kubwa , inawezekana kulikuwa na kikao cha Finance ila wakaenda hata watu wa HR,Procurement ili mradi pawe na wajumbe wengi .
Kuna mdada alikuwa ndio karudi kutoka kweny likizo ya uzazi (maternity leave) basi alitakiwa kwenda kama unavyojua akishamaliza basi anakuwa anarudi mapema kwake kwa ajili ya mtoto , masaa mawili kabla ya mda wa kutoka yeye anatakiwa kuondoka kisheria ili kwenda kumnyonyesha mtoto .
Sasa alitaka kwenda Mwanza na nafasi ilikuwepo kabisa kweny bajeti tena ilifemea watu wawili wengine walihitajika .Alipomuaga mumewe palikuwa na mgogoro mkubwa demu anataka zile per diem mil na point , nilikuwa namuheshimu ila baadae aliandika maneno kweny status kumsema mumewe.
Kati ya maneno hayo alisema kazi ni bora kuliko ndoa kwa vile anajiweza kulelea wanae , alisema pia yeye alisomeshwa na wazazi wake ili kuja kuwasaidia wazazi wake sio kutumikia ndoa . Kma mtoto anaweza kumuacha maana wana housegirl halafu akirudi atamnyonyesha ni wiki nzima tulikaa Mwanza , naye alienda .