Jana wakati nipo zangu sehemu nmetulia kijiweni nikaamua kuagiza soda fanta passion nikawa nakunywa zangu taratibu huku nikipiga story na wana..mara akapita jamaa flan ambae simfahamu wala hanifahamu na kuja nilipokaa na kuanza kunishambulia kwa maneno kuwa nakunywa sumu kwamba mda c mrefu nitakufa kama nikiendelea kunywa hzo soda nikamuelewesha kuwa mm hz sinywi mara kwa mara inaweza tokea kwa wk mara mbili au mara tatu lakn jamaa akadai haitakiwi ninywe kabsa kwa kuwa ni sumu,cjakaa sawa nao wale jamaa wa kijiweni nao wakamuunga mkono jamaa yule mpita njia kuwa ni sumu
Sasa moyoni nikajiuliza kama hv vitu ni sumu mbn kuna shirika la kuthibisha ubora wa hivi vitu na hata kama kuna sumu mbona soda watu tumeanza kunywa mda tangu tupo watoto,na kama ni sumu kwan kazi ya ini ni nini katika mwl wa binadamu kama sio kupambana na hzo sumu?....wakuu hebu hii kasumba ipo vipi na je hili swala lina ukwel kiuhalisia???