Madini aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi

Wewe utakuwa ni bonge la mjinga. Kweny ae vifo kuna utani? Narudia tena wewe ni mjinga kwelikweli!
Kwenye vifo alionesha kuumizwa na kusikitishwa na akatoa hadi salamu za pole. Utani alioufanya ni kuwaamba " kama wengine mazao yao yakifurika ,ninyi mkaline"
 
Sidhani kuwa Hana utu kiasi hicho...ila ni mioyo yetu tu iliyovurugika. Halafu kwangu mimi binafsi ni bora kuniambia ukweli kuliko kunilaghai.
Ukijenga bondeni ukafirikwa kubali matokeo.
Ukijenga barabarani ukavunjiwa sema Amina
Ukipewa mkopo ukashindwa kulipa utafirisiwa tu.
Hata hivyo unapaswa kuwa na tahadhari ingawa ukweli unaumiza lakini mengi yakupatayo Yana mchango wako. Siyo kila baya huletwa na shetani au Mungu mengine ni udhaifu wako tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha wafu wazike wafu wao...yeye anawaza mambo makubwa kama ndege ambayo inapita juu sana hivyo haiwezi kuguswa na mafuriko!
 
Haya ni matokeo ya kutesa na kupiga watoto.

Mtoto ukimlea kwa kumtesa na kumpiga, hilo linamkaa kichwani hata kwenye subconscious, anakuwa mnyonge, lakini na yeye siku akipata kuwa mkubwa/nafasi/cheo, anaona ni zamu yake kulipiza.

Kuna wachache wanaweza kuona historia yao ya kupigwa inawafanya wawe na huruma zaidi kwa wenzao, wengi wanakuwa wanaona kupigana na kunyanyasana ni sawa tu.

Ni haki ya mwenye nguvu kumsimanga na kumpiga mnyonge.

Ndiyo maana utasikia kauli hizi si mara moja tu kwa Magufuli, ni pattern.

Aliwasengenya waliopata tetemeko Kagera, alisema atawapiga mpaka shangazi za wapinzani wake, aliwasema watu wanaofeli katika nchi isiyo na mifumo kuwa ni vilaza, sasa anawasengenya watu waliopatwa na maafa.

Hii kitu Wajerumani wanaita schadenfreude. Ni mtu kufurahia maafa ya mwenzako, mara nyingi kwa wewe kujiona bora zaidi.

Kisaikolojia kwa undani kabisa inaonesha mtu hajipendi mwenyewe, ana machungu fulani na maisha, na hivyo, hawezi kupenda wengine.

Atawazodoa, atawasimanga, atawanyanyasa.

Matatizo haya si ya Magufuli pekee. Watanzania wengi wana matatizo haya.

Na ndiyo maana wengi wanamuelewa na kumshabikia sana Magufuli.

Maisha ya mtu hayana thamani sana katika jamii ya watu masikini.

Ukiyapa thamani sana, watu wanakushangaa wewe unayetaka kuyapa maisha ya mtu thamani.

Hawamshangai huyu anayeshusha thamani ya maisha ya mtu.

After all, kufa ni jambo rahisi sana katika jamii ya watu masikini, sasa ukishangaa rais anasheherekea watu kufa, watu masikini wengine watakushangaa wewe, unashangaa nini wakati hilo ni jambo la kawaida sana kwao?
 
Nimwjiuliza swali hilohilo. Kwanini Rais awaause raia walipa kodi wake kule bukoba lakini aidhinishe misada ikasaidie Msumbiji na Zimbabwe ? Mwenye jibu tafadhari
 
Kila kosa lina exception mkuu, kuna wale kweli wamefuata mkondo wa maji, wanatakiwa wafundishwe kwa kaa la moto.
 
Sijui kama unaelewa maana ya kuishi mabondeni kunakotamkwa na waheshimiwa hawa!!!?
Hata hivyo matamko ya Rais yanapotokea majanga kwa Wananchi yanakera na kudhihirisha tabia ya mtu katili asiye na huruma.
Kule Kagera: "Mimi sikuleta mafuriko..."
Dawa kuondokana na Utawala usio na huruma. Oktoba tafadhali tusipigie kura ukatili.
 
Kwa mantiki hiyo, sehemu kubwa ya waTanzania wote ni 'victims' wa kunyimwa haki ya yote hayo yaliyomo kwenye orodha uliyoweka hapo juu.

Kwa maana hiyo ni kwamba hawa 'victims' ni lazima akili ziwaingie kichwani...; tunarudi pale pale tulipoanzia kuhusu swala la 'akili kichwani'. Kama 'victim' atasubiri anayemnyima haki yake na kumsimanga ndie amtie akili kichwani, huyo mateka atasubiri milele.
 
MA Tanzania sisi mataahira wacha tutukanwe maana utayakuta hata kwenye huo uharo yalikuwa yanapiga makofi!
 
Sijabishia kwamba atasubiri milele.

Nimesema tu hawa ni victims na kuwalaumu ni kuwalaumu victims.

Kuna mwngi ya hawa victims kujipanga na kumaliza matatizo yao.

Ila si rahisi, maana unaweza kukuta victim mmoja polisi wa ngazi ya chini anatumika kuwakandamiza victims wengine wanaotaka kudai haki zao za msingi za kiraia.

Divide and rule style.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kama tatizo ni "kumlaumu 'victim'".

But, it seems fair to conclude the discussion based on the rest of the observation.
 
Duh! Aisee..
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kama tatizo ni "kumlaumu 'victim'".

But, it seems fair to conclude the discussion based on the rest of the observation.
Kwa nini kumlaumu victim kusiwe tatizo?

Na "the rest of the observation" mana yake nini? Observations gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…