Tusitiane ujinga ......this is very wrong, you have no idea what you're missing by NOT reading books. Hii ni hatari sana kuwa na mawazo ya aina hii. Ni hatari sana hata kwa ustawi na jamii yetu na kwa nchi. Kama unapinga tabia ya usomaji wa vitabu unataka watu wawe wanafanya nini mbadala wake?, toa suluhisho hapa wafanye nini badala yake. Usomaji wa vitabu ni chakula bora kabisa cha akili kwa mwanadamu. Mtu anayesoma vitabu mara kwa mara ameshiba kiakili, ana upeo mkubwa wa kuwasiliana na kuelewa mambo kwa marefu na mapana kwenye nyanja mbalimbali za maisha. Mtu anayesoma vitabu anajijengea uwezo wa reasoning au kujenga hoja (Reasoning is the action of thinking about something in a logical, sensible way). Asiyesoma vitabu ni sawasawa na mtu ambaye akili yake imekufa/imesimama, aliye mfu lakini anatembea, hawezi kujenga hoja, atakuwa bubu hata pale anapotakiwa kuchangia hoja fulani ya msingi, au hata akiamua kufungua mdomo wake atabishana si kwa hoja bali kwa povu na mabavu, au kupandisha sauti pasipo lazima. Kama wewe ni mvivu na si msomaji wa vitabu na wengine kama wewe, basi BAKI HIVYO HIVYO lakini usiwapumbaze wengine wawe kama wewe. Unaposoma kitabu kimoja maana yake unasoma wazo au kazi mtu iliyotafitiwa kwa muda wa miaka kadhaa. Unapomaliza kusoma kitabu kimoja ni sawasawa umemaliza kumsikiliza mhadhiri (Lecturer) mmoja anayetoa somo/mada fulani, maana yake ukisoma kitabu kimoja kwa mwezi tu, ni sawasawa na kuwasikiliza wahadhiri 12 wa vyuo vikuu. Kuna tofauti kubwa sana kati ya anayesoma vitabu na asiyesoma vitabu....kubwa mno! Usomaji wa vitabu una faida lukuki.
"You will be the same person in five years as you are today except for the people you meet and the books you read." By Charlie Jones