Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

Akipatia sifa haziendi kwa washauri, ila mambo yakienda hovyo wakalaumiwa ni washauri! Ila chawa kazi mnayo. Ni mtu mjinga tu anaweza kuamini Kuna mabadiliko ya kweli yataletwa na wanaomini ni haki ya chama chao kukaa madarakani kwa njia yoyote ile.
 
Kuwa na msimamo basi .
 
Mzee wa kungata na kupuliza

UchaguZi unaokuja,panapo majaliwa mahudhurio,ushiriki
Ya upigaji kura utakuwa mdogo sana

Ova
Kabisa, hakuna mtu anayejitambua ataendelea kushiriki zoezi la danganya toto, wakati watu wana matokeo wayatakayo mfukoni. Kuliko kuendelea kupoteza muda kwenye uhuni ni Bora kufanya mambo mengine ya maana.
 
Mayala njaa inakuharibu sana
Sahihisha , njaa imemharibu na siyo inamharibu. Sijawahi kuwaelewa Wasukuma wanataka nini katika nchi hii. Wapowapo tuu pamoja na wingi wao most ni useless. Mf. Mboga ya Viazi, Kashakeu Dr., Mpini, Nyeti,Bitako nk. Ukiwasikiliza hoja zao, nje ya unafiki na uchonganishi,sijawahi kuwaelewa!¡
 
Ifikie wakati mambo mengine uyaache yapite kuliko kuyaongelea ukaharibu reputation yako maana kuna watu tunakuheshimu sana.
Asilaumiwe ili alaumiwe nani? Mbona mambo yakiwa mazuri hawasifiwi wataalamu anasifiwa yeye? Kwamba yeye sio mwanasheria ni kweli na mimi pia sio mwana sheria lakini nina uwezo wa kusoma sheria nikaona na kujua kwamba kifungu hiki ni kibovu na hiki ni kizuri,je huoni kwamba yeye kushindwa kutambua vitu kama hivyo ana tatizo na hivyo anapaswa kulaumiwa?
 
Nikushangaa sana jana ukaja unak8mbia kusifia kuwa lile fupa liliwashinda wengi Samia ameliweza. Leo tena unatuambia Samia asilaumiwe. Why?? Kwahiyo ungekuwa na mapendekezo mazuri tumpongeze Samia na ukiwa hovyo km ulivyosema walaumiwe wengine?
Brilliant
 
Wakati mwingine unaandika point lakini ukishaanza kuwaza teuzi unapoteza akili.
 
Hatujawahi kuwa na rais mwanasheria lakini hata Kenya walipobadili katiba hawakuwa na rahisi mwanasheria. Bunge linaongozwa na mwanasheria na ndilo linaongozwa kwa kupitisha na kubadili mikataba na miswada mibovu.
Hapo utaona tatizosiyo rais kutokuwa mwanasheria Bali uwezo wake wa kuchambua vitu.
 
Bwana Paskali Mayala (Magufulu alikuita Njaa) mwenye tatizo ni wewe siyo Rais. Hukumu ya Mahakama ya Rufaa huwezi ukaiita ni ubatili labda uwe na njaa kikwelikweli. Mgombea binafsi inaonekana ni kitu kizuri lakini ni lazima pawe na masharti. Mabilionea wa CHADEMA au Mo au Bill Gates au "Sauti ya Watanzania" wa Dr Slaa walio nje majambazi na watakatisha fedha kesho na keshokutwa watanunua kura zote tupate Rais binafsi atathibitiwa na nani? Kuhusu tumehuru, naamini kabisa tume iliyopo ni totally huru 100% kwa vile ni ya Majaji wa Mahakama ya Rufaa. Hata Kenya huwezi kumshitaki Rais mchaguliwa akishapitishwa na Supreme Court, sisi tume yetu ni Supreme Court tayari. Rais ndiye kielelwzo cha Nchi, ndiye sovereign, haiwezi kukawa na taasisi ingine juu yake au isiyowajibika kwake. Kwa maoni yangu Tume ya Uchaguzi ya sasa ni perfect, inatosha. Anything less ni kuipunguzia uhuru wake. Jambo moja mnalosahau ni kuwa Wajumbe wa Tume nao ni Watanzania, wana kura mija moja kila mtu. Hawawezi kutuchagulia mtu tusiyemtaka.
 
Akipatia sifa haziendi kwa washauri, ila mambo yakienda hovyo wakalaumiwa ni washauri! Ila chawa kazi mnayo. Ni mtu mjinga tu anaweza kuamini Kuna mabadiliko ya kweli yataletwa na wanaomini ni haki ya chama chao kukaa madarakani kwa njia yoyote ile.
Ila wasilojua ni kuwa binadamu asipopenda kufanya mabadiliko kwa hiari na kistaarabu basi utafikia wakati mabadiliko hayo huwa ni kwa nguvu na pengine yakiambatana na ukatili mkubwa.
Tumeona hivyo katika maeneo mbali mbali duniani. Jee nasi twataka iwe hivyo? Yafaa nini katika maisha kutengenezea shida na mateso ya kizazi chako kwa shibe isiyo halali ya leo?
Hebu viongozi waangalie ya Nyerere, hadi wajukuu leo wanaishi peaceful kwa ajili ya aliyofanya na mahusiano yake na jamii wakati wao acha watoto hadi wenyewe wako kwenye red alert!
 
Unategemea mchawi asimamie vita dhidi ya uchawi?
 
Inategemea unaongea na nani. Kama unaongea na sisi wananchi wa kawaida, wapiga kura wa CCM, basi huwezi kutuambia tusimlaumu SSH. SSH ndio mtumishi wetu. Sisi ni ma boss wa SSH(Rais aliyepo madarakani). Wasaidizi wake huwatafuta yeye baada ya sisi wananchi kumpa yeye kazi. Hao hatuwajui. Tunamjua Rais was JMT. Lawama za kila kitu tunaelekeza kwa Rais.
Kwa nguvu tuliompa anaweza kutafuta wasaidizi waaminifu na kuwachekecha kila wakifanya jambo na siyo kuwaachiaaaaaaaaa.
 
Maanake ukubwa wa taasisi ya urais hauna tija hata kama Rais si mwanasheria,pili tumekuwa na Marais copy and paste ambao wanajua kusaini bila perusing kwa hiyo kama kuchomekewa ni sababu ya udhaifu wao tu.

Anapofanga vikao na wadau mbalimbali inaonyesha haweki kumbukumbu ya kile alichokisemea kitu ambacho kina mfanya kuto deal na key point za speech zake pale anapoletewa kusaini.

Kelele zikipigwa site ndiyo anashtuka kuwa hee hili mlipitishaje,lakini hatusiki walio temper docs wamechukuliwa hatua. Hii nchi ngumu sana.
 
 
Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Hili hoja ya ubatili wa katiba yetu uliochomekewa kiubatili bado ipo mpaka leo kwa hiki kinachoendelea sasa kwenye vikao vya Bunge vinaendelea jijini Dodoma kupitishwa miswada 3 ya sheria, ikiwemo sheria mpya ya uchaguzi inayokwenda kupitishwa na ubatili ule ule!

Swali ambalo bado najiuliza, mambo haya ya ajabu hivi ya Bunge letu Tukufu kujadili sheria ya uchaguzi yenye kifungu batili kinachokwenda kinyume cha katiba ya JMT
yanaweza kufanyika vipi wakati tuna wanasheria manguli wabobezi na wabobevu wa sheria!, huo unguli, ubobezi na ubobevu wa sheria ni kwenye nini?.
P
 
Mchakato wa kuwapata Wanasheria wa serikali upoje?au ndiyo mwendo wa vimemo!
Ile aibu tulipata kwenye Mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara juu ya usitishwaji holela wa leseni za Madini ni balaa!, Wanasheria wetu bado sana!
 
Mchakato wa kuwapata Wanasheria wa serikali upoje?au ndiyo mwendo wa vimemo!
Ile aibu tulipata kwenye Mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara juu ya usitishwaji holela wa leseni za Madini ni balaa!, Wanasheria wetu bado sana!
Nafasi huo zinatangazwa watu wanaomba.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…