Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

hapo kwenye kusajir gari itumike kwa ajili ya uber mbona nilijaribu wanasema usajir wangu una shida tatizo nini hasa
 
Habari kama hii wa mikoani wanaugulia ndani kwa ndani.
niliijaribu nikiwa iringa nikaambiwa "sorry,this service is not yet available in your area" nikatoka ndukii[emoji125] [emoji125]
 
Juzi hapa nimetumia UBER kutoka buguruni hadi kkoo mida ya saa nne usiku hivi. Dereva alikuwa kadada flani karembo around 26yrs ana kaPasso kananukia vizurii.Njiani full story aisee,hadi sikutamani kushuka.

Akawa ananiambia yeye anafanya kazi ya Uber part time, akiwa anatoka kazini kwake ndo anapiga trips kadhaa then anarudi nyumbani.

Cha kushangaza nauli ikasoma buku tano tu
 
Mbona inanikatalia sasa hivi kulog in jamaan kwa no yangu nimeunstall app nimeinstall tena bado tu tatizo ni hilo
 
Hongera kutumia huduma za Uber, waambie na wengine tafadhali wajiunge
 
Ninachoomba uber,wafanye uwezekano:
1:Wakumkodishia gari,mtu aliyeko Dar,wakati nikiwa nje ya Dar.Kwa mfano naweza kusafari nje ya Dar,lakini familia yangu,mke ,watoto,baba,mama na wngineo wako Dar.
2.Uber iweke njia ya kuweza kupata gari anayotaka mteja.Kwa mfano mteja anataka Toyota wish,iwe inajionyesha kabla ya kuita gari.
 
Asante kwa maswali yako Mkuu
Swali No1.
Uwezekano wa kumkodishia mtu Dar wewe ukiwa nje ya Dar inawezekana kabisa, kwenye app ya Uber ukirequest usafiri kuna sehemu ya kujaza namba ya mtu mwingine atakayetumia usafiri endapo sio wewe utakayetumia.Ukishajaza namba yake yeye atatumiwa details zote kwenye simu yake(namba ya simu ya dereva;pia dereva nae atatumiwa namba ya huyo mtu automatically ili waweze kuwasiliana). Kitu cha muhimu inabidi ukiwa unarequest usafiri uandike kabisa mahali ambapo huyo mtu yupo manually.

Swali No2.
Unapoita usafiri, aina ya gari huwa inajionyesha.Mfano Toyota Wish,Vitz n.k.Lakini kwa sasa bado hatuna huduma ya kuchagua aina ya gari, magari yote yako katika category moja.Ila kwa hapo baadae category za magari zitaongezeka na mtu atapata choices mbalimbali za kuchagua.
 
kusema ukwlei madereva taxi wajipange sana... gari zao chafu
zinanuka sana
wana lugha mbaya haijawahi tokea
Mkuu asante sana ubarikiwe sana sana nimefanikiwa
 
Ni kweli usafiri wa UBER ni rahisi ukilinganisha na Taxis nyingine. Mfano kutoka Ubungo kwenda Airport kwa UBER ni 15,000; Taxis nyingine ni 25,000 mpaka 40,000 kutegemeana na unavyojua kuomba punguzo. Toka Ubungo mpaka Bottle majengo pacha ni 12,000 Taxis nyingine hapo ni 30,000 hivi
 
Hongera sana kutumia UBER mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…