Soda 1 inakadiriwa kuwa na vijiko 10 vya sukari. Hii ni sawa na 100% ya mahitaji yako ya siku. Hivyo kunywa soda kila siku au mara kwa mara huongeza hatari ya kupata Kisukari.
Ndani ya dakika 20 baada kunywa soda, ini linaitikia kwa haraka na kubadili sukari yote iliyomo kwenye soda na kuifanya mafuta. Mafuta humfanya mtu anenepe na kuwa uzito kupita kiasi kitu kinachoathiri afya na kuharibu muonekano mzuri wa mtu.
Dakika 40 baada ya kunywa soda, mboni za macho hutanuka, shinikizo la damu huongezeka na ini lako huitikia kwa kuongeza kiwango cha sukari kwenye mfumo wa mzunguko wa damu unaohusisha moyo na mishipa ya damu.
Baada ya kunywa soda, kibofu hujaa na mtu kuhisi kubanwa mkojo hivyo kwenda kukojoa mara kwa mara. Kalisi (calcium), magnesi & zinki zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kuimarisha mifupa hupotea kwa njia ya mkojo. Pia maji, sodiamu na madini mengine hupotea.
Masaa zaidi ya mawili baada ya kunywa soda hali ya kujisikia furaha/vizuri (euphoria) huisha na sukari hupungua kwenye damu na kukufanya mwenye njaa, mchovu na mwepesi wa hasira.
TibaFasta