Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Kutokana na mfumo wa maisha ya sasa, ikiwemo hali ngumu ya maisha watu wameamua kuvunja sheria ili kujiingizia kipato kwa namna yoyote ile iwayo.
Maduka haya yamegeuka kuwa zahanati kwa kuendesha shughuli za. Matibabu tofauti na leseni waliyopewa
Mengi sana yamejificha nje ya maduka haya dawa za binadamu yaliyopo mjini na vijijini na baadhi ya watu wanalijiua hili.
Utoaji mimba, baadhi ya maduka ya dawa yamekuwa yakiendesha shughuli hii kwa kificho na baadhi ya wateja wao ni wanafunzi, na wakati mwingine hufanywa na wasiokuwa wataalam na hivyo chanzo za vifo kwa wahanga.
Wasiokuwa na elimu ya ufamasia kuuza duka la dawa, unakuta mtu katoka form four au kaishia form two, anaelekezwa kwa muda wa wiki moja na mwenye duka tayari anaanza kuuza dawa pamoja na kuchoma wagonjwa sindano na kusafisha vodonda wafikapo dukani kwake..
Matibabu kwa wagonjwa, kuna baadhi ya wagonjwa pindi waendapo duka la dawa kueleza dalili za maumivu ya Mwili wanayoyasikia basi muhudumu wa duka humpa dozi ya dawa kwa kukisia aina ya ugonjwa bila vipimo badala ya kumshauri aende hospitali.
Huduma za kujifungua, baadhi ya maduka yaliyopo vijijini hutoa huduma hii kwa wakina mama wajawazito wanaojifungua, na hata baadhi ya maduka ya mjini nayo pia yanafanya huduma hii kitu ambacho ni hatari kwa afya ya binadamu.
Hii ni hatari kwa afya ya binadamu na sio la kufumbia macho, maduka ya dawa kufanya kazi zinazotakiwa kufanywa na Hospital.