Madhara ya kuzaa nje: Familia inajuta mpaka leo kwa uamuzi walioufanya kwenye urithi wa kaka yao. So sad

Ni kuweka wazi, by the way watoto wanapaswa kuwa waelewa tu! Wagawane kdg then waendelee kutafuta zao.
 
Wanawake ni WABINAFSI by nature
 
Acha kutisha watu mnaendeshwa na properties Marehu aliacha MKE, watoto kadhaa na wajukuu kadhaa sijawahi Sikia wakisa ameacha majumba magari ... Wale watoto wataendeleza ukoo bilamkujali Wana chochote . Uzuri ninkuwa tulivyovichuma duniani ni vya hapa hpa na Kwa matumizi ya hapa tu duniani
 
Ni kweli tunaviacha hapa duniani. Wengine unakuta ni vingi mno, wenye tamaa hata wasio wahusika na wao wanajichomeka humohumo wapate kitu
 
KATAA NDOA......
 
Sasa na yeye anakufaje kizembe
Msongo wa maawazo wa kujitakia, ni hizo mali ama ni nini? Kwani watoto waliozaliwa wana makosa gani. Huo ni ubinafsi.
 
matumizi mabaya msongo
usishikamane sana na vitu tumeyakuta tena tukuja uchi
 
Inaumiza,mmepambanaa weweee mmeejinyimaa wee,mshua anadodoka danga tu anakujaa takaa mgaoo na wanaee bila jashoo. Si aletee na zakee tugawaneeee!
kumbuka naye alikuwa akijibana na huyo mshua wenu, naye alitongozwa kama huyo mama yenu
 
Mama alikufa kwa roho yake mbaya akitaka mjane mwenzake ateseke na watoto wadogo bila pa kuanzia. Mumewe akifanya kuncheat sasa kwanini watoto ambao katika kucheat hawakushirikishwa wakazaliwa wateseke kisa baba aliyecheat kafa.
Tujifunze kusamehe na kusonga mbele. Alikufa kwa sababu ya kutosamehe
 
Hapo tatizo sio kuzaa nje ya ndoa,zingatia hili.Tatizo ni maamuzi yaliyofanywa na ndugu na mahakama.
Wanaume zaeni kadiri muwezavyo ila weka mipango sawa kabla haujarudi mavumbini.
 
Wanawake Wana tamaa mno na Mali za mwanaume utadhani Kama ndio hewa ama maji kuwa watakufa.
Sasa watoto wote ni wangu why wasipate. Suala la kuwasiliana na ndugu kwani mnaoishi nao hamuongei ama mnataka na huyo aje kuongeza kesi na shida, Mana nyie tu hapo nyumbani mnagombana , acha watu wakale nyasi wakiishi maisha yao wanapoona ni sahihi kwao.
 
Luka12:13 Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.
14 Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?
15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.
22 Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hiyo nawaambia, Msisumbukie maisha yenu, mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini.
23 Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
24 Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, na Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!
25 Na yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
26 Basi, ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo, kwa nini kujisumbua kwa ajili ya yale mengine?
27 Yatafakarini maua jinsi yameavyo; hayatendi kazi wala hayasokoti; nami nawaambia ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
28 Basi, ikiwa Mungu huvika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatawatendea ninyi zaidi, enyi wa imani haba?
29 Ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa; wala msifanye wasiwasi,
30 kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.
 
Kwahiyo ulitaka ndugu wamkatalie ndugu yao kuwatambulisha watoto wake kwao? Hata hivyo kilichotokea imetokea tu hii haina maana watoto wote waliozaliwa nje ya ndoa au huyo mama yao wapo hivyo.
 
Sisi kwetu, msiba wa baba 10 years back..Kuna watoto wa nje walikua wanajulikana kabisa na mwingine kaishi kwa bibi mzaa baba..LKN kwenye mirathi ukoo uliwakataa wote - bila kupepesa macho - ukoo ulisema haujawahi tambulishwa rasmi - unawaona wanaishi nao tu..ile pin ilikua hatari sana. Kumbuka mmoja alikua mkubwa kutuzidi wote, mwingine rika letu - anamzidi mdogo wetu wa mwisho...
Hawakuambulia hata 1000 - wale wazee walikataa katakata
 
Kuzaa nje ya ndoa kwa mwanaume HAINA MADHARA YOYOTE! BARAKA TUPU NA KAMA MWANAUME MSHUKURU MWENYEZI MUNGU!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…