Madiwani wa Temeke: Mkurugenzi alitumia ubabe kununua gari la milioni zaidi ya 400

Ile gari ya Geita ni tsh 460,000,000.00 hii ya Temeke ni tsh 470,000,000.00

Hapa lazima kuna ufisadi!
Kama nchi hatuwezi ku deal na ufisadi kwa kuangalia nani kufanya nn lini na wapi?.? Sheria kanuni na mfumo ipo kama haijafuatwa hicho ni kitu kingine. Ni matokeo ya kutegemea Rais /mtu badala ya taasisi inayoendeshwa kwa kujibu wa sheria. Juzi hapa mlitwambia rushes imeisha chini ya MAGUFULI hii nanini sasa???
 
Kweli mkuu Sheria zenyewe hazifuatwi Bali maneno ya kiongozi ndo yanafuatwa.Yaleyale ya kina ndugai ni mwendo wa kuvunja katiba waliyoapa kuilinda.
 
Huyo Diwani aache uzwazwa. Huyo Mkurugenzi alijiandikia mhutasari wa kikao cha maazimio ya baraza la madiwani bila ya ridhaa ya madiwani?

Mbona wanakosa ujasiri wa kusimamia maamuzi yao?
Jitahidi kuwa unasoma post na kuielewa kabla hujakimbilia kutoa ushuzi wako, hata kama unalipwa kwa kutetea basi jitahidi uwe unatetea mambo kwa hoja.
 
Majaliwa ni jipu.Yeye ndo anaidhinisha manunuzi hayo, baada ya JPM kulalamika kaamua kugeuka. Ningekuwa JPM ningemtumbua PM
Kweli kabisa Pm and amekalia kuti kavu, asipokuwa makini hili sakata huenda likamuondoa na kumpoteza mazima kwenye ulingo wa kisiasa
 
Jana kuna wadau wa maendeleo waliachwa solemba tangu asubuhi 8.30 kwenye kikao cha wadau wote wenye viwanda mkoa wa Temeke kilichokuwa kiendeshwe na Mkuu wa wilaya. Wadau walisubiri huku madiwani wakila nyama na matikiti maji na baadae wakaja kuwatoa wadau kwenye ukumbi waliokaa huku wakipiga miayo ya njaa na kupelekwa kwenye ukumbi mwingine. mwishowe wadau wakaona ujinga wakajiondokea kurudi zao mazini.
 
Majaliwa ni jipu.Yeye ndo anaidhinisha manunuzi hayo, baada ya JPM kulalamika kaamua kugeuka. Ningekuwa JPM ningemtumbua PM
Aliishapewa red light siku ya kuapa kwake, kwamba hana "gaurantee" ya kumaliza miaka 10! jambo linasukwa!!
 
Hii kitu itaondoka na Majaliwa
Haina haja ya kuondoka na mtu. Watolee muongozo kusiwepo tena na magx sijui mavx sijui v8 na mengine ya aina hiyo. Hayo yawe kwa Rais na PM na makamu wa rais tu. Wengine wote mkonga na zile land cruiser sijui LX. Hivyo. From now on

Hiyo iwe kwa taasisi yoyote ya serikali
 
Mbona Kuna Gari nzuri tu Kama hizi fortuner

Zimekaa kiboss na Ni Gari za kazi wangenunua hizo waachane na maGXr vxr v8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…