Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

Je mnampango wa kufanya biashara hata mikoa mingine kama Dodoma?
Kama jibu ni ndiyo, mnatarajia kufanya mchakato huo lini?
 
Je mnampango wa kufanya biashara hata mikoa mingine kama Dodoma?
Kama jibu ni ndiyo, mnatarajia kufanya mchakato huo lini?
Mkuu siwezi kukujibu ni lini hasa,kwasababu hata Dar-es-Salaam bado watu wengi hawajafahamu huduma hii kiasi cha kushawishi kuingia mikoa mingine, ila plans hizo zipo
 
Sio nyingi ukizingatia kwamba ukiwa na taxi ya kawaida unaweza kupark asubuhi mpaka jioni ukapata mteja mmoja tu.Lakini kwa Uber unapata trips nyingi,hivyo hiyo 25% hutaona kama kubwa sana
Nasubiria jibu lako mkuu
 
Mkuu siwezi kukujibu ni lini hasa,kwasababu hata Dar-es-Salaam bado watu wengi hawajafahamu huduma hii kiasi cha kushawishi kuingia mikoa mingine, ila plans hizo zipo
Sawa
 
Mhe Dricks /Uber kwa kweli network yenu inasaidia jamii kwa hili swala la usafiri mjini, Tatizo limejitokeza baadhi ya madereva hasa wa watu binafsi , makampuni binafsi hata mashirika ya umma(yenye Private Numbe) wanachukua kadi za magari (bila ruhusa ya mwnye gari)na kuja kujisajiri kwenu na bahati mbaya sana nyie hamuulizi IDHINI YA MWENYE GARI na wazi kabisa mnaona jina la dereva ni tofauti kabisa na la mwenye gari (kadi) bado mnamsajili kwa kuituia hilo gari kibiashara dereva akitumwa mahala kikazi nyie mnampa abiria mnagawana hizo pesa na mwenye gari hana habari na hapati kitu. swali langu:

1. Je hauoni kwamba UBER imeshirikiana na huyo dereva kumuibia /kumuhujumu mwenye gari ?

2. Hivyo hivyo dereva tax alieajiriwa kwa mkataba na mwenye gari analeta dereva mwingine (DAIWAKA) nyie mkijuwa kabisa wao sio wamiliki wa hilo gari mnawasajiri hata wanne kwa gari mmoja la mtu mwingine ? ?

............Sorry niko busy ntaendelea baadae kidogo jibu hayo kwanza
 
Kuna masharti ya aina ya gari na umri wa gari?
 
Mm nime download app yenu ila kila nikiita gari inasema network error. Nime uninstall na install upya ila bado. Nahitaji msaada wenu
 
Nyie uber hebu mnisaidie.
Mm nimepakua app yenu. Ila kila nikijisajili,inarudi mwanzo.

Yaan naweka namba ya simu,majina. Ile nikisema iendelee mbele,inarudi tena kwenye namba
 
Kwa Maelezo haya hayanipi uhakika Wa usalama Wa kutosha.

Kwann msifunge GPS devices kwenye GARI ?
 
Nyie uber hebu mnisaidie.
Mm nimepakua app yenu. Ila kila nikijisajili,inarudi mwanzo.

Yaan naweka namba ya simu,majina. Ile nikisema iendelee mbele,inarudi tena kwenye namba
Tatizo hilo huwa linatokea mara chache; naomba unitumie PM namba yako ya simu unayotumia kujisajili mkuu
 
Utashangaa Dereva wa uber aliekuja kukuchukua ni scorpion mtoa macho wa buguruni utatokaje nduki!
 
Mm nime download app yenu ila kila nikiita gari inasema network error. Nime uninstall na install upya ila bado. Nahitaji msaada wenu
Fanya hivi mkuu, hakikisha umeweka data ON na location ON. Pia hakikisha wakati wa kuinstall app ya uber ikikuomba permissions uiruhusu
 
Mkuu hayo nimeyapokea ntayafikisha kwenye uongozi; ila kama ukigundua mtu anatumia gari yako bila idhini yako unaweza ukafika ofisi za Uber viva towers ukatoa taarifa
 
Duuu kwamaana kwamba wew ukienda na driving licence yako na gari ya mtu yoyote unaingizwa kwenye system? No supportive documents za owner wa gari
Uber tupeni full info zinatakazosaidia na wengine
 
Uber imerahisisha sana maisha yangu

Nimetoka Ubungo stendi hadi Karume usiku wa saa saba kwa elfu nane
 
Eh sasa hapa maderava wakikosa wateja sio ndio watakapo tumia chance hii, yaani wata report kua mteja kanitoroka kumbe hakua na mteja wowote, au akamtumika rafiki yake na huyo rafiki akajifanya mkorofi wakati wa malipo kumbe ni deal Yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…