Madudu ya Mkataba wa Bandari yazidi kuonekana. Rais alisaini kwa niaba ya Serikali ya Dubai pia

Madudu ya Mkataba wa Bandari yazidi kuonekana. Rais alisaini kwa niaba ya Serikali ya Dubai pia

Imetokea kwa bahati mbaya au ilikuwa imepangwa na waarabu DP World kwa ujanja wao au ni uvivu wa wanasheria wetu kusoma kilichoandikwa kwa makini, na ni nani hasa aliandaa andiko hili. —-AND—.

View attachment 2686950.
Viongozi wavivu hata kuusoma mkataba. Wanajuu kusaini tu.. Tutakuwa coloni la waarabu baada ya miaka michache.
 
Dubai sio nchi, na haina government yake. Nchi ni U.A.E ambao kimsingi ndo walitakiwa kusign kama Government na sio Dubai. Ndo mana kina Mwakabusi wana baseline za kusema iyo contract ni null and void. Ila unakuta kina Jerry Slaa wanaojiita wasomi wenye digree 7 wanautetea ndo hapo unakuja kugundua kina Jerry shule haijawasaidia
Jerry Slaa mjinga sana anatafuta sifa kijinga mno anajidhalilisha tu. Mama mwenyewe hataki hata kuamini alichokifanya.
 
Yani mama kawapa Dubai zawadi ya bandari zetu baada ya kupewa rushwa
Upo sahihi. Rushwa na kuiuza nchi jumla. Hajali chochote hata kuongea na Watanganyika.

Maslahi ya waarabu ni muhimu kwake kuliko Maslahi ya Watanganyika.
 

Mmekazana sana na mambo yasiyo na kichwa wala miguu kwenye huo mkataba kama sehemu ya matatizo.

Pitia article 18 ya ‘VCLT 1969’ hizo signature ndani ya huo mkataba hazina nguvu zozote za kisheria pekee yake, bila ya ratification.

Nguvu ya kisheria kwenye treaty inakuja baada ya ratification ya bunge. Vinginevyo mikataba yote ya baadae terms zake ambazo zipo kwenye treaty azitambuliki mahakamani kama ratification aikufanyika.

Kwanza nchi ingeweza ata ikana hiyo treaty (IGA) yenyewe ata kama raisi mwenyewe angekuwa ndio la sign; provided katika muda huo bunge lilikuwa bado alijaridhia.

Yaani watu mmekezana na upotoshaji badala ya kuwabana hawa watu tujue huko mbele ni kipi hawa wakezaji wanatoa, wanarudisha vipi investment yao na win situation kwetu ina sura gani katika hiyo mikataba. Hayo mambo hawajifikia bado au ndio wanajadiliana kwa sasa nyuma ya pazia.

Lakini wapotoshaji mmekazana na mambo yasiyo ya kichwa wala miguu; kuivuruga serikali matokeo yake tunaweza ata kuwatoa umakini kwenye future negotiations ambazo huko sasa wakiingia kichwa kichwa ndio nchi inaenda tandikwa kweli.
Una akili kumshinda Shivji ama Nshala.
 
Concerning with economic and social partnership for development........
Mnaosema bandari imeuzwa hamjui kingereza au? Neno kuuza Kwa kingereza ni sell/sold!.
Aloyelioja hapo anionyeshe
Zingatia vipengele,masharti tuliowekewa.
 
Hiki ni kiwango cha ujinga ambacho sijawahi kukishuhudia nadhani katika hii karne nzima hakuna kiongozi duniani kote ambae amewahi fanya kituko kama hiki

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Hatimaye mangungo tumempumzisha.. Sasa hivi y
Tuna Samia, Tulia, mbawara na majaliwa hao kamwe tunatakiwa tuwasome kwenye bogus treaties Tanzania
 
Haya ni matokeo na ushahidi kuwa si rais, waziri wala mwanasheria wake mkuu hawajui kiingereza. Nadhani waliandika kiingereza kwa kiswahili. Kilichokuwa kimekusudiwa hapa ni the empowerment of the minister to sign the said agreement on behalf of Tanzania in the agreement between Tanzania and Dubai. Hili ndilo balaa la kuwa na viongozi wanaopenda kutumia lugha za wenzao wakati hawaziwezi. Si wangeandika kwa kiswahili tu ikizingatiwa kuwa andiko au mamlaka haya yangetafsiriwa kwa lugha safi?
Na raisi na pamoja Na lile jicho kubwa na miwani yenye magnification ya x4000 hakuona?
 
Kwa hiyo huu mkataba wameingia makanjanja tupu, ofisi ya mwanasheria mkuu walikuwa likizo?
Hivyo vyeo wanapewa kuwa kujuana ,ndio matokeo yake hayo ,mwanasheria wa serikali Anaandika kwa kingeraza kwa kiswahili ,na PHD holder naye anaanguka saini
 
Mkuu maoni yako ni yapi? Unaona huu mkataba hupo kwa maslahi ya Tanzania?
IGA sio mkataba wa kibiashara, kwa mantiki hiyo kama ulivyo auna shida yoyote ni standard structure ya treaties karibu zote duniani.

Maslahi ya Tanzania yatakuwa huko mbele kwenye mikataba ya ‘lease and project agreements’ ambayo watajadiliana TPA na DPW huko sasa tukipeleka mazwazwa wasiojua maswala ya biashara ndio tuta-tandikwa; na mimi siwezi jua quality ya TPA negotiators.
 
Ime editiwa au Mie sijaelewa?Rais anaongoza Nchi mbili?
Hao ni wanasheria wa DPWorld ndiyo walioandika hicho kifungu wakakikosea makusudi ili na sisi tupate mahali pa kusahihisha angalau tuonekane tumeshiriki kuandika mkataba. Lakini wakaona tumeamua kusaini bila hata kurekebisha hilo kosa.
 
IGA sio mkataba wa kibiashara, kwa mantiki hiyo kama ulivyo auna shida yoyote ni standard structure ya treaties karibu zote duniani.

Maslahi ya Tanzania yatakuwa huko mbele kwenye mikataba ya ‘lease and project agreements’ ambayo watajadiliana TPA na DPW huko sasa tukipeleka mazwazwa wasiojua maswala ya biashara ndio tuta-tandikwa; na mimi siwezi jua quality ya TPA negotiators.
IGA ya wapi Rais wa nchi moja anasaini kwa niaba ya nchi nyingine? Jitahidi angalau kupitisha macho usome hoja iliyopo mezani hata kama umeshapewa vipande vya fedha.
 
Ohooo sasa mambo mapya kabisa.

Nyie wapinga DP World, Ukraine wanataka DP World iendeshe bandari zao zote wanasema wezi wengi.
 
Back
Top Bottom