Madhara ya kuzaa nje: Familia inajuta mpaka leo kwa uamuzi walioufanya kwenye urithi wa kaka yao. So sad

Yaani tutafute mali miaka yote baada ya kifo analetwa mtu tu hukoo Ooh alikuwa mtoto wake soo what?Mama yake alivyokuwa anajua anatanua miguu kwa mume wa mtu alitegemea nini?Sarah kwenye biblia hii issue ilimuwia vigumu mimi ndio nitaweza.Niwe honest tu huu upumbavu ni moja ya vitu vinavyoumiza wanawake, kama nyie wanawake zenu wakicheat mnavyoumia na ndio na sisi pia.Kama mali ni za kupita huyo mtoto akapitie za wengine aachane na zangu
 
Busara wewe unaiyona ni sawa hapo kaka, tuelezee.
Cha kwanza kabisa ni kuona kama yule mama wa watoto wa kambo kuwa tayari kuwaachia watoto kwa utaratibu fulani kuchukuliwa na ndugu wa baba. Hicho huwa ni kipimo cha kubaini kama huyo mama kaja kuleta watoto au kafuata pension.

Pia hali kama hiyo inapotokea mnaweza toa urithi chini ya mwangalizi wa upande wa baba.
 
Cha kwanza kabisa ni kuona kama yule mama wa watoto wa kambo kuwa tayari kuwaachia watoto kwa utaratibu fulani kuchukuliwa na ndugu wa baba. Hicho huwa ni kipimo cha kubaini kama huyo mama kaja kuleta watoto au kafuata pension.
Akitaka kukaa na wanae
 
Ilitumika sheria gani kumnyima huyo mama % yake kwenye hizo nyumba mbili? Wote tumesoma sheria ngumu kukosa vyote kisa ushahidi tu. Kuishi nae kindoa ni ushahidi tosha
 
Hapa tatizo sio kuzaa nje, tatizo ni busara iliyotumika kugawa mali.

Busara isipotumika kwenye kugawa urithi hayo huwa yanatokea hata bila kuwa na watoto wa nje.
Fafanua kidogo boss busara gani inaitajika
 
Watumishi wa serikali ndio wanaongoza kwa kuzaa nje ya ndoa etii.??
 

Sasa binadamu akiamua yeye mwenyewe, kukata mawasiliano na kwenda kuishi mbali wewe unaumia na nini sasa? Au kuna mtu anaishi kwa niaba ya wengine?
 
Tatizo ni kuiga uzungu, ndoa siyo utamaduni wa mwafrika, umeletwa na wahuni. Mwafrica kazi yake ni kuijaza dunia. Kosa alilofanya huyo mzee ni kuficha damu yake. Alipaswa awatambukishe watoto wake mapema ili familia yake itambue ndugu zao.
 
Migogoro kuhusu mali za marehemu au mirathi inatokea hata kwa watoto waliozaliwa ndani ya ndoa, yaani wa Baba na Mama mmoja
 
Mmmmh hii tabu sana
 
Walisomeshwa na kuandaliwa mazingira vizuri, hawana muda na mali za baba wala nini. Shida ukute wote misheni town amna mchongo wa maana mnategemea kodi alafu na nyie mnaishi humohumo na wake zenuu....apa maji lazima yazidi unga
 
Kuna mzee mmoja ni tajiri tu. Anajiweza, magorofa kadhaa mji huo anapoishi na familia yake. Ni mfanyabishara mkubwa tu, ana wake wengi tu. Sasa hata watoto wake anaishi nao na hata kwenye hizo biashara utawakuta wote, wa mama yule mweusiiiii na wale wengine rangi ya mtume. Hapa nilishangaa sana na binafsi mbaka leo nashangaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…