Madiwani wa Temeke: Mkurugenzi alitumia ubabe kununua gari la milioni zaidi ya 400

Madiwani wa Temeke: Mkurugenzi alitumia ubabe kununua gari la milioni zaidi ya 400

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kauli ya Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, kuzitaka Halmashauri zilizonunua mashangingi ya bei mbaya mkoani Mwanza, kujieleza, imeendelea kuungwa mkono.

Baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam, wameibua madai mazito wakidai sheria ya manunuzi ya umma haikuzingatiwa wakati wa ununuzi wa gari la Mkurugenzi wao.

Badala yake, madiwani hao wanamlalamikia Mkurugenzi huyo Lusubilo Mwakabibi, wakidai alitumia ubabe kuilazimisha kamati ya zabuni kutekeleza matakwa yake.

Gari lililonunuliwa na manispaa hiyo ni Toyota Landcruser VXR, kwa bei ya milioni 470, huku wadau wa maendeleo wakidai manispaa inakabiliwa na changamoto nyingi za kijamii.

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi, Sekondari pamoja nakukosekana ama ukamilishwaji wa vituo vya afya.

Madiwani hao walidai japo matatizo ya kijamii Temeke yasingemalizwa na milioni 470 zilizotumika, lakini zingesaidia kupunguza adha za kijamii katika Manispaa hiyo kongwe.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alipotakiwa kutolea ufafanuzi suala hilo, hakutaka kulizungumzia kwa kina, badala yake alikiri kuwa ni kweli wamenunua gari hilo.

Pia soma> Wito: Waziri Jafo tumeona maelekezo ya Geita na Mpanda ni maamuzi mazuri, Temeke je?

“Ni kweli, tumenunua gari hilo, lakini sina majibu kuhusu hilo, mimi ni mtumishi, kuna mamlaka zinazoweza kutoa majibu kwa niaba yangu kuhusu suala hilo, asante.” alisema Mwakabibi.

Mbali na ununuzi wa gari, pia wamedai kuna ubabe unaotekelezwa na Mkurugenzi huyo kwa watumishi wa idara ya mbalimbali ikiwano ile ya zabuni na manunuzi, matumizi ya ovyo ya fedha za Umma kwa ajili ya ukarabati wa ofisi yake na thamani za ofisi hiyo.

Pia walidai fedha zinatumika bila kuidhinishwa na kamati ya Fedha, kwa
ajili ya kazi zikiwemo ukarabati wa nyumba na ununuzi wa thamani za ofisi na nyumbani kwa mkurugenzi zikiwamo TV kubwa.

“Kuna kamati iliyokuja kuchunguza mambo kadhaa Temeke, kamati ile kwa hakika haikufanya kazi, badala yake imeacha majeraha kwa watumishi waliohojiwa.” aliongeza kusema diwani mwingine.

Madiwani hao wamemuomba Waziri Mkuu, kuchukulia hatua kali dhidi ya mambo yaliyotekelezwa na Mkurugenzi huyo na wengine aliosaidiana nao, ili kuwa fundisho.

Wamesema hawataki kumfundisha kazi Waziri Mkuu, lakini wanashauri, Mkurugenzi huyo asimamishwe kazi, ili kupisha uchunguzi wa mambo mbalimbali, likiwamo suala la kudhalilisha watumishi.

Waliongeza kusema kuwa, wapo watumishi waliofikisha madai yao kwa ngazi za Wilaya, kwa maana ya ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo wakati huo, DC Felix Lyaniva, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

“Huyu ndio mkurugernzi wa kwanza Tanzania kutengeneza mahabusu maalumu ya watumishi, yaani mtumishi akichelewa kazini anawekwa mahabusu, ameweka kontena Manispaa kwa ajili hiyo, mtumishi anakaa mahabusu masaa kadhaa.” alisema mmoja wa diwani.

Waziri wa TAMISEMI Sulemani Jaffo, ambaye ndiye mamlaka ya nidhamu ya wakurugenzi nchini, hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo, lakini madiwani hao walidai kumfikishia barua ya malalamiko.
 
Mtoto wa Magufuli. Alisaidia ushindi wa CCM kule kwa Chiza. Baada ya kumtangaza Chiza akahamishwa usiku huo huo. Kuletwa Temeke. Kama akiweza sema hawezi kuongea na mwandishi wa habari, atashindwaje kuwa na mahabusu ofisini kwake. Tanzania ya Magufuli ina furahisha. Kila mmoja ni boss kwa nafasi yake..
 
Huyo Diwani aache uzwazwa. Huyo Mkurugenzi alijiandikia mhutasari wa kikao cha maazimio ya baraza la madiwani bila ya ridhaa ya madiwani?

Mbona wanakosa ujasiri wa kusimamia maamuzi yao?
 
Ile gari ya Geita ni tsh 460,000,000.00 hii ya Temeke ni tsh 470,000,000.00

Hapa lazima kuna ufisadi!

Ile kudhibiti vyombo vya habari lengo kubwa lilikuwa ni kupandikiza wizi na ukatili wa kimfumo. Hao Madiwani wanapiga kelele leo wakati wizi na ukatili mwingi wa kimfumo umeshika hatamu.

Hizo kelele hao madiwani wanapiga leo ili zikifike mahali fulani, lakini ukweli ni kuwa hao wakurugenzi wameamua kuwa wezi na wakatili kama walio juu, lakini wana uhakika wa kinga ya yule wa juu yao, ambaye anawatumia kwenye mambo yote machafu ya kimfumo.

Hao wakurugenzi ndio wametumika Uchafuzi wa chaguzi zote hapa nchini, wao ndio wanaojua kuwa CCM hawashindi wala kushinda kwa box la kura. Kama wanajua serikali iliyopo haina uhalali wa umma, wataogopaje huo umma?

Zile propaganda tulizokuwa tunasema ni utapeli kuwa nidhamu imerejea serikalini yako wapi? Huwa tunasema nidhamu haijarejea serekalini, bali vyombo vya habari vimezibwa midomo ili wizi na unyama ufanyike bila kufahamika. Haya ni baadhi tu ya unyama na wizi mwingi unaofanywa bila kuwekwa hadharani.
 
Katika hili la ununuzi wa mashangingi, watu wa kwanza kutumbuliwa inapaswa wawe.
1. Kassimu Majaliwa...

Hilo haliwezi kutokea maana hakuna wakuwatumbua, hakuna serikali adilifu ya kuwawajibisha. Kama serikali hii imepatikana kwa wizi wa kura, itapata wapi nguvu ya kuwachukulia hatua walioshiriki kufanikisha wizi huo? Kama ni hatua basi zitakuwa ni za tofauti ama chuki binafsi, lakini sio kwa sababu ya uadilifu.
 
Huyu ndio mkurugenzi wa kwanza Tanzania kutengeneza mahabusu maalumu ya watumishi

CCM mliitaka wenyewe,tena kwa wizi wa kura,pambaneni sasa

Tena alitakiwa atengeneze mahabusu ya chumba cha kemikali ili kutolea toucher. Maana sasa hivi watu wanafanyiwa ukatili, kisha wanatoka hapo wanasifia kuwa serekali hii ni ya wachapakazi.
 
Tena alitakiwa atengeneze mahabusu ya chumba cha kemikali ili kutolea toucher. Maana sasa hivi watu wanafanyiwa ukatili, kisha wanatoka hapo wanasifia kuwa serekali hii ni ya wachapakazi.
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom