Madogo wa Kiume, Acheni Tabia ya Kuja Inbox Kuomba Hela

Madogo wa Kiume, Acheni Tabia ya Kuja Inbox Kuomba Hela

Jamani madogo hasa new members acheni hii tabia ya kuingia inbox za watu kuanza na Bro naomba hela ya kula.Ukienda inbox za watu 100 ukitegemea mmoja atakutumia pesa hiyo siyo sawa.

Pesa hutafutwa, siyo kuombwa ovyo. Kama kweli umekwama siku hiyo na una njaa anza kutafuta msaada mtaani kwenu hukohuko kwa majirani. Hata migahawani kuna uwezekano ukapata msaada wa chakula kuliko kutuma copy-paste kwa members

Bora hata uombe fursa, kazi au connection kuliko kuomba hela moja kwa moja. wanadhani kila mtu wa JF ni tajiri. Ukweli ni kwamba sisi ni akina nyie tu tupo hapa kutafuta madini, maarifa na habari.

Yaani ndani ya wiki moja nakuta meseji tatu tofauti zote zinaanza na Bro sikujui hunijui ila nina shida, nisaidie hela ya kula.
Bora umesema..
 
Daaah ila umaskini mbaya sana kmmke nilishawahi kuzama dm za wadau wawili nakaambulia patupu hiyo siku usiku wake chupuchupu nimpige kabari mstaafu mmoja mgonjwa halafu alikuwa ana kama laki mbili mfuko wa shati halafu anazurura usiku ila maadili yalinizidi nikavunga hiko kipindi ukinipa buku mbili nakuona kama malaika amenishukia.....

NB: Wadau niliowaDM sifa nyingi majina makubwa humu kumbe njaa kali tu, Ila pia nimejifunza kutodhihaki mapito ya mtu though me pia ukinidm unataka hela sitoi mia mbovu sio kwa ule msoto me wa kuuza maji stendi hahahaha.
 
Back
Top Bottom