Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

Hongera sana kutumia UBER mkuu
Inachukua muda gani kwa mtu mwenye gari kusajiliwa na UBER ili atoe huduma hivyo kwani namfahamu jamaa yangu mmoja ni zaidi ya mwezi sasa tangu afike ofisini kwenu asajili gari yake UBER, hamjampa jibu mpaka sasa
 
Kutoka Ubungo hadi Airport kwa Uber ni kati ya 15,000 hadi 17,000. Ukilinganisha na Taxi ya kawaida ni 25000 hadi 35,000
 
Inawezekana kuna baadhi ya vitu alikuwa hajakamilisha. Alipofika ofisini aliambiwa arudi baada ya muda gani? Ni vyema akafika ofisini tena, Viva towers Posta na nna uhakika atapewa maelezo ya kuridhisha kulingana na usajili wake
 
Kutoka Ubungo hadi Airport kwa Uber ni kati ya 15,000 hadi 17,000. Ukilinganisha na Taxi ya kawaida ni 25000 hadi 35,000.
Karibuni tutumie usafiri wa Uber, wenye gharama nafuu na salama zaidi
 
samahani sijaelewa hapo baada ya kufika(stop trip) itaonyesha nauli hii nauli ni tofauti na ile ya mwanzo inayoonekana kabla ya reqeust?
 
Mimi huwa namkodishia mtu. Mfano nipo kazini na nina mgonjwa Muhimbili anataka kurudi nyumbani, huwa nabadilisha pick up location na kuweka Muhimbili, halafu namlipa dereva kupitia MPESA. Nampa maelezo kwa simu. Kwa hiyo waweza fanya ukiwa popote.
Naunga mkono wazo la pili kwani unaweza kuwa na familia unaagiza gari kupitia UBER unaletewa Vitz.
 
samahani sijaelewa hapo baada ya kufika(stop trip) itaonyesha nauli hii nauli ni tofauti na ile ya mwanzo inayoonekana kabla ya reqeust?
Mara nyingi inakuwa ile ile au inaweza kuongezeka kidogo, kulingana na muda uliotumia kusafiri; mfano kukiwa na foleni sana basi nauli inaweza ikaongezeka kidogo; sio tofauti kubwa na ya mwanzoni. Mfano inaweza ikaonyesha 6000 na baadae ikawa 6800
 
Inachukua muda gani tangu mtu kuandikisha gari yake UBER mpaka kupata majibu? Nina mfano hai wa mtu ambaye amepeleka gari yake UBER ni zaidi ya miezi miwili hajapata majibu
 
Rav 4 kilitime 3door mpya inafaa kuwa uber!?
 
Ubber naipenda sana hasa kwa wafanyabiashara ni ngumu kuchorewa mchezo wa kuibiwa....nipo nairob naitumia mno na bei ni poa nikiwa dar pia naitumia inarahisisha mambo.....mpaka umigie dereva wako akudanganye woi hiyo dereva yupo karib na ulipo muda wote
 
 
Hongera sana mkuu, kutumia Uber
 
Teknolojia inaenda mbele, tusibaki nyuma wadau. Epuka kulipa gharama kubwa,Tumia Uber, ni rahisi,nafuu na salama.
 
Umeenda kwenye sherehe,club, au umechelewa kutoka kazini usiku; usiwe na wasiwasi toa simu yako fungua app ya Uber, na gari litakufata hapohapo ulipo,na kukufikisha uendapo kwa bei nafuu
 
Mkuu kuna ndugu yangu alijaribu kujisajili kama mteja wa Uber ila sasa baada ya kuingiza zile codes anaambiwa account iko disabled

Nini cha kufanya?
 
Mi nilipoipendeA hii program ni kwamba ata ukiwa na gari binafsi unaweza ukalitumia kupiga pesa mjini,,, na pia hauna kituo cha kupak pesa,, wewe popote tuu ulipo unapata notification ya mteja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…