Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Jana wakati nipo zangu sehemu nmetulia kijiweni nikaamua kuagiza soda fanta passion nikawa nakunywa zangu taratibu huku nikipiga story na wana..mara akapita jamaa flan ambae simfahamu wala hanifahamu na kuja nilipokaa na kuanza kunishambulia kwa maneno kuwa nakunywa sumu kwamba mda c mrefu nitakufa kama nikiendelea kunywa hzo soda nikamuelewesha kuwa mm hz sinywi mara kwa mara inaweza tokea kwa wk mara mbili au mara tatu lakn jamaa akadai haitakiwi ninywe kabsa kwa kuwa ni sumu,cjakaa sawa nao wale jamaa wa kijiweni nao wakamuunga mkono jamaa yule mpita njia kuwa ni sumu
Sasa moyoni nikajiuliza kama hv vitu ni sumu mbn kuna shirika la kuthibisha ubora wa hivi vitu na hata kama kuna sumu mbona soda watu tumeanza kunywa mda tangu tupo watoto,na kama ni sumu kwan kazi ya ini ni nini katika mwl wa binadamu kama sio kupambana na hzo sumu?....wakuu hebu hii kasumba ipo vipi na je hili swala lina ukwel kiuhalisia???
 
Vizuri sana, ni swala zuri sana hili kujadili hapa! labda nijaribu kukujibu kadiri ya uelewa wangu !

'too much is harmful' hapa wazungu wanamaanisha 'ukizidi kiwango ni hatari' huu ni ukweli ambao haupingiki, kwamba kila kitu ukizidisha kiwango kinachohitajika ni hatari. Now nikirudi kwenye hoja. Soda ni kinywaji kama vinywaji vingine. Kinywaji hiki kiuhalisia hakina madhara kabisa kama utakunywa kuzingatia mahitaji kiafya.

kunywa soda moja au mbili kwa wiki au hata siku tatu sidhani kama kunashida yoyote kiafya, lakini kunywa soda mbili au tatu kwa siku moja lazima kutakuletea madhara. Hata maziwa freshi ukinywa kuzidisha kiwango kinachohitajika mwilini pia yanamadhara yake. Kwa hivyo ndugu yangu nashauri kunywa kuzingatia afya yako na ushauri.

Mwisho nasisitiza soda hazina madhara ukizingatia unywaji sahihi, na hata mara nyingine kama sukari itashuka utashauriwa unywe soda na wataalamu wa afya!
 
Tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa mwaka japokuwa kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku ambayo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo.

Biashara ya soda inalipa sana Duniani kwani ni kinywaji cha pili kinachoongoza kunywewa Duniani baada ya maji. Sasa ukiangalia unywaji mdogo wa soda kila siku kiafya una madhara makubwa kuliko unywaji mdogo wa pombe kila siku. Yaani ni bora unywe chupa moja ya bia kila siku kuliko chupa moja ya soda kila siku (simaanishi kuhalalisha matumizi ya pombe nayo pia hudhuru INI)

Yafuatayo ni madhara ya soda ambayo yatakufanya ufikirie mara mbili kunywa soda.
Jana wakati nipo zangu sehemu nmetulia kijiweni nikaamua kuagiza soda fanta passion nikawa nakunywa zangu taratibu huku nikipiga story na wana..mara akapita jamaa flan ambae simfahamu wala hanifahamu na kuja nilipokaa na kuanza kunishambulia kwa maneno kuwa nakunywa sumu kwamba mda c mrefu nitakufa kama nikiendelea kunywa hzo soda nikamuelewesha kuwa mm hz sinywi mara kwa mara inaweza tokea kwa wk mara mbili au mara tatu lakn jamaa akadai haitakiwi ninywe kabsa kwa kuwa ni sumu,cjakaa sawa nao wale jamaa wa kijiweni nao wakamuunga mkono jamaa yule mpita njia kuwa ni sumu
Sasa moyoni nikajiuliza kama hv vitu ni sumu mbn kuna shirika la kuthibisha ubora wa hivi vitu na hata kama kuna sumu mbona soda watu tumeanza kunywa mda tangu tupo watoto,na kama ni sumu kwan kazi ya ini ni nini katika mwl wa binadamu kama sio kupambana na hzo sumu?....wakuu hebu hii kasumba ipo vipi na je hili swala lina ukwel kiuhalisia???
 
Soda imesheheni sukari na sukari nyingi mwilini haina faida, zaidi inachangia unene. Ukiweza ni bora kupunguza matumizi ya soda na sukari kwa ujumla
 
Back
Top Bottom