Madogo wa Kiume, Acheni Tabia ya Kuja Inbox Kuomba Hela

Madogo wa Kiume, Acheni Tabia ya Kuja Inbox Kuomba Hela

Inabidi nichunguze PM yangu nineona kuna meseji kutoka kwa member mmoja mwezi wa tatu na wa sita zote anaomba hela ya kula japo 10,000.

Kuna siku nimepost single ya stake ya 50,000 nikaona PM hiyo mtu anaomba hela ya kula.
Ambacho hawajui sisi wenyewe wababaishaji tu hatuna hela, ni ngumu sana kumsaidia 10,000 mtu usiyemjua wakati wewe mwenyewe tia maji. Ukiwa na shida unaanza kwanza na watu wa circle yako, ukiona hukopesheki au hawawezi kukusaidia ujue wewe ni tatizo.
 
Yawezekana ni kweli ila kwenye kuomba pesa, wanawake ni kawaida sana.
Naona mmeifanya kawaida hadi kwenu sasa.
Kingine business za PM kwangu mimi huishia PM na nikiona mwanaume anaomba pesa au fursa. Huwa najua kabanwa kweli kweli, aidha nimpe suggestion au nimuambie sina..

Kwa sababu hata mimi sio muombaji lakini kuna kipindi nilibanwa kwelikweli. Nikawafuata baadhi ya members hata kwa ushauri tu, na ni watu tunachat sio strangers. Waliponipa cold shoulder nikaelewa what to do lakini hakuna aliyekuja public hata kama hawakujibu chochote pm
Oooh kumbe!!! Ndio maana!
 
Kila uchwao mnatulalamikia wanawake kuomba omba hela. Ila sio rahisi mwanamke kumvamia tu mtu pm na kuomba hela.

Matapeli wengi hata wa "ile pesa tuma kwenye namba hii" ni wanaume. Mna njia nyingi sana za kuomba omba hela. Waomba omba hela pm wa jf wanaolalamikiwaga ni wanaume🙆‍♂️
Kwanza ni vigumu kujua ID ipi ya kiume na ipi ya kike humu JF, inawezekana wanaomba pesa ni wanawake ila yeye anasema ni madogo wa kiume.
Atume kwanza pesa aangalie majina ya miamala ndio athibitishe ni wa kiume au wa kike.
 
Kwanza ni vigumu kujua ID ipi ya kiume na ipi ya kike humu JF, inawezekana wanaomba pesa ni wanawake ila yeye anasema ni madogo wa kiume.
Atume kwanza pesa aangalie majina ya miamala ndio athibitishe ni wa kiume au wa kike.
Kesi karibia zote za omba omba wa pm zinazoletwaga humu huwa wengine wamethibitisha kabisa ni wanaume.

Hata wanaowatapeli wanaume humu kujifanya ni wa kike huwa bado ni wa kiume.
 
Jamani madogo hasa new members acheni hii tabia ya kuingia inbox za watu kuanza na Bro naomba hela ya kula.Ukienda inbox za watu 100 ukitegemea mmoja atakutumia pesa hiyo siyo sawa.

Pesa hutafutwa, siyo kuombwa ovyo. Kama kweli umekwama siku hiyo na una njaa anza kutafuta msaada mtaani kwenu hukohuko kwa majirani. Hata migahawani kuna uwezekano ukapata msaada wa chakula kuliko kutuma copy-paste kwa members

Bora hata uombe fursa, kazi au connection kuliko kuomba hela moja kwa moja. wanadhani kila mtu wa JF ni tajiri. Ukweli ni kwamba sisi ni akina nyie tu tupo hapa kutafuta madini, maarifa na habari.

Yaani ndani ya wiki moja nakuta meseji tatu tofauti zote zinaanza na Bro sikujui hunijui ila nina shida, nisaidie hela ya kula.
Ndo mana wangese ni wengi, nasema kama mtu unafukua mimavi huwezi waacha maana yanajizalilisha sana
 
Kesi karibia zote za omba omba wa pm zinazoletwaga humu huwa wengine wamethibitisha kabisa ni wanaume.

Hata wanaowatapeli wanaume humu kujifanya ni wa kike huwa bado ni wa kiume.
Sioni tatizo mtu kuomba hela kama katingwa , ila naona tatizo la aliye ombwa kuja kuanika hapa kuwa kaombwa hela ni tabia za hovyo tu
 
Back
Top Bottom