To yeye
BILGERT
Wakuu mimi nimewahi ona kesi moja hivi wanandoa kuachana.
Wanandoa wale walijenga nyumba mbili, ila mahakama katika kuamua zile nyumba mbili alibakinazo mume tuu, coz ilionekana kuwa mume wake ndo kazijenga na majina ya nyumba ni ya mume wake.
Ila yule mama alisema alichangia kwenye ujenzi wa zile nyumba kiasi kikubwa tuu. Na yule mama Anakazi yake kabisa.
Ila ishu ni kwamba inawezekana kipindi anamchangia mume wake kuzijenga zile nyumba hakuweka ushahidi, na ndio yeye sababu ya kukosa nyumba hata moja, akatoka empty.
Ndoa nyingi ndivyo zilivyo mama anachangia mali bila kuweka ushaidi. Na hicho baadae kinawahumiza sana wanawake. Utakuta nyumba moja kila kitu ni Gharama yake ni million labda let's say 80. Ukute mama alichangia 25 million out of 80 million.
Ila ushahidi hana. Jina la nyumba ni la mume.
Sasa unafikili mama huyo atajiteteaje. Akija mtoto wa nje wanagawana sawa sawa na wa ndani , lakini kumbuka kuna jasho la mama ya ndani, hapo ndipo wanawake wengi wanapata maumivu bro. Usiseme ni roho mbaya kaka.
Na ndo maana wanawake wa siku hizi hawashirikiani mali z waume zao wakitaka kushilikiana basi anawambia amwandike na yeye kuwa kashiriki.
Wa mama wemgi siku hizi wanatafuta mali zao.